Heko waraka wa Elimu

NANDERA

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
2,024
2,486
Nikiwa na imani kuwa waraka huu wa elimu 2020 ni wa kweli, ninapenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa serikali kwa kuonesha nia ya dhati ya kujali ustawi wa watoto wake. Unyanyasaji wa watoto hasa kwa shule za binafsi umekithiri sana. Watoto hasa wanaoitwa wa madaraasa ya mitihani wamekuwa wakibaki mashuleni baada ya saa 9 au kulazwa mabwenini ili kukaririshwa. Wale wasiokaa mabwenini wanarudi usiku wakati mwingine mpaka saa 2 usiku.

Wakirudi ni kuoga, kula, kupanga vitabu na madaftari ya kesho na kulala na kuamkia shule. Mbaya zaidi hata huko shule wanafunzi wa madarasa ya mitihani hawashiriki vipindi vya ziada kama michezo. Ni kukariri na kukaririshwa. Hawapati muda wa kufua hata vest nyumbani wala kusaidia kufagia. Wakati mwingine wanalala na vyakula mdomoni.

Hakuna muda wa kukuza karama zao wala kuwapatia maarifa ya ziada. Mafundisho ya dini imekuwa kazi kweli kweli. Wazazi ngangari kidogo wanakomaa wanawapeleka watoto mafundisho Jumamosi. Wale waoga wanawapeleka shule. Makuzi ya kiroho yanaathirika kwa sababu pamoja na kwamba taasisi za dini siyo pekee za kutunza mtoto kiroho, nyumbani hili swala linakuwa gumu.

Hatufanyi sala za kueleweka asubuhi maana saa 11 tumeshaamka saa nyingi tunakimbizana tusiachwe na skulubasi. Jioni ni majaliwa.

Kuna watoto wamesherehekea Krismasi mashuleni kwa jina la pre-form one!! Shule za binafsi zimeanzisha huu upuuzi ili kujihakikishia wateja na kunyonya wazazi. Pre-form Disemba!

Hawa wa darasa la 7 wakati wenzao wanapumzika mwezi mzima, wao wanapumzika wiki 2 na kisha kuanza masomo ya darasa la 7 mwezi wa 12 ili eti ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza kazi ibaki "kusovu" maswali.

Ni vululuvululu tu. Watoto hawaonani na jirani zao wala ndugu. Ni shule, shule na wao. Kuna siku nilikuwa ninaongea na mwanangu mazungumzo ya kawaida tu. Nikamuuliza ni vitu gani hupendi? Alijibu "cha kwanza ni shule!" Nikajiuliza kama huyu mtoto ambaye hajipindi sana kupata A anachukia shule, vipi wale wa uwezo wa kati na wa chini ambao wanawekewa matarajio makubwa kupita kiasi na walimu wao? Haya ni baadhi ya matatizo. Yako mengi.

Pia najua si shule zote zinanyanyasa watoto kwa namna hizi nilizotaja. Pia sijaelezea madhila yanayowapata wazazi maana ukiukaji huu wa ratiba unawaathiri kijamii na kiuchumi.

Nitoe wito kwa wazazi tunaopenda watoto wetu na tunaojali mustakabali wa taifa tuungane na serikali kutekeleza huu waraka. Shule ni sehemu ya mtoto kufurahia maisha.

Wale wazazi ambao huwa mnatuzomea kwenye mikutano ya shule kwa sababu hamtaki kulea wanenu nyumbani pia tuungane katika hili.

Watoto siyo punda ni binadamu. Wanahitaji kiasi katika mambo yote. Tuwapende watoto kwa kuwapumzisha na shule mwisho wa wiki na sikukuu, tuwapende watoto wetu kwa kuwatambulisha maarifa ya tofauti na darasani, tuwapende watoto wetu wa kuwafundisha kujitegemea kwa vitendo nyumbani, tuwapende watoto wetu kwa kuwajumuisha na watoto wenzao, tuwapende watoto wetu kwa kuwaacha wajiachie kucheza n.k

SAIDIA MTOTO APATE ELIMU RASMI KWA USAHIHI
 
Lakini ndio wanaopasua huo mtihani unaoandaliwa na watoa waraka. Mtihani huo ukiwapeleka wanafunzi kama keki ya harusi sidhani kama watakuwa na ufaulu wa juu. Japo zipo case chache kama za yule dogo aliyepiga wani ya saba. Pamoja na hayo sipingi watoto kupumzishwa ni haki yao kama ambavyo sera ya elimu inavyotaka
 
Education should expose wanafunzi kwa vitu mbalimbali ili wawe well rounded individuals. Rest and extra curricular activities ni very important.

Ila kwa vile shule nyingi zimekalia ufaulu at all costs(for business reasons). Wanaishia kutengeneza cramming machines badala ya well rounded students.
 
Hautekerezeki kwani ukiangalia idadi ya masomo na mda hauwezi kumuandaa mtoto awe amemaliza topic zote na awe tiyar kufaulu mtihan. Hii ni kwasababu necta hutunga mda zote hsijalish umemaliza au la sasa kama hamna remidial hakuna wa kufaulu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa na imani kuwa waraka huu wa elimu 2020 ni wa kweli, ninapenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa serikali kwa kuonesha nia ya dhati ya kujali ustawi wa watoto wake. Unyanyasaji wa watoto hasa kwa shule za binafsi umekithiri sana. Watoto hasa wanaoitwa wa madaraasa ya mitihani wamekuwa wakibaki mashuleni baada ya saa 9 au kulazwa mabwenini ili kukaririshwa. Wale wasiokaa mabwenini wanarudi usiku wakati mwingine mpaka saa 2 usiku.

Wakirudi ni kuoga, kula, kupanga vitabu na madaftari ya kesho na kulala na kuamkia shule. Mbaya zaidi hata huko shule wanafunzi wa madarasa ya mitihani hawashiriki vipindi vya ziada kama michezo. Ni kukariri na kukaririshwa. Hawapati muda wa kufua hata vest nyumbani wala kusaidia kufagia. Wakati mwingine wanalala na vyakula mdomoni.

Hakuna muda wa kukuza karama zao wala kuwapatia maarifa ya ziada. Mafundisho ya dini imekuwa kazi kweli kweli. Wazazi ngangari kidogo wanakomaa wanawapeleka watoto mafundisho Jumamosi. Wale waoga wanawapeleka shule. Makuzi ya kiroho yanaathirika kwa sababu pamoja na kwamba taasisi za dini siyo pekee za kutunza mtoto kiroho, nyumbani hili swala linakuwa gumu.

Hatufanyi sala za kueleweka asubuhi maana saa 11 tumeshaamka saa nyingi tunakimbizana tusiachwe na skulubasi. Jioni ni majaliwa.

Kuna watoto wamesherehekea Krismasi mashuleni kwa jina la pre-form one!! Shule za binafsi zimeanzisha huu upuuzi ili kujihakikishia wateja na kunyonya wazazi. Pre-form Disemba!

Hawa wa darasa la 7 wakati wenzao wanapumzika mwezi mzima, wao wanapumzika wiki 2 na kisha kuanza masomo ya darasa la 7 mwezi wa 12 ili eti ifikapo mwisho wa muhula wa kwanza kazi ibaki "kusovu" maswali.

Ni vululuvululu tu. Watoto hawaonani na jirani zao wala ndugu. Ni shule, shule na wao. Kuna siku nilikuwa ninaongea na mwanangu mazungumzo ya kawaida tu. Nikamuuliza ni vitu gani hupendi? Alijibu "cha kwanza ni shule!" Nikajiuliza kama huyu mtoto ambaye hajipindi sana kupata A anachukia shule, vipi wale wa uwezo wa kati na wa chini ambao wanawekewa matarajio makubwa kupita kiasi na walimu wao? Haya ni baadhi ya matatizo. Yako mengi.

Pia najua si shule zote zinanyanyasa watoto kwa namna hizi nilizotaja. Pia sijaelezea madhila yanayowapata wazazi maana ukiukaji huu wa ratiba unawaathiri kijamii na kiuchumi.

Nitoe wito kwa wazazi tunaopenda watoto wetu na tunaojali mustakabali wa taifa tuungane na serikali kutekeleza huu waraka. Shule ni sehemu ya mtoto kufurahia maisha.

Wale wazazi ambao huwa mnatuzomea kwenye mikutano ya shule kwa sababu hamtaki kulea wanenu nyumbani pia tuungane katika hili.

Watoto siyo punda ni binadamu. Wanahitaji kiasi katika mambo yote. Tuwapende watoto kwa kuwapumzisha na shule mwisho wa wiki na sikukuu, tuwapende watoto wetu kwa kuwatambulisha maarifa ya tofauti na darasani, tuwapende watoto wetu wa kuwafundisha kujitegemea kwa vitendo nyumbani, tuwapende watoto wetu kwa kuwajumuisha na watoto wenzao, tuwapende watoto wetu kwa kuwaacha wajiachie kucheza n.k

SAIDIA MTOTO APATE ELIMU RASMI KWA USAHIHI
IMG-20200208-WA0002.jpeg

I see ndugu NANDERA umesema kweli, unesema ya moyoni mwangu. Wengi watakupinga lakini simamia kweli daima. Ubarikiwe na usitetereke
 
Lakini si utashi wa mzazi kumpeleka mtoto huko? Huku kwetu st kayumba hayo huwa hayapo ni mwendo wa kupunzika bila bugudha...shuleni saa moja unusu asubuhi na saa nane unusu anatoka anaenda zake kuchunga mbuzi, kuchota maji na kutafuta kuni...december yuko msituni anatengeneza mkaa wa kuwauzia matajiri wa mjini ili wapate mkaa wa kupikia pilau la sikukuu..ili na yeye apate pesa kidogo ya kujinunulia nguo za krisma na mwaka mpya alafu na matumizi yake madogo baada ya kufungua shule...mlete mwanao st Kayumba hutojuta mzazi
 
  • Thanks
Reactions: K11
Waraka huo uende sambamba na kufuta mitihani yote ya kiroboti (kupima kumbukumbu), badala ya kupima uelewa na utambuzi, najua mitihani ya kupima uelewa na utambuzi ni gharama kubwa, lakini mtaka cha uvunguni sharti ainame.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom