Hawa jamaa wana ratiba nyingi mpaka basi! Wakati mwingine tuwaache tu. Kwanza ni viumbe wenye tamaa sana! Yaani akiona kitu halafu akakipenda, basi ni lazima tu atakinunua. Wana mahitaji mengi sana kuliko sisi wanaume! Mfano kwenda saluni, kupaka rangi na kusafisha kucha, nk.
Ni watoaji wazuri wa sadaka kwa Manabii na Wachungaji uchwara ukilinganisha na sisi wanaume! Wana vikundi vingi vya kukopeshana na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe!
Ni wepesi sana kwenye kusaidia familia zao mfano baba na mama zao, ndugu zao, nk zitokeapo changamoto za kifedha, au shida fulani nyumbani ukilinganisha na sisi.
Wanawake wengi hupenda kuishi na akiba ya fedha ndani ili ziwasaidie wakati changamoto zinapotokea nyumbani, tofauti kabisa na sisi wanaume ambao wengi hatupendi kuweka akiba. Hivyo unaweza kushangaa hela iko wapi, kumbe ameweka akiba sehemu ambayo kamwe mwanaume huwezi kuigundua.
Hao ndiyo wanawake bhana tunao takiwa kuishi nao kwa akili sana.