Hela za matunzo ya mtoto ninazotuma, wanakula na jamaa yake

Hela za matunzo ya mtoto ninazotuma, wanakula na jamaa yake

...Tumekua tukisumbuana sana na huyu binti kuhusu matunzo ya mtoto kwa muda mrefu amekua na matumizi mabaya ya pesa nikimpa hela leo siku mbili mbele anaomba tena wakati mtoto anakula shuleni milo miwili jioni ndo anakula nyumbani.

Mtoto huyo ana umri gani?

Badala ya kutoa fedha za matunzo jaribu kubadilisha namna ya kutoa matunzo kwa mwanao...

Nunua mahitaji yote muhimu ya mtoto kuanzia chakula, mavazi na vifaa vya shule na uvipeleke hivyo kwa mzazi mwenzio...

Fungua akaunti maalumu na fedha zote za matumizi ya mwanao hifadhi huko na hizo ziwe ni akiba na si za matumizi ya kila siku...
 
Huu sasa ni wivu...

Wewe si uliachana na huyo mwanamke?

Mbona sasa wataka kumpangia namna ya kuenenda katika mahusiano yake?

Kitu kibaya labda utuambie kuwa uwepo wa huyo jamaa unamuathiri vipi mtoto au unamuhatarisha vipi mtoto...

La hasha kijana unachofanya ni wivu hata kama pango walipa wewe...

Juzi nimeenda kumuona mtoto nashangaa kulikuta jitu lake hapo, lililala hapo kwenye nyumba ninayoilipia mm na linakula hapo hapo chakula changu...

Nikimuuliza mzazi mwenzangu huyo jamaa haishi hapo huwa anakataa anasema anakuja na kuondoka ila mi nina uhakika analalaga hapo
 
Wakuu,

Kuna binti nilizaa nae mtoto miaka kadhaa iliyopita kabla sijaoa kwa bahati mbaya uhusiano huo haukuweza ku materialise kufikia ndoa nikawa nimeoa mwanamke mwingine yeye hajaolewa hadi sasa nimempangia upande wa nyumba anaishi hapo na mtoto wetu. Tumekua tukisumbuana sana na huyu binti kuhusu matunzo ya mtoto kwa muda mrefu amekua na matumizi mabaya ya pesa nikimpa hela leo siku mbili mbele anaomba tena wakati mtoto anakula shuleni milo miwili jioni ndo anakula nyumbani yeye nimempa mtaji mara kadhaa afanye biashara mtakuja unakatika.

Juzi nimeenda kumuona mtoto nashangaa kulikuta jitu lake hapo, lililala hapo kwenye nyumba ninayoilipia mm na linakula hapo hapo chakula changu, gaya niliambiwa na house girl ninaemlipa mimi mshahara, hii ni kama familia yangu ya pili ninaigharamia kila kitu sasa wakuu hili jamaa lina haki gani ya kuja kula na kulala hapo?

Nikimuuliza mzazi mwenzangu huyo jamaa haishi hapo huwa anakataa anasema anakuja na kuondoka ila mi nina uhakika analalaga hapo Juzi binti kanisumbua wameishiwa hela nikadhani wana emergency nikawatumia laki mbili cha kushangaza usiku wa tatu nikapita pale nikamkuta housegirl na mtoto tu, kumuuliza kulikoni mbona mpo peke yenu akanijibu mama na jitu lake wameenda FM academia iliyokua imekuja kutumbuiza bar ya hapo mtaani.

Ndipo nikagundua laki mbili yangu ndio inayotumika huko maana jitu lake halina kazi na yeye hana kazi.Nikamfuata huko bar nikamtumia sms akatoka nje nilipomuhoji alikua amechangamka na bia akaniporomoshea Maneno makali kwamba namfuatilia sana, kwamba nisimtishe na hicho ki laki mbili nikamuacha nikaondoka zangu.

Tangu siku hiyo nimekata mawasiliano anapiga simu asubuhi hadi jioni sipokei, anatuma sms za kuomba msamaha sizijibu maana nimeshachoka nae sasa wakuu nimekosea kwa uamuzi huu? Pia nauliza nitumie utaratibu gani kuendelea mbele ya safari? Maana nimetaka kumchukua mtoto mara kadhaa lakini mama yake hataki anataka kukaa nae
mke wangu pia huonyesha kukereka ninapomzumzia huyo mtoto hivyo nikapata picha hapendi aje kuishi na sisi.

Nasikitika kulikuta jitu kwenye nyumba niliyonunua, kwenye makochi niliyonunua, kwenye TV niliyonunua mimi limeweka nne likiwa na remote mkononi bila hata aibu halafu halinisalimii. Nitakuja kulitimua humo siku moja.

Msaada wenu please, nishaurini nifanyeje wadau

Cha kwanza kapime DNA cha pili hiyo ishu ukienda ustawi wa jamii huyo mama ananyang'anywa huyo mtoto bila ya huruma coz anamuharibia future huyo dogo.
 
Pole sana.Chukua mtoto kama ana umri wa miaka 7. Otherwise report hiyo issue Ustawi na muandikiane kiasi cha matunzo ya mtoto. Masuala ya kodi ya pango sitisha!
 
Khaaaaaaa

Umeyataka yaani hadi nyumba umlipie?????

Yaani ungelipa ada ya shule na laki 2 tu kila mwezi...

Umejigeuza atm

Halafu yupo sahihi acha kumfuatafuata....... na unamfuata fuata kwa kiherehere chako cha kulipa kodi ya nyumba kununua tv makochi na kumlipa housegirl
 
Samahani Kaka, nimeshindwa kusoma lote,
Ukituma hela mama anavyotumia,
je, mtoto analala njaa??
 
Hapa suluhisho ni kukaa na mkeo kumuomba akuruhusu umchukue mwanao. Sioni kwanini akatae kumchukua huyu mtoto ilhali ulimpata kabla ya kuwa naye.

Huyo mke halali hamchukui ng'o!!!
Walishakosea mwanzoni na akilazimisha huyo mke mnamtafuta ubaya na hamumtakii mema huyo mtoto
 
Dawa mpeleke kwa mamayako, utatuma matumizi huko na ataishi vzr
 
Mkuu unatumika kama kitega uchumi kwa kisingizio cha mwanao aliye naye, suluhisho ni kumchukua huyo mtoto toka kwa huyo mama, usipochukua hatua utaendelea kuchunwa. Ila unaonekana una ka wivu fulani mwachie huyo mwanaume mwenzio asuuze rungu hapo!!
 
Ndio hapo wakati mwingine baadhi ya wake huonekana wana roho mbaya. Mtoto hana kosa, mume hana kosa alimpata kabla ya kukutana na mkewe. Anamuona mwenzie anavyohangaika na kukosa raha kuhusu mtoto wake na si ajabu kukosa raha kwa mume kunamuathiri mke pia indirectly. Mke mwenye uelewa mkubwa angemchukua huyu mtoto na kumleta kama wakwake.

Huyo mke halali hamchukui ng'o!!!
Walishakosea mwanzoni na akilazimisha huyo mke mnamtafuta ubaya na hamumtakii mema huyo mtoto
 
Wakuu,

Kuna binti nilizaa nae mtoto miaka kadhaa iliyopita kabla sijaoa kwa bahati mbaya uhusiano huo haukuweza ku materialise kufikia ndoa nikawa nimeoa mwanamke mwingine yeye hajaolewa hadi sasa nimempangia upande wa nyumba anaishi hapo na mtoto wetu. Tumekua tukisumbuana sana na huyu binti kuhusu matunzo ya mtoto kwa muda mrefu amekua na matumizi mabaya ya pesa nikimpa hela leo siku mbili mbele anaomba tena wakati mtoto anakula shuleni milo miwili jioni ndo anakula nyumbani yeye nimempa mtaji mara kadhaa afanye biashara mtakuja unakatika.

Juzi nimeenda kumuona mtoto nashangaa kulikuta jitu lake hapo, lililala hapo kwenye nyumba ninayoilipia mm na linakula hapo hapo chakula changu, gaya niliambiwa na house girl ninaemlipa mimi mshahara, hii ni kama familia yangu ya pili ninaigharamia kila kitu sasa wakuu hili jamaa lina haki gani ya kuja kula na kulala hapo?

Nikimuuliza mzazi mwenzangu huyo jamaa haishi hapo huwa anakataa anasema anakuja na kuondoka ila mi nina uhakika analalaga hapo Juzi binti kanisumbua wameishiwa hela nikadhani wana emergency nikawatumia laki mbili cha kushangaza usiku wa tatu nikapita pale nikamkuta housegirl na mtoto tu, kumuuliza kulikoni mbona mpo peke yenu akanijibu mama na jitu lake wameenda FM academia iliyokua imekuja kutumbuiza bar ya hapo mtaani.

Ndipo nikagundua laki mbili yangu ndio inayotumika huko maana jitu lake halina kazi na yeye hana kazi.Nikamfuata huko bar nikamtumia sms akatoka nje nilipomuhoji alikua amechangamka na bia akaniporomoshea Maneno makali kwamba namfuatilia sana, kwamba nisimtishe na hicho ki laki mbili nikamuacha nikaondoka zangu.

Tangu siku hiyo nimekata mawasiliano anapiga simu asubuhi hadi jioni sipokei, anatuma sms za kuomba msamaha sizijibu maana nimeshachoka nae sasa wakuu nimekosea kwa uamuzi huu? Pia nauliza nitumie utaratibu gani kuendelea mbele ya safari? Maana nimetaka kumchukua mtoto mara kadhaa lakini mama yake hataki anataka kukaa nae
mke wangu pia huonyesha kukereka ninapomzumzia huyo mtoto hivyo nikapata picha hapendi aje kuishi na sisi.

Nasikitika kulikuta jitu kwenye nyumba niliyonunua, kwenye makochi niliyonunua, kwenye TV niliyonunua mimi limeweka nne likiwa na remote mkononi bila hata aibu halafu halinisalimii. Nitakuja kulitimua humo siku moja.

Msaada wenu please, nishaurini nifanyeje wadau

Enzi hizo haya yalinikuta mkuu, ila mimi nikawa mjanja kiasi, nilikuwa namsainisha kitabuni kila alipokuwa achukuwa hela ya matumizi ya mtoto, sasa siku nilipoona kwamba natumiwa kama ATM nikakata kutoa tena hela, akakimbilia ustawi wa jamii, nikaitwa, nikaenda na nikasikiliza mashitaka. Nilichokifanya ni kuwapa kile kitabu. Walishangaa na kumwambia kwamba hakuwa na akili kwani katika kesi zoote zilizokuwa zinafikishwa pale hakuna mwanaume aliyekuwa anatoa hata robo niliyokuwa nimetoa mm. Walishauro na kumlazimisha nimchukuwe mtoto. Nikampleleka kwa mama (bibi yake).
 
Nakushaur uende ustawi wa jamii wakupe haki zakumchukua huyo mtoto akakake kwa wazazi wako.,,
 
Hahahahaaaaaaaaaaaaa! Na linavohonga hilo jitu, toto lako linakula vilevile. Mambo kusaidiana au umesahau kama watanzania wote ni ndugu!:becky:. Mpende ndugu yako Jitu bwana, usiwe hivo.

Haa haa yani wewe lara wewe duuuh! Ila nyie wanawake ni pasua kichwa kabisa. Sema jamaa naye asingetakiwa kumlipia kodi atoe matunzo ya mtto tuu.
 
Hahaa kwa maelezo yako bado unampenda huyo zilipendwa wako.. huwez ukawa na wivu nae kias hiko kha!! kwahyo kawsbbu unawahudumia bas dada aruhusiw kuwa na mtu mwngne tn! na wakat wew umeshaoa, unatarajia nae hataolewa?! atakaa aishi kwa misaada yako mpk lin!! Anahitaji mume nae. Na mkeo hatak kuckia habar za mtto maana anaona jins unavyoendelea kuhangaika na mama ake mtto, Tunza mtoto ikishndikana mpeleke kwa bibi
 
Back
Top Bottom