Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
3) Tuache bajeti tegemezi, tuache kutegemea wafadhili
4) Tufungue viwanda vingi sisi wenyewe, tujifunze ku-export ready made material, na siyo rawa materials,
5) Wananchi wanunue bidhaa za ndani , zilizotengenezwa humu humu, baada ya point ya nne kufanyika. viwanda vya ndani vitengenezewe mazingira mazuri ya kushindana na vya nje, to my surprise serikali wanapigana usiku na mchana kuweka mazingira mazuri kwa wageni!
6) point ya 4,5 ikishafikiwa, tuhamasishe matumizi ya fdha yetu ambayo inacirculate humu humu, kiasi ambacho itaongeza thamani ya fedha nje ya nchi.
inatokana na kuwa we have no say about our economy! piga ua!
when you talk about donors, katika nchi yenye kila sababu ya kuendelea yenye, maliasili za kumwaga, when you talk about them, you are confirming that, all these issues of inflation, or whatever may be Tanzania is not a country to talk about! we are exporting raw materials mkuu, thats wrong very very wrong.
waberoya
Waberoya:
Vitu ulivyosema vinawezekana kabisa kuvifanya lakini vinaweza kusababisha Social Upheaval kitu ambacho wanasiasa na nchi zilizoendelea hawataki kukiona kinatokea.
Kama bajeti yetu inategemea misaada kwa asilimia 40, ina maana wahisani wakiacha kutoa misaada basi serikali inashindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake na kutoa huduma zingine kwa jamii.
Na serikali kushindwa kulipa mishahara kutaambatana na vurugu za kijamii ambazo zinaweza kufanya serikali ianguke na kusababisha matatizo yenye mfano wa Somalia.
Hakuna mwanasiasa ambaye anataka kuongoza nchi huku kukiwa na vurugu. Hata Nyerere mwenyewe hakuweza kukwepa misaada maana bila ya misaada hakuna ambaye angempa sikio la siasa za ujamaa.
Kwa mtaji huo haitoshi kusema kuwa sisi tuna maliasili za kutosha. Kinachotakiwa ni Innovative Approaches ya nchi kutoka kwenye misaada na madeni bila kusababisha matatizo ya kijamii.
Katika post yangu moja nilisema kipindi cha sasa ni kizuri kujifunza na kupata expertise kwa sababu tunaona jinsi gani nchi kama Marekani inavyoweza kutumia tools za kiuchumi kutatua matatizo yake. Hizi tools ni Innovative Approaches. Kwa mfano wana bail out makampuni, wanamwaga stimulus package baadaye wataingia kwenye fiscal responsibility.
I am curious na kitu kimoja kuhusu matatizo ya uchumi dunia yanayotokea sasa. Je watanzania tunawatizama wenzetu wanavyopambana na matatizo yao na wakifanikiwa tuendelee kuwaomba misaada au na sisi tunajifunza vitu fulani?
Hypothetically ningependa mtu atueleze katika kipindi cha miaka mitano zitumike Innovative Approaches zipi kuondoa misaada bila kushusha standard of living ambayo watanzania wanayo sasa.