Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

Ujinga na upumba.vu siyo sehemu ya utakatifu. Kama watu wetu watakufa kwa sababu ya kukosa matibabu bora, kama watu wetu watateseka kwa kukosa ajira, kama watoto wetu watakosa elimu nzuri kwa sababu ya umaskini wakati Mungu alitupatia vyote vilivyopo kwa manufaa yetu, utakuwa ni upumbav.u. Tutapata maisha ya mateso Duniani, na mbingu/ahera hatutaziona. Mungu hujivunia watu werevu siyo watu wapumbavu waliopewa rasilimali mbalimbali lakini wakashindwa kuzibadilisha ili ziwasaidie wao na wazao wao.

Tunahitajika kufanya mabadiliko lakini kwa werevu siyo kwa kutumia nguvu bila akili. Tuna uwezo wa kuirekebisha sekta ya madini ili iwe na manufaa zaidi lakini siyo kwa namna tuliyofanya. Ulimwengu wa kutumia nguvu uliishia karne ya 18. Karne ya sasa ni ya akili na werevu.

Utatukanwa si kwa sababu umewatukana ila kwa sababu siyo mwenzao
 
Mada ndeeeefu ukweli punje.Tuambie Uganda walitaka bomba hilo lipitie wapi? nini kilifanya lipitie Tanzania na siyo lilikotarajiwa?
Wawekezaji walitaka lipitie Kenya ila kwa kuwa yule mfuga ng'ombe ni mtu wetu ndio kimetokea ulichokiona, fadhila
Mnataka ukweli HALISI au ukweli wa kutafutia kick?!!

Kama mtanataka ukweli wa kutafutia kiki, basi mradi wa bomba la mafuta kuja Tanga kulitokana na kukubalika kwa JPM! How does it sound?!

Kama mnataka ukweli HALISI, mradi wa bomba la mafuta JPM kaukuta!!!!

Originally, Museveni alitaka mradi upitie Mombasa!!! Kama mtakumbuka, Uhuru Kenyatta aliwatia upepo akina Kagame na Museven hadi wakaanza kuitenga Tanzania na kuanzisha Ushoroba wa Kaskazini!! Moja ya miradi ambayo walikubaliana ni pamoja na reli na bomba la mafuta kutoka Uganda to Mombasa!!!

JK na serikali yake wakausambaratisha ule umoja wao fake!! Baada ya kusambaratika, Kagame akaenda Dar es salaam March 2015 kujadiliana suala la kushirikiana ujenzi wa Reli na akawa ameachana na suala la reli kwenda Mombasa!!

Total nao, kama wawekezaji wakubwa kwenye mradi wa mafuta Uganda, wakashituka suala la kupitisha bomba hadi Mombasa!!! Sababu kubwa zilikuwa ni umbali, terracing along Uganda-Kenya route, thamani ya ardhi ya Kenya lakini bila kusahau hali ya kiusalama (Al Shabab)!

Ingawaje Museven bado alitamani bomba lipitie Lamu, Total wakasema NO!

October 2015, Total & Uganda's Ministry of Energy wakaenda Dar es salaam na kusaini first agreement ya kuangalia uwezekano wa kupitisha bomba Tanga!!!

JPM alipoingia tu madarakani, nadhani hata kabla mwezi hajamaliza, Total na wenzake wakawa wameshaamua kwamba bomba litapita Tanga!!!
 
hakuna haja ya wawekezaji kutoka nje kwenye madini...hayo madini tunayo uwezo wa kuyachimba wenyewe na kuyauza nje.......kwa mfano madini ya dhahabu ukiwa na sururu na karai unayachimba vizuri tu wawekezaji kutoka nje wa nini hao ni wezi tu wamekuja kutunyonya
Duh! Sururu na karai tu, halafu upate madini ya kuuza nje!?Na wewe unahitaji kuombewa kama Baba J.
 
Leo kwa kupitia mabadiliko ya sheria zetu mbovu za Prof. Kabudi, hakuna kampuni ya nje itakayokuja kufanya utafiti wa madini ya Tanzania. Vipengere vinavyozuia wawekezaji kuja Tanzania kufanya utafiti wa madini ni pamoja na:
hayo ndio wanafanya Ghana na Botswana.Haiwezekani kiwango kitakachogunduliwa kisiwekwe kwenye maandishi.
Nia ya kupeleka data GST ni kuweka kumbukumbu tu.Wawekezaji wana tabia ya kutangaza ugunduzi pungufu ili wachimbe kwa wingi.
Tunataka ukigundua tani 100 za dhahabu,kwenye vitabu vyetu vikionesha umeshazalisha tani 100,tuanze kupatana upya.
Ni muwekezaji wa kubabaisha tu ndio anaweza kukimbia Tanzania
 
Ujinga na upumba.vu siyo sehemu ya utakatifu. Kama watu wetu watakufa kwa sababu ya kukosa matibabu bora, kama watu wetu watateseka kwa kukosa ajira, kama watoto wetu watakosa elimu nzuri kwa sababu ya umaskini wakati Mungu alitupatia vyote vilivyopo kwa manufaa yetu, utakuwa ni upumbav.u. Tutapata maisha ya mateso Duniani, na mbingu/ahera hatutaziona. Mungu hujivunia watu werevu siyo watu wapumbavu waliopewa rasilimali mbalimbali lakini wakashindwa kuzibadilisha ili ziwasaidie wao na wazao wao.

Tunahitajika kufanya mabadiliko lakini kwa werevu siyo kwa kutumia nguvu bila akili. Tuna uwezo wa kuirekebisha sekta ya madini ili iwe na manufaa zaidi lakini siyo kwa namna tuliyofanya. Ulimwengu wa kutumia nguvu uliishia karne ya 18. Karne ya sasa ni ya akili na werevu.
Sina hakika kama unajua unachoandika. Issue hapa, Ni kwamba tunahitaji sheria za kulinda rasilmali zetu ili tunufaike. Kama tunaibiwa madini yetu na kuachiwa mashimo tu ni heri waondoke kwa sheria zetu hizi. Wewe unataka wachimbe tu madini yetu na kuondoka. Amka, mtu wa mungu.
 
Wakati wa bomba la gesi kulikuwa na mbwembwe nyingi jinsi litakavyomwaga mamilioni ya ajira kwa (hasa) vijana wa Kitanzania. Sisikii tena mtu akiliongelea hilo baadla yake wanaongelea ajira za bomba la mafuta.
Ujinga ni kitu kibaya na ndio maana Vitabu vitakatifu vikatuasa kuwa kumuomba Mungu hekima (akili) ni jambo jema zaidi. Tuna mfano wa bomba la TAZAMA na tungeangalia linatoa ajiri kwa watu wangapi (ambao kimsingi ni 'walewale') kabla ya kuliangalia hili ambapo na wenye nalo (Uganda) vijana wao wanafukuzia ajira hizo hizo!
Miradi mingi ya nchi za Afrika iko kisiasa zaidi.
 
Kama unadhani wanafukuzwa hapa na kuna nchi wanapewa ahueni, waende tu huko, kwani ni lazima kulalama kwa sehemu unayonyanyasika ilhali wewe ni mgeni eneo hilo? Kama wenyeji watakufa njaa kwa kuondoka kwako, waache wafe, wakiona pengine chanzo cha njaa yao ni kuondoka kwako, watakuja kukubembeleza tu, una wasiwasi gani?

Na aina hii ya wanakijiji hiki kujiona wasomi na waelewa sana wa haya maujanja ya watu weupe huwa unanihuzunisha sana. Kama mali ni yetu, wewe mwanakijiji nini inakusumbua hata uungane nao. Si ajabu hukuwa sehemu yoyote ya maamuzi au kupata CLASSIFIED INFO halafu unazungumzia kile walichotaka wao ukijue na kuja kutuambia sisi hatujui!!!

PARAPANDA IMELIA.......
 
hayo ndio wanafanya Ghana na Botswana.Haiwezekani kiwango kitakachogunduliwa kisiwekwe kwenye maandishi.
Nia ya kupeleka data GST ni kuweka kumbukumbu tu.Wawekezaji wana tabia ya kutangaza ugunduzi pungufu ili wachimbe kwa wingi.
Tunataka ukigundua tani 100 za dhahabu,kwenye vitabu vyetu vikionesha umeshazalisha tani 100,tuanze kupatana upya.
Ni muwekezaji wa kubabaisha tu ndio anaweza kukimbia Tanzania
Hakuna mwekezaji mwendawazimu ambaye amegundua ounces za dhahabu 2 million halafu aseme nimegundua 0.5 million ounces. Hayupo mjinga wa namna hiyo. Kwanza faida kubwa kwenye makampuni ya madini haitegemei mauzo ya madini bali mauzo ya hisa. Hisa zako ili ziwe na soko kwenye share market ni lazima uoneshe taarifa zilizo nzuri za kuvutia wawekezaji na hasa taarifa za ugunduzi na uzalishaji.

Ni mwekezaji mbabaishaji ndiye anayeweza kuficha taarifa za ugunduzi lakini siyo wawekezaji makini ambao wanafanya trading kwenye share markets.

Nitajie kampuni hata moja duniani iliyowahi kudanganya ore resource kwa kutaja kiwango pungufu. Nina uhakika haipo. Lakini yapo makampuni yaliyoripoti resource kubwa zaidi kuliko uhalisia ili kuvutia wawekezaji.

Kwanza hata kama kampuni ikiripoti resource kiasi fulani haimaanishi yote itakuwa mineable. Au ile ambayo nasema leo inaweza kuchimbika, siyo lazima ichimbike miaka mitatu ijayo.

Ni uwongo kuwa Botswana na Ghana wanafanya hivyo. Nimefanya kazi Ghana, Mali na Liberia. Ghana na Botswana kama yalivyo mataifa mengine mengi, kampuni zinapofunga au wanapoachia leseni ndipo database na core samples hukabidhiwa serikalini. Nchi ya Ghana, Liberia, Botswana na Mali ni kati ya nchi zenye sheria, sera na mazingira rafiki sana kwa mining sector.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kweli MTU au kampuni imedhamiria kufanya utafiti inashindwaje kupata vibali GST?

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida siyo kupata kibali lakini fikiria muda na gharama.

Wewe unafanya drilling Mpanda, samples unapeleka Australia, drill rig ipo site kwa contract, waiting charge $400 kwa saa, unataka samples zipelekwe maabara haraka, upate majibu haraka ili zikusaidie kuendelea kurekebisha program plan bila ya kusababisha standby charges. Halafu usimamishe rig, uanze kulipa $400 per hour, uende Dodoma kupata kibali cha kupeleka samples nje ya nchi. Wakati huo huo kuna afisa wa serikali wa idara ya madini mnaye kwenye project. Ni urasimu usiokuwa na msingi wala hauongezi chochote upande wa Taifa, zaidi ya kuongeza gharama za utafiti na kuifanya nchi yetu mahali pabaya kwa uwekezaji katika sekta hii.
 
Sina mahaba na ngosha, lakini ktk hili la bomba la mafuta amejitahidi sana. Tusiongelee kama kitu kisicho na faida. Leteni data hapa ya kiasi cha pesa ambacho nchi itapata kwa pipa moja litakalopita ktk bomba kabla ya kuanza kulaumu. Ubaya wa sheria zetu za madini haifanyi na mradi wa bomba la mafuta kuwa mbaya.

Ninachokiona ni kukosekana kwa taarifa sahihi kutokana na uchanga wetu ktk sekta ya madini. Ndipo hapo wenye uelewa nusu na vibaraka wanataka watupe shule ambayo wao wenyewe hawana.
 
Katika jambo linaloshangaza ni jinsi Tanzania inavyoonesha kushabikia na kufurahia mradi wa bomba la mafuta ya Uganda. Bomba hili la mafuta ni matokeo ya sera za nchi ya Uganda kuvutia wawekezaji katika utafiti na ujenzi wa miradi ya uvunaji mali za asili za Uganda. Ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu. Uganda imefanya hivyo kwa kupitia sera, sheria na ushirikiano wa moja kwa moja na makampuni ya nje yanayowekeza Uganda.

Tunafurahia mradi wa mafuta ya Uganda wakati kwetu tunafanya kila jitihada za kufukuza wawekezaji kwa maelezo kuwa tunaibiwa. Tunafanya hivyo kwa kupitia sheria zetu mbovu zinazosimamia utafiti wa mali za asili, uvunaji na kauli za viongozi wakuu. Leo karibu makampuni 160 yaliyokuwa yanafanya utafiti Tanzania yamesimama, lakini yanaendelea kufanya utafiti katika mataifa mengine.

Leo kwa kupitia mabadiliko ya sheria zetu mbovu za Prof. Kabudi, hakuna kampuni ya nje itakayokuja kufanya utafiti wa madini ya Tanzania. Vipengere vinavyozuia wawekezaji kuja Tanzania kufanya utafiti wa madini ni pamoja na:

1) Sampuli za madini huwezi kupeleka nje mpaka upate kibali toka GST. Wenzetu wanapunguza urasimu, sisi tunaongeza urasimu. Sheria hiyo imewekwa na watu wasiojua chochote kuhusu utafiti wakifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia sampuli. Huo ni ujinga wa hali ya juu. Unajiuliza ni dhahabu gani inaweza kuwepo ndani ya sampuli ya 1kg mpaka kuwepo wizi wa madini kupitia sampuli! Hivi unapokuwa na grade ya 15g/t, ndani ya kilo moja ya sampuli? Dhahabu itakayowepo ni 15÷1000=0.015g. Gramu 1 ya dhahabu ni kama TZS 50,000. Kwa hiyo 0.015g itakuwa na thamani ya 0.015×50,000=TZS750. Hivi kuna mwekezaji anayeweza kuja kuiba Tanzania TZS 750 kwa kila sampuli? Sheria kama hii inaifanya Tanzania kuonekana nchi ya wajinga watupu.

2) Majibu ya maabara ya sampuli (database) za mwekezaji yapelekwe GST. Unajiuliza kama walioandika sheria hiyo wana uelewa japo mdogo wa biashara ya madini. Utafiti haumwingizii pesa mtafiti hata shilingi moja. Thamani ya mradi anaoutafiti ipo katika data. Ni data hizi, kama zikiwa nzuri ndiyo anaweza kuuza ili kurudisha sehemu ya pesa aliyotumia au ikarudisha gharama na kumpa faida, au asirudishe hata shilingi 1. Serikali inalazimisha ipate data mapema bure!!. Data ni taarifa ya siri ya kampuni kwa sababu usipokuwa makini ya namna ya kuzitoa zinaweza kuua kampuni kwenye share markets. Lazima hiyo kampuni iwe ya wajinga watupu ili kuweza kwenda kufanya utafiti katika nchi yenye sheria kama hii. Kama watakuwepo, basi ni lazima watapeleka data ambazo siyo halisi

3) Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, ndiyo unapata uhakika ule ukweli kuwa academicians are poor managers and poor entrepreneurs. Wanashindwa kutafsiri nadharia walizo nazo kwenye uhalisia. Mabadiliko yale yanamtaka mwekezaji kutoa 16% free carried shares (nchi nyingi zinapata 0 - 10% free carried shares), mrabaha 7% (inajumuisha inspection ya 1%; Dunia nzima ni Mugabe pekee yake anatoza 7% royalty lakini wao wana corporate tax ndogo kuliko Tanzania. Mataifa mengi mrabaha ni 0 - 5%). Bahati mbaya sana Rais wetu amejenga imani kubwa sana kwa academicians, kuna siku atakuja kugundua kuwa they were WRONG PEOPLE FOR THE RIGHT JOB. By then it will be too late.

Kwa mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, tutaendelea kuwa na kampuni ambazo tayari zina migodi Tanzania, lakini hatutapata miradi mipya wala wawekezaji wapya. Leo Tanzania inatajwa kama eneo hatari kwa mitaji ya nje. Baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, makampuni yote yaliyowekeza katika eneo hatari la Tanzania, hisa zao katika soko la fedha Sydney yalipoteza 30 - 50%.

Kupanga ni kuchagua, lakini kwa nini tufurahie matunda ya sera nzuri za uwekezaji za Uganda wakati sisi kwetu hatutaki kuwa na sera rafiki za uwekezaji? Leo makampuni ya utafiti wa madini yanaondoka Tanzania yanaenda Kenya, Angola, Mali, Uganda, Amerika Kusini na Asia, halafu baada ya miaka 5 tutaanza kushangilia miradi iliyopo Kenya na Uganda.

Wawekezaji wasipopata madini toka Tanzania, watapata mahali pengine Duniani. Katika dhahabu sisi hatupo katika top 15, lakini kuna mataifa zaidi ya 100 yenye dhahabu. Kwa nickel na iron hatupo hata katika top 20. Katika copper, silver, PGEs hatupo hata katika top 50. Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini hii ni saphire yenye vanadium, saphire ya kawaida ipo mataifa mengi Duniani. Zaidi ya yote ni kuwa tanzanite ni kwaajili ya urembo. Kwa nini tuna fikra kuwa ni sisi pekee yetu?

Dunia inaweza kuendelea bila ya Tanzania lakini Tanzania haiwezi bila ya Dunia. Tufanye jitihada mbalimbali lakini tusisahau tumo ndani ya Dunia yenye kila kitu.
Wewe utakuwa umetumwa si bure!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada na swali... tulikuwa tunaibiwa au ni uzushi wa siasa tu?
 
Mkuu with due respect maandiko yako ni propaganda tupu. Hutoi mifano halisi ila unataja nchi kwa ujumla wake tu. Mfano Botswana wanafanyeje? Ghana wanafanyeje nk. Tumeibiwa vya kutosha sana na imetosha sasa.

Mfano Botswana ukija na upembuzi wa mradi wako wa tuseme umepanga kuvuna ounces million 2.5 za dhahabu, ukiwekeza na ukavuna kweli kiasi hicho lakini kulingana na halisi ukawa bado kuna reserve ya kutosha, wanaingia ubia na wewe wa 50 kwa 50. Nakumbuka wakati ukiwa unavuna wakia millioni 2.5 ulikuwa ukilipa royalty na kodi zake kama kawa.

Pia fikiria sisi tunaumiliki wa karibu asilimia 30 mgodi wa almasi mwadui lakini tangu kabla ya uhuru mpaka leo hakuna gawio ni hasara juu ya hasara. Ni upuuzi mtupu kutuambia watakimbia. Wacha wakimbie tutavuna sisi na technology yetu.

Tanzanite inapatikana Tanzania wauzaji wakubwa wahidi, marekani na Kenya. Sisi sijui ni wanne, upuuzi gani huu!

Tunataka haki sawa na mimi.niko mgodini tangu 2005 najua uhuni wote. Sydney wanaandika taarifa nyingi za uongo na uzushi na wanafanya biashara za kufa mtu kwenye masoko yao ya hisa kwa mali zikiwa Tanzania. Transfer price arrangement ndo usiombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mwekezaji mbabaishaji ndiye anayeweza kuficha taarifa za ugunduzi lakini siyo wawekezaji makini ambao wanafanya trading kwenye share markets.
Hivi unajua kama ACACIA waliwasilisha hesabu za kupika TRA kuonesha kuwa wamepata hasara ili wasilipe kodi,wakajisahau wakapeleka taarifa sahihi LSE,ili bei ya hisa ipande?
TRA wakazisoma taarifa zao za kweli kwenye website ya LSE wakapeleka bili ya dola milioni 20 jamaa wakalipa.Unalijua hilo au unaongelea vitu ambavyo vinafurahisha mtima wako?
 
Nyie acheni kufanan
Teh teh teh!

Kuna TAZAMA. Nadhani hili linatoka Dar kwenda Zambia. Kuna tofauti na hili la kutoka Tanga kwenda Uganda?

Naomba nami nishangiliwe kwani nimefungua restaurant mpya huko Nakapanya. Natarajia kutoa ajira kwa watu kama 20 hivi.
isha bomba la mafuta la TAZAMA na la Uganda. La TAZAMA linaenda Ndola kwenye kiwanda cha kusafisha mafuta kwa ajili ya soko la Zambia na hata DRC. Lakini hili la Uganda ni kubwa kwa ajili ya kusarisha kwa ajili ya kuuzwa, so mafuta ya Uganda ni kwa ajili ya kuuzwa nchi mbalimbali.
 
Back
Top Bottom