Hekima za shaaban robert kuhusu ujana

Jan 4, 2012
61
23
Ebu vijana wa zamani na wa sasa tujikumbushe kuhusu UJANA. Soma shairi la Shaaban Robert alilotunga miaka ya 50 lakini hekima zake zadumu mpaka ukamilifu wa dahari.

UJANA

1. Ujana kitu kitamu, tena ni azizi sana,
Maungoni mwangu humu, nilikuwa nao jana,
Kwa wingi katika damu, tahamaki leo sina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

2. Kichwa kimejaa mvi,kinywani meno hamna,
Nikenda kama mlevi, miguu nguvu haina,
Kumbe ujana ni hivi, ukenda hauji tena,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

3. Jua langu limekuchwa, na nyota nilizoona,
Ukinitazama kichwa, nywele nyeusi hakina,
Kama zilizofikichwa, zikang'olewa mashina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

4. Natatizika kauli,midomo najitafuna,
Nimekusanya adili, walakini hali sina,
Dunia kitu bahili, hiki una kile huna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana


5. Nilikuwa ni waridi, furaha ya wasichana,
Neno hawakunirudi, wakati wa kukutana,
Sasa nanuka baridi, wanionapo waguna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

6. Walio wakinihusu, walikuwa wengi sana,
Wanawake wenye busu,uzuri na usichana,
Leo sina hata nusu, ya wanitajao jina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

7. Wazuri wenye uturi, na mikono yenye hina,
Kila mtu mashuhuri, alipenda kuniona,
Nilifaa kwa shauri, na sasa kauli sina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana


8. Dunia bibi harusi,kwa watu kila namna,
Inapendeza nafsi, wakati wa kuiona,
Na leo sina nafasi, kwa uzee kunibana,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

9. Kilichokuwa gizani, niliweza kukiona,
Nikakijua thamani, sura yake hata jina,
Leo sijui ni nini, hata ikiwa mchana,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

10. Kilichotaka fikra, niliweza kukinena,
Kwa mfano na kwa sura, mpaka kikafanana,
Leo tazama hasara, nguvu hiyo sina tena,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

11. Kilichotaka mapimo, sikifahamu mapana,
Marefu yake na kimo, siifahamu bayana,
Nusu nimo nusu simo, duniani najiona,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

12. Hadumu nasikitika, rafiki yangu ujana,
Machozi yamiminika, na kutenda hapana,
Ni wakati umefika, uzee dawa hauna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

13. Hauna dawa uzee, mabega yamepetana,
Anionaye ni 'wee", ondoka hapa laana,
Wanaposema na miye, niliyekuwa na jina!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

14. Kaditamati shairi,uchungu wanitafuna,
Walakini nafikiri, twafuata Subuhana,
Katika ile amri, ya "kuwa" na "kutengana"
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

Shaaban Robert, Tanga
 
Maneno mazito. Maneno ya kweli. Ole wetu tusiosikia ya wakubwa hawa!!
 
Ebu vijana wa zamani na wa sasa tujikumbushe kuhusu UJANA. Soma shairi la Shaaban Robert alilotunga miaka ya 50 lakini hekima zake zadumu mpaka ukamilifu wa dahari.

UJANA

1. Ujana kitu kitamu, tena ni azizi sana,
Maungoni mwangu humu, nilikuwa nao jana,
Kwa wingi katika damu, tahamaki leo sina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

2. Kichwa kimejaa mvi,kinywani meno hamna,
Nikenda kama mlevi, miguu nguvu haina,
Kumbe ujana ni hivi, ukenda hauji tena,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

3. Jua langu limekuchwa, na nyota nilizoona,
Ukinitazama kichwa, nywele nyeusi hakina,
Kama zilizofikichwa, zikang'olewa mashina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

4. Natatizika kauli,midomo najitafuna,
Nimekusanya adili, walakini hali sina,
Dunia kitu bahili, hiki una kile huna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana


5. Nilikuwa ni waridi, furaha ya wasichana,
Neno hawakunirudi, wakati wa kukutana,
Sasa nanuka baridi, wanionapo waguna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

6. Walio wakinihusu, walikuwa wengi sana,
Wanawake wenye busu,uzuri na usichana,
Leo sina hata nusu, ya wanitajao jina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

7. Wazuri wenye uturi, na mikono yenye hina,
Kila mtu mashuhuri, alipenda kuniona,
Nilifaa kwa shauri, na sasa kauli sina,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana


8. Dunia bibi harusi,kwa watu kila namna,
Inapendeza nafsi, wakati wa kuiona,
Na leo sina nafasi, kwa uzee kunibana,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

9. Kilichokuwa gizani, niliweza kukiona,
Nikakijua thamani, sura yake hata jina,
Leo sijui ni nini, hata ikiwa mchana,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

10. Kilichotaka fikra, niliweza kukinena,
Kwa mfano na kwa sura, mpaka kikafanana,
Leo tazama hasara, nguvu hiyo sina tena,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

11. Kilichotaka mapimo, sikifahamu mapana,
Marefu yake na kimo, siifahamu bayana,
Nusu nimo nusu simo, duniani najiona,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

12. Hadumu nasikitika, rafiki yangu ujana,
Machozi yamiminika, na kutenda hapana,
Ni wakati umefika, uzee dawa hauna,
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

13. Hauna dawa uzee, mabega yamepetana,
Anionaye ni 'wee", ondoka hapa laana,
Wanaposema na miye, niliyekuwa na jina!
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

14. Kaditamati shairi,uchungu wanitafuna,
Walakini nafikiri, twafuata Subuhana,
Katika ile amri, ya "kuwa" na "kutengana"
Nasikitika hadumu, rafiki yangu ujana

Shaaban Robert, Tanga

Hakika ya hili shairi ndio linalonisukuma kuandika haya niandikayo,huwa nalisoma tena na tena na wala katu sintoweza kuacha kulisoma. Hili shairi lilitungwa miaka mingi sana na sheikh shaaban Robert. Lau mwenyeezi mungu angekuwa amempa uhai hadi leo basi sheikh shaaban Robert angekuwa na umri wa zaidi ya miaka 100. Alizaliwa vibambani Tanga 1909 na kufariki 1962 na kuzikwa machui huko huko Tanga ambako ndio kulikuwa asili haswa ya mama yake mzazi, aliyejulikana kama Mwanamwema (mwana binti mwidau).Yasemekana hakuwahi kutokea mtu bingwa wa Lugha ya kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki kama huyu bwana (mwenyezi mungu mrehemu). Pamoja na kufanya kazi serikalini kwa miaka 33 katika idara mbalimbali kama forodha, wanyama na utawala alikuwa na mapenzi makubwa na lugha ya kiswahili na alijivunia kuitwa mswahili na pia alijulikana kama baba wa kiswahili. Alipata tuzo mbalimbali kwa kazi ya uandishi wake hata nje ya ukanda wa Afrika mashariki, kama ile ya M.B.E ya uingereza. Katika kumuenzi marehemu sheikh Shaaban Robert leo hii ndio tuna Shule na Mtaa wa Shaaban Robert pale Dar es salaam, (sina hakika na maeneo mengine nchini ambayo yame enzia kama kumbukumbu yake). Ukisoma kazi zake utaona amezungumzia mambo kadha wa kadha kama mapenzi, siasa na matukio mengine ya kijamii. Angalia kitabu chake cha Mapenzi Bora, ameandika Tenzi 700 akizungumzia mapenzi..........!
Huyu mtu kuna mengi ya kumzungumzia ila haya ni kwa uchache, kwani kaandika mambo mengi kuhusu maisha yake binafsi, utoto mwake, makuzi yake, kazi zake na hata baada ya kustaafu kwake.
Huyu ndio Sheikh Shaaban Robert (m'mungu umsamehe makosa yake na umrehemu).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom