Hela za matunzo ya mtoto ninazotuma, wanakula na jamaa yake

Hela za matunzo ya mtoto ninazotuma, wanakula na jamaa yake

Wewe unahusika kwa upande wa mtoto tu,mambo ya kumlipia pango yangemhusu huyo jitu lake,sitisha malipo ya pango,Kama msingejuana angeishije mpaka umlipie pango?mchukue mtoto Kama hataki waache usiwape matumizi na malipo ya pango akifulia atamleta tu
 
Haya nayo mapya...jukumu lako kumhudumia mtoto tu..huyo mzazi mwenzio umempa mtaji kashindwa kujiendeleza japo kibiashara kwasababu unamlemaza na anajua utampa kila atakacho.Wewe kuzaa nae isiwe chanzo akuelemee..na sielewi kwanini unamlipia nyumba??Au mchukue mwanao mlee uondoshe dhahma yote.
 
amchukue mwanae kwa misingi ipi hapo,hebu fafanua...kama mwanamke hajawahi kumuoa sio kwamba mtoto bado yuko na haki kwa mama zaidi?

Kiafrika na Tanzania mtoto ni wa baba...hayo unayosema yana apply ulaya na marekani...uoe usioe mtoto ni wa baba...ila akiwa below 7 ana haki ya kuishi na mama yake...

Hiyo ndio sheria kandamizi tulonayo...ila kwa tabia ya kuomba omba ya jinsia ya kike bado inatufaa...maana wanawake hata awe na uwezo utashangaa analia lia na ela za kumtunza mtoto
 
ha ha ha...eti kama unamuweka kama nyumba ndogo...ndio maana mkewe kawachukia...maana hata mimi sioni mantiki ya kumkodishia nyumba mzazi mwenzie kama si mchepuko....na ndio maana anakuwa na wivu....anatia timu muda wowote sababu nyumba ni yake...siamini kama hakuna uhusiano hapo...

mara nyingi ni vigumu kwa mtu kueleza jambo kwa upande wake akalieleza kama lilivyo bali wengi huwa tunapenda kuliweka katika mtizamo unaotuvutia tulinda sisi wenyewe tunaohadithia.

maisha ni magumu kuliko mtu ambaye hajawahi kupata shida maishani mwake na akahitaji msaada kutoka kwa watu wengine tena ambao hata hawana connection yoyote na pale wanaposhindwa kumsaidia anajisikiaje.

huyo mtu kama ulizaa naye makanke mlikuwa wapenzi, mbali na hilo yuko na mwanao.

msaidie kujitegemea lakini si kwa kumpa mtaji eti fanya biashara bali mfungulie biashara ambayo mwanzoni umfanye kama mfanyakzi wako umsimamie mpaka atapopata maarifa ya kuiendesha biashara ndio umwambie ni yake.

hii itamsaidia hata mwanao

kama unamuweka kama nyumba ndogo yako mueleze kuwa aachane na hao jamaa wengine lakini kama mahusiano yako na yeye ni kumlea mtoto tu basi unaweza kumuongoza kama unaona anamahusiano na watu ambao unahisi hawawezi kutoa malezi kwa mwanao lakini kubwa ni kumpatia security ya maisha kwani kwa kumpatia fedha kila mwezi mtu lazima afikirie kuwa hivi siku moja nikikosa hizi fedha itakuwaje.

kumsusia ni jambo ambalo kiukweli hutumii busara kwani fedha unayompa ni matunzo ya mwanao sasa mama kakuudhi unawasusa unadhani mtoto wako anaishije?

kwangu mimi huwa naamini naweza kukosana na mzazi mwenzangu na tukagombana lakini ugomvi huo siwezi kumnyima mzazi mwenzangu na mtoto wangu chakula au mahali pa kulala. naweza nisitishe mambo yasiyo ya muhimu katika maisha kama mazungumzo, mahusiano lakini sio chakula, tiba kama ni ugonjwa na sehemu ya kulala.
 
Huyo kashakufanya chanzo cha hela mkuu. Nenda umweleze wazwaz kwamba unataka kumchukua mwanao na kama hataki hautatoa hata shilingi tena. Nina uhakika ukikata hela atamleta mwenyewe
 
Jukumu lako ni kutunza mtoto. Hiyo ya kulipia nyumba inatoka wapi?
Mkeo alijua una mtoto toka awali. Kwa nini amkatae hapo kwako? Kaona udhaifu fulami kwako. Mwambie kama hamtaki mtoto aanze mbele. Kuwa Mwanaume.
Ufumbuzi ni kuchukua mtoto na kama huyo binti hataki sitisha huduma kwa maana ya hela za kula na kodi ya nyumba ambayo lazima isitishwe kwa vyovyote vile. Ada ya shule na nguo za shule ulipe /ununue mwenyewe.
 
Hayo mkuu ni mojawapo tu ya madhara ya dhambi ya zinaa,Mungu alijua yote hayo na mengine mengi yatatokea iwapo utazini,pole sana bado yanakuja sihayo pekee,Muombe Mungu akusamehe ili uweze kurudi kwenye mstari usijefanya linalofanana na hilo,ingawa mkono ukisha katika haurudi endelea tu kumtunza mwanao.
 
Kiafrika na Tanzania mtoto ni wa baba...hayo unayosema yana apply ulaya na marekani...uoe usioe mtoto ni wa baba...ila akiwa below 7 ana haki ya kuishi na mama yake...

Inategemea na kabila. Kwetu mtoto ni wa mama. Pia mtoto kuwa wa baba ni mfumo unaoweza kubadilika.
 
Inategemea na kabila. Kwetu mtoto ni wa mama. Pia mtoto kuwa wa baba ni mfumo unaoweza kubadilika.
Ok. Nimekupata...wewe utakuwa unatokea mikoa ya kusini ambako mwanamke ndio kichwa cha familia...hiyo sasa ni exceptional case...

Ila nikuulize kama mwanaume anaamia ukweni...mkiachana unatakiwa utunze mkeo na wana au mna assume mwenye kipato ni mke? Hii culture yenu ni very interesting..ntajafanyia ka research...

Ok. Nimekupata...wewe utakuwa unatokea mikoa ya kusini ambako mwanamke ndio kichwa cha familia...hiyo sasa ni exceptional case...

Sheria itabadilika wanawake wakiacha kujilemaza...as long as wanajirudsha nyuma mfumo dume ni saizi yetu
 
Tunakwepa lawama tu wanaume. . . . . .tujifunze sasa kuzaa zaa tu kisa unaweza kutunza sio sawa!!!

1. Why uzae na mwanake usiyeweza kuishi naye???!
2. Umezaa sawa kwa nini msiongee hilo na mwanamke unayemuoa kwa muktadha wa wewe kuishi na mwanao???!!
3. Umezaa na mwanamke unamtunza mwanao why usijiweke salama kisheria badala ya fadhila na maneno kama hivi??!!
4. Tukubali kubadilika sasa. . . . .Inawezekana tatizo liko kwetu zaidi kuliko kwao
 
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako mazuri, yana tija sana
Nimelazimika kusitisha huduma kwa mzazi mwenzangu kutokana na sababu nilizoeleza kwenye Uzi, na sitarudisha hizo huduma hadi tumepata mechanism itakayotumika bila shida mbeleni,

Option nayoipa kipaumbele ni kumchukua mtoto ili alelewe na mama yangu alieko mkoani arusha, si kwamba mke wangu kamkataa huyo mtoto ila kila mtu humu anajua tabia ya mke wake. Mm ni mtu mzima nisingependa kuanika mengi sipendi mtoto aje kupata shida kwangu, atakuja akiwa ameshajielewa na hataweza kuteswa kwa umri huo
Lakini kwa sasa atapata shida

Kama mzazi mwenzangu hatokubali option hii nitalipeleka kwenye vyombo husika kwa ufumbuzi zaidi
Kwa sasa mtoto ana miaka sita
 
Ungeutambulisha tu mchepuko kwa mkeo wajuane kama mke mdogo.
 
Ok. Nimekupata...wewe utakuwa unatokea mikoa ya kusini ambako mwanamke ndio kichwa cha familia...hiyo sasa ni exceptional case...

Ila nikuulize kama mwanaume anaamia ukweni...mkiachana unatakiwa utunze mkeo na wana au mna assume mwenye kipato ni mke? Hii culture yenu ni very interesting..ntajafanyia ka research...

Ok. Nimekupata...wewe utakuwa unatokea mikoa ya kusini ambako mwanamke ndio kichwa cha familia...hiyo sasa ni exceptional case...

Sheria itabadilika wanawake wakiacha kujilemaza...as long as wanajirudsha nyuma mfumo dume ni saizi yetu

chi hii inaendeshwa na sheria na taratibu za nchi wala sio sheria na taratibu za kabila fulani.
 
Mkuu nashukuru kwa mawazo yako mazuri, yana tija sana
Nimelazimika kusitisha huduma kwa mzazi mwenzangu kutokana na sababu nilizoeleza kwenye Uzi, na sitarudisha hizo huduma hadi tumepata mechanism itakayotumika bila shida mbeleni,

Option nayoipa kipaumbele ni kumchukua mtoto ili alelewe na mama yangu alieko mkoani arusha, si kwamba mke wangu kamkataa huyo mtoto ila kila mtu humu anajua tabia ya mke wake. Mm ni mtu mzima nisingependa kuanika mengi sipendi mtoto aje kupata shida kwangu, atakuja akiwa ameshajielewa na hataweza kuteswa kwa umri huo
Lakini kwa sasa atapata shida

Kama mzazi mwenzangu hatokubali option hii nitalipeleka kwenye vyombo husika kwa ufumbuzi zaidi
Kwa sasa mtoto ana miaka sita

Ok kaka nimekuelewa sana, . . .
1. Endelea na supportive measures interms of consumables and not cash. . . ili mtoto asikose mahitaji muhimu
2. Punguza mawasiliano na huyo mzazi mwenzio especially physical mpaka kuwe na umuhimu wa kufanya hivyo. . . . . acha kwenda kwake mara kwa mara
3. Ongea naye tena na tena umuhimu wa mtoto kulelewa na mama yake na umuweke wazi kuwa unataka iwe hivyo kwa faida ya mtoto wenu ila pia ikiwa ngumu utamuondoa mtoto mara ifikapo muda wa kisheria
4. Mzazi mwenzio maadam anajua uwepo wa huyo mtoto hawezi sumbua huyo mtoto akiwa hamtegemei, fight kiuchumi na Mungu akujaalie uweze kuwatunza wote sawa, shemeji hawezi kuwa na ghubu kama unatunza watoto na yeye kwa kadiri ya uwezo wako

All the best son
 
Wanaume tunatofautiana kweli!,mkeo anakataa kukaa na mtoto wako ambae alikukuta nae?na si kwamba ulimpata ukiwa nae?...chukua mwanao wewe jamaa uishi nae,acha blah blah.
 
Wakuu,

Kuna binti nilizaa nae mtoto miaka kadhaa iliyopita kabla sijaoa kwa bahati mbaya uhusiano huo haukuweza ku materialise kufikia ndoa nikawa nimeoa mwanamke mwingine yeye hajaolewa hadi sasa nimempangia upande wa nyumba anaishi hapo na mtoto wetu. Tumekua tukisumbuana sana na huyu binti kuhusu matunzo ya mtoto kwa muda mrefu amekua na matumizi mabaya ya pesa nikimpa hela leo siku mbili mbele anaomba tena wakati mtoto anakula shuleni milo miwili jioni ndo anakula nyumbani yeye nimempa mtaji mara kadhaa afanye biashara mtakuja unakatika.

Juzi nimeenda kumuona mtoto nashangaa kulikuta jitu lake hapo, lililala hapo kwenye nyumba ninayoilipia mm na linakula hapo hapo chakula changu, gaya niliambiwa na house girl ninaemlipa mimi mshahara, hii ni kama familia yangu ya pili ninaigharamia kila kitu sasa wakuu hili jamaa lina haki gani ya kuja kula na kulala hapo?

Nikimuuliza mzazi mwenzangu huyo jamaa haishi hapo huwa anakataa anasema anakuja na kuondoka ila mi nina uhakika analalaga hapo Juzi binti kanisumbua wameishiwa hela nikadhani wana emergency nikawatumia laki mbili cha kushangaza usiku wa tatu nikapita pale nikamkuta housegirl na mtoto tu, kumuuliza kulikoni mbona mpo peke yenu akanijibu mama na jitu lake wameenda FM academia iliyokua imekuja kutumbuiza bar ya hapo mtaani.

Ndipo nikagundua laki mbili yangu ndio inayotumika huko maana jitu lake halina kazi na yeye hana kazi.Nikamfuata huko bar nikamtumia sms akatoka nje nilipomuhoji alikua amechangamka na bia akaniporomoshea Maneno makali kwamba namfuatilia sana, kwamba nisimtishe na hicho ki laki mbili nikamuacha nikaondoka zangu.

Tangu siku hiyo nimekata mawasiliano anapiga simu asubuhi hadi jioni sipokei, anatuma sms za kuomba msamaha sizijibu maana nimeshachoka nae sasa wakuu nimekosea kwa uamuzi huu? Pia nauliza nitumie utaratibu gani kuendelea mbele ya safari? Maana nimetaka kumchukua mtoto mara kadhaa lakini mama yake hataki anataka kukaa nae
mke wangu pia huonyesha kukereka ninapomzumzia huyo mtoto hivyo nikapata picha hapendi aje kuishi na sisi.

Nasikitika kulikuta jitu kwenye nyumba niliyonunua, kwenye makochi niliyonunua, kwenye TV niliyonunua mimi limeweka nne likiwa na remote mkononi bila hata aibu halafu halinisalimii. Nitakuja kulitimua humo siku moja.

Msaada wenu please, nishaurini nifanyeje wadau
Huna akili
 
Back
Top Bottom