Hela yangu ni yetu na hela yake ni yake?

Kiluuj

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
692
277
Wakuu mpo?

Siku nyingi ila nipo nang'ang'ana na maisha.
Nimeoa na nimejaliwa watoto wawili. Nimeajiriwa na moja ya NGOs muhimu nchini. Hii inamaana naikimu familia vizuri.

Mke wangu naye nimemfungulia biashara anayoindesha na wala siingilii hata kidogo. Sababu yangu kuu ya kumfungulia biashara ni hili aweze kunisaidia kuiinua familia yetu juu juu zaidi. Hili halifanyiki.

Nimekuwa nikilipia kila kitu hata yuko radhi asitumie gari nililomnunulia endapo litaisha mafuta muradi tu asitumie hela yake!
Yaani kila kitu nyumbani ninagharamia kuanzia mavazi yake, watoto hadi kibiriti nikijua ni jukumu langu.

Wakuu, nianze kuingilia hiyo biashara ama hela yangu ni yetu na yake ni yake peke yake!?
 
huo ndio uanaume sasa. wakati hana biashara alikuwa anachangia nini? punguza complication ndoa yako itadumu
 
Ndio uanaume huo.....
Hebu lea familia....
Anyway mkeo hajawahi nunua hata chumvi?
Kununuoia watu wa kwenu na kwao?
 
huo ndio uanaume sasa. wakati hana biashara alikuwa anachangia nini? punguza complication ndoa yako itadumu
Acha ujinga wewe! Biashara kafunguliwa na nani? Angekuwa kafungua kwa nguvu zake au wazazi wake sawa hela haimhusu jamaa ila hela ya biashara ni ya jamaa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maana ya ndoa ni watu wawili waliopendana na kuamua kuishi pamoja kama mwili mmoja.........
Kwa mantiki hii ya ndoa....ni kuwa wanandoa wanatakiwa wawe kitu kimoja katika kila hali za nyakati kwenye maisha yao yote......

Ushirikiano huo unaendelea hadi kwenye hadi kwenye masuala yanayohusu ujenzi wa familia nikiwa na maana kila mmoja atimizie wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake....lengo ni kuijenga ndoa na mafanikio yake kwa manufaa ya wote......

Kitendo cha mwanandoa kuanza kujifikiria yeye kama yeye badala ya mumewe au mkewe kinaleta mpasuko na ufa mkubwa sana kwenye ndoa.....ambayo hupelekea kuzaliwa hali ya wasi wasi na kutoaminiana kwenye ndoa.....

Kama hali hiyo isipotafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo inaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa.......

Busara na hekima inatakiwa katika maisha ya ndoa.....
 
hahahahaha hivi mnavyoambiwa kuoa ujipange nyie mwadhani ndoa ni kupapata papuchi tuu.

ukitaka kufurahia ndoa kaka yangu gundua kuwa mwanamke hela ni ya kwake kujiremba basi. mambo yote ya msingi yanayohusu nyumba nini wewe mwanaume. hapo wala huna shida.
tambua hili. jukumu la mwanamke ni kugegedwa, kuzaa na kulea watoto. suala la kufungulia biashara au yeye kufanya kazi ni kiherehere chetu sie wanaume.
 
Kwenye ndoa hakuna cha huyu wala cha yule, kuna cha kwetu. Na hayo yanafundishwa mapema kabisa kabla hamjafunga ndoa labda ziwe ni ndoa hizi za mwendi kasi. na nI jukumu lenu kuweka mifumo itakayosaidia kukitambulisha kila mlichonacho kama cha kwenu. Anza sasa, hujachelewa.
 
Labda anatuma hela kwao huyo.

Hata kumhudumia mtoto wake?

Huyo si msaidizi wako kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Maana ya ndoa ni watu wawili waliopendana na kuamua kuishi pamoja kama mwili mmoja.........
Kwa mantiki hii ya ndoa....ni kuwa wanandoa wanatakiwa wawe kitu kimoja katika kila hali za nyakati kwenye maisha yao yote......

Ushirikiano huo unaendelea hadi kwenye hadi kwenye masuala yanayohusu ujenzi wa familia nikiwa na maana kila mmoja atimizie wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake....lengo ni kuijenga ndoa na mafanikio yake kwa manufaa ya wote......

Kitendo cha mwanandoa kuanza kujifikiria yeye kama yeye badala ya mumewe au mkewe kinaleta mpasuko na ufa mkubwa sana kwenye ndoa.....ambayo hupelekea kuzaliwa hali ya wasi wasi na kutoaminiana kwenye ndoa.....

Kama hali hiyo isipotafutiwa ufumbuzi mapema iwezekanavyo inaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa.......

Busara na hekima inatakiwa katika maisha ya ndoa.....
Kimsingi ulivoeleza ndivyo ndoa inatakiwa iwe. Wanaume tunatimiza wajibu wetu wa kuhakikusha kuwa kila tunachokichuma kinakuwa ni mali ya familia, cha ajabu ni kuwa akichumacho mwanamke anataka kiwe chake peke yake!! Dhulma hii lazima watailipa siku ya kiyama hawa wanawake maana wamegeuka kuwa kupe.
 
Back
Top Bottom