Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

UWEKEZAJI NI NINI?

UWEKEZAJI ni njia ya kufanya fedha zako kuzaa fedha zaidi. Ili uweze kuwa MWEKEZAJI unapaswa kuwa na shughuli inayokuingizia KIPATO KWANZA halafu ndipo unaweza KUWEKEZA sehemu ya kipato chako ambacho kinaweza kutokana na mshahara, kufanya biashara na kadhalika.

Ili uweze kuwekeza unapaswa kuweka akiba ya mapato yako. Tunaweza kujifunza kutoka kwa WABABILON ambapo walitumia HEKIMA YA KUWEKA AKIBA angalau asilimia 10 ya mapato yao ya kila mwezi kwa lengo la KUWEKEZA ifikapo mwanzoni mwa mwaka mpya. NIDHAMU hiyo ilifanya wengi wao kuwa MATAJIRI na BABILON kuwa JIJ TAJIRI zaidi duniani kwa wakati ule na hasa sasa imebakia kuwa SHERIA muhimu ya FEDHA inayomfanya mtu yeyote anayeifuata kuweza KUTAJIRIKA.

Capital letters hazina maana yoyote. Take a good example from Said Salim Bakhresa. Hayo mengine ni mashudu tu ya kuwapelekea ng'ombe na nguruwe.
 
M


Mada ndeeeefu ukweli punje.Tuambie Uganda walitaka bomba hilo lipitie wapi? nini kilifanya lipitie Tanzania na siyo lilikotarajiwa?
Wawekezaji walitaka lipitie Kenya ila kwa kuwa yule mfuga ng'ombe ni mtu wetu ndio kimetokea ulichokiona, fadhila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ingekuwa hatuvutii wawekezaji hilo bomba lingepita kenya, kumbuka juhudi kubwa zilizofanywa na serikali ili lipite tz, hilo bomba halijajileta,
 
Kikwete alikataa kuwashobokea hawa madicteta M7 na Kagame naona huyu ameingia mkenge.....

Nakumbuka kuna kipindi M7 alitaka kuleta lami hadi sehemu shule yake ilipo ambayo ipo kwenye Ardhi ya Tanzania huko mkoani Kagera Kati ya wilaya Karagwe au kyerwa lakin KIKWETE alikataa na alimwambia hyo shule uliyojenga katika Ardhi ya Tanzania ni shukrani/upendeleo tosha....

Pia kuna KIPINDI KAGAME alizozana na KIKWETE kwenye issue ya uwekezaji maaana alitaka kuilinda sehemu ya anga ya Tanzania lakini KIKWETE alikataaaa na aliona mbali....

Sasa huyu siku yakimtokea puani ndo atajua........
 
Kwa hiyo unaamini kuwa waganda ni wapumbavu kiasi cha kuwekeza kwenye fadhila,na Kenya ni dhaifu kiasi cha kushindwa kuomba fadhila?
Wawekezaji walitaka lipitie Kenya ila kwa kuwa yule mfuga ng'ombe ni mtu wetu ndio kimetokea ulichokiona, fadhila

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We're too optimistic with oil pipeline kuliko Waganda wenyewe walivyo optimistic with mafuta yenyewe!!!

Mbaya zaidi, ni kama tumesahau kwamba sisi wenyewe kule Lindi kuna mradi wa zaidi ya $30 Billion kwa ajili ya gas processing plant... zaidi ya mara kumi ya ule wa Uganda!!!

Hata hivyo, kinachoendelea hivi sasa only God knows!!!

He who knows not and knows that he knows not teach him,he is teachable. Mwalim wangu mmoja wa lugha alifundisha nani unaweza kumfundisha.
 
hizo data ulizoweka ni ngumu sana kwa mtu aliyesoma theory primary mpaka kuwa profesa kuzielewa...
 
M


Mada ndeeeefu ukweli punje.Tuambie Uganda walitaka bomba hilo lipitie wapi? nini kilifanya lipitie Tanzania na siyo lilikotarajiwa?
Mwehu we we!!! Yaani katika yote kwenye hilo bango, content uliyoiona ndo hiyo tu ya bomba? Nadhani una ubongo wenye kamasi
Tanzania hii watu wenye akili zako no zaidi ya asilimia 60! Ndo maana bado tunaumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwehu we we!!! Yaani katika yote kwenye hilo bango, content uliyoiona ndo hiyo tu ya bomba? Nadhani una ubongo wenye kamasi
Tanzania hii watu wenye akili zako no zaidi ya asilimia 60! Ndo maana bado tunaumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naam kwa kipimo chako na aina ya ufahamu wako una akili kubwa ya matusi.Hongera.
 
hakuna haja ya wawekezaji kutoka nje kwenye madini...hayo madini tunayo uwezo wa kuyachimba wenyewe na kuyauza nje.......kwa mfano madini ya dhahabu ukiwa na sururu na karai unayachimba vizuri tu wawekezaji kutoka nje wa nini hao ni wezi tu wamekuja kutunyonya
 
Mtoa mada umeongea point Sana ,tatizo Vijana wa Lumumba watasema sio Mzalendo

Sent From Kisana Kiki Iphone
 
Mkuu Bams umekuja na aandiko linalofikirisha sana. Ukiwasikikiza viongozi wetu ni kama wamelogwa na mchawi mmoja. Wanaamini tuna raslimali adimu ambazo haziko pengine popote duniani. Ukiwasikia wanaongelea dhahabu unaweza ukadhani ni Tanzania tu ipo. Njoo kwenye wanyama pori, tuliaminishwa tuna mbuga zenye wanyama ambai hawapo pengine dunia hii. Kumbe wala usiende mbali, nenda hapo Mozambique, Zambia na Drc ndio usiseme. Kuna wanyama makundi kwa makundi.

Anyway inabidi tujilaumu wenyewe kwa kuongozwa na watu wenye elimu ya darasani lakini wenye uwezo duni kiubunifu.

Nisaw ana tulivyo karirishw aetiu wazungu walifuata ardhi yenye rutba africa, kitu ambcho si kweli, huko ulaya rutba ni ya kutosha na technology pia.
 
Katika jambo linaloshangaza ni jinsi Tanzania inavyoonesha kushabikia na kufurahia mradi wa bomba la mafuta ya Uganda. Bomba hili la mafuta ni matokeo ya sera za nchi ya Uganda kuvutia wawekezaji katika utafiti na ujenzi wa miradi ya uvunaji mali za asili za Uganda. Ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu. Uganda imefanya hivyo kwa kupitia sera, sheria na ushirikiano wa moja kwa moja na makampuni ya nje yanayowekeza Uganda.

Tunafurahia mradi wa mafuta ya Uganda wakati kwetu tunafanya kila jitihada za kufukuza wawekezaji kwa maelezo kuwa tunaibiwa. Tunafanya hivyo kwa kupitia sheria zetu mbovu zinazosimamia utafiti wa mali za asili, uvunaji na kauli za viongozi wakuu. Leo karibu makampuni 160 yaliyokuwa yanafanya utafiti Tanzania yamesimama, lakini yanaendelea kufanya utafiti katika mataifa mengine.

Leo kwa kupitia mabadiliko ya sheria zetu mbovu za Prof. Kabudi, hakuna kampuni ya nje itakayokuja kufanya utafiti wa madini ya Tanzania. Vipengere vinavyozuia wawekezaji kuja Tanzania kufanya utafiti wa madini ni pamoja na:

1) Sampuli za madini huwezi kupeleka nje mpaka upate kibali toka GST. Wenzetu wanapunguza urasimu, sisi tunaongeza urasimu. Sheria hiyo imewekwa na watu wasiojua chochote kuhusu utafiti wakifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia sampuli. Huo ni ujinga wa hali ya juu. Unajiuliza ni dhahabu gani inaweza kuwepo ndani ya sampuli ya 1kg mpaka kuwepo wizi wa madini kupitia sampuli! Hivi unapokuwa na grade ya 15g/t, ndani ya kilo moja ya sampuli? Dhahabu itakayowepo ni 15÷1000=0.015g. Gramu 1 ya dhahabu ni kama TZS 50,000. Kwa hiyo 0.015g itakuwa na thamani ya 0.015×50,000=TZS750. Hivi kuna mwekezaji anayeweza kuja kuiba Tanzania TZS 750 kwa kila sampuli? Sheria kama hii inaifanya Tanzania kuonekana nchi ya wajinga watupu.

2) Majibu ya maabara ya sampuli (database) za mwekezaji yapelekwe GST. Unajiuliza kama walioandika sheria hiyo wana uelewa japo mdogo wa biashara ya madini. Utafiti haumwingizii pesa mtafiti hata shilingi moja. Thamani ya mradi anaoutafiti ipo katika data. Ni data hizi, kama zikiwa nzuri ndiyo anaweza kuuza ili kurudisha sehemu ya pesa aliyotumia au ikarudisha gharama na kumpa faida, au asirudishe hata shilingi 1. Serikali inalazimisha ipate data mapema bure!!. Data ni taarifa ya siri ya kampuni kwa sababu usipokuwa makini ya namna ya kuzitoa zinaweza kuua kampuni kwenye share markets. Lazima hiyo kampuni iwe ya wajinga watupu ili kuweza kwenda kufanya utafiti katika nchi yenye sheria kama hii. Kama watakuwepo, basi ni lazima watapeleka data ambazo siyo halisi

3) Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, ndiyo unapata uhakika ule ukweli kuwa academicians are poor managers and poor entrepreneurs. Wanashindwa kutafsiri nadharia walizo nazo kwenye uhalisia. Mabadiliko yale yanamtaka mwekezaji kutoa 16% free carried shares (nchi nyingi zinapata 0 - 10% free carried shares), mrabaha 7% (inajumuisha inspection ya 1%; Dunia nzima ni Mugabe pekee yake anatoza 7% royalty lakini wao wana corporate tax ndogo kuliko Tanzania. Mataifa mengi mrabaha ni 0 - 5%). Bahati mbaya sana Rais wetu amejenga imani kubwa sana kwa academicians, kuna siku atakuja kugundua kuwa they were WRONG PEOPLE FOR THE RIGHT JOB. By then it will be too late.

Kwa mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, tutaendelea kuwa na kampuni ambazo tayari zina migodi Tanzania, lakini hatutapata miradi mipya wala wawekezaji wapya. Leo Tanzania inatajwa kama eneo hatari kwa mitaji ya nje. Baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, makampuni yote yaliyowekeza katika eneo hatari la Tanzania, hisa zao katika soko la fedha Sydney yalipoteza 30 - 50%.

Kupanga ni kuchagua, lakini kwa nini tufurahie matunda ya sera nzuri za uwekezaji za Uganda wakati sisi kwetu hatutaki kuwa na sera rafiki za uwekezaji? Leo makampuni ya utafiti wa madini yanaondoka Tanzania yanaenda Kenya, Angola, Mali, Uganda, Amerika Kusini na Asia, halafu baada ya miaka 5 tutaanza kushangilia miradi iliyopo Kenya na Uganda.

Wawekezaji wasipopata madini toka Tanzania, watapata mahali pengine Duniani. Katika dhahabu sisi hatupo katika top 15, lakini kuna mataifa zaidi ya 100 yenye dhahabu. Kwa nickel na iron hatupo hata katika top 20. Katika copper, silver, PGEs hatupo hata katika top 50. Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini hii ni saphire yenye vanadium, saphire ya kawaida ipo mataifa mengi Duniani. Zaidi ya yote ni kuwa tanzanite ni kwaajili ya urembo. Kwa nini tuna fikra kuwa ni sisi pekee yetu?

Dunia inaweza kuendelea bila ya Tanzania lakini Tanzania haiwezi bila ya Dunia. Tufanye jitihada mbalimbali lakini tusisahau tumo ndani ya Dunia yenye kila kitu.
Umesahau, tunataka win-win na wawekezaji otherwise waondoke tutachimba wenyewe baadaye tukipata uwezo. Mbona Nyerere aliyasubirisha? Wewe una dharura gani ambayo Nyerere hakuwa nayo? Unasikitisha, mtu wa mungu.
 
Umesahau, tunataka win-win na wawekezaji otherwise waondoke tutachimba wenyewe baadaye tukipata uwezo. Mbona Nyerere aliyasubirisha? Wewe una dharura gani ambayo Nyerere hakuwa nayo? Unasikitisha, mtu wa mungu.
Ujinga na upumba.vu siyo sehemu ya utakatifu. Kama watu wetu watakufa kwa sababu ya kukosa matibabu bora, kama watu wetu watateseka kwa kukosa ajira, kama watoto wetu watakosa elimu nzuri kwa sababu ya umaskini wakati Mungu alitupatia vyote vilivyopo kwa manufaa yetu, utakuwa ni upumbav.u. Tutapata maisha ya mateso Duniani, na mbingu/ahera hatutaziona. Mungu hujivunia watu werevu siyo watu wapumbavu waliopewa rasilimali mbalimbali lakini wakashindwa kuzibadilisha ili ziwasaidie wao na wazao wao.

Tunahitajika kufanya mabadiliko lakini kwa werevu siyo kwa kutumia nguvu bila akili. Tuna uwezo wa kuirekebisha sekta ya madini ili iwe na manufaa zaidi lakini siyo kwa namna tuliyofanya. Ulimwengu wa kutumia nguvu uliishia karne ya 18. Karne ya sasa ni ya akili na werevu.
 
Nchi ya wagigikoko ni shida.Tulitakiwa kukaa chini kuangalia wapi tuliangukia,kwanini tulianguka tufanyeje tusianguke lakini tukaweka maganda ya ndizi kila mahali ili kila tukipiga kona ni.mueleka.Na mlaumu JK kumleta jamaa ambaye hata PhD yake INA walakini
 
Back
Top Bottom