Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

Hekima ya Tanzania, bomba la mafuta

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,934
Katika jambo linaloshangaza ni jinsi Tanzania inavyoonesha kushabikia na kufurahia mradi wa bomba la mafuta ya Uganda. Bomba hili la mafuta ni matokeo ya sera za nchi ya Uganda kuvutia wawekezaji katika utafiti na ujenzi wa miradi ya uvunaji mali za asili za Uganda. Ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu. Uganda imefanya hivyo kwa kupitia sera, sheria na ushirikiano wa moja kwa moja na makampuni ya nje yanayowekeza Uganda.

Tunafurahia mradi wa mafuta ya Uganda wakati kwetu tunafanya kila jitihada za kufukuza wawekezaji kwa maelezo kuwa tunaibiwa. Tunafanya hivyo kwa kupitia sheria zetu mbovu zinazosimamia utafiti wa mali za asili, uvunaji na kauli za viongozi wakuu. Leo karibu makampuni 160 yaliyokuwa yanafanya utafiti Tanzania yamesimama, lakini yanaendelea kufanya utafiti katika mataifa mengine.

Leo kwa kupitia mabadiliko ya sheria zetu mbovu za Prof. Kabudi, hakuna kampuni ya nje itakayokuja kufanya utafiti wa madini ya Tanzania. Vipengere vinavyozuia wawekezaji kuja Tanzania kufanya utafiti wa madini ni pamoja na:

1) Sampuli za madini huwezi kupeleka nje mpaka upate kibali toka GST. Wenzetu wanapunguza urasimu, sisi tunaongeza urasimu. Sheria hiyo imewekwa na watu wasiojua chochote kuhusu utafiti wakifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia sampuli. Huo ni ujinga wa hali ya juu. Unajiuliza ni dhahabu gani inaweza kuwepo ndani ya sampuli ya 1kg mpaka kuwepo wizi wa madini kupitia sampuli! Hivi unapokuwa na grade ya 15g/t, ndani ya kilo moja ya sampuli? Dhahabu itakayowepo ni 15÷1000=0.015g. Gramu 1 ya dhahabu ni kama TZS 50,000. Kwa hiyo 0.015g itakuwa na thamani ya 0.015×50,000=TZS750. Hivi kuna mwekezaji anayeweza kuja kuiba Tanzania TZS 750 kwa kila sampuli? Sheria kama hii inaifanya Tanzania kuonekana nchi ya wajinga watupu.

2) Majibu ya maabara ya sampuli (database) za mwekezaji yapelekwe GST. Unajiuliza kama walioandika sheria hiyo wana uelewa japo mdogo wa biashara ya madini. Utafiti haumwingizii pesa mtafiti hata shilingi moja. Thamani ya mradi anaoutafiti ipo katika data. Ni data hizi, kama zikiwa nzuri ndiyo anaweza kuuza ili kurudisha sehemu ya pesa aliyotumia au ikarudisha gharama na kumpa faida, au asirudishe hata shilingi 1. Serikali inalazimisha ipate data mapema bure!!. Data ni taarifa ya siri ya kampuni kwa sababu usipokuwa makini ya namna ya kuzitoa zinaweza kuua kampuni kwenye share markets. Lazima hiyo kampuni iwe ya wajinga watupu ili kuweza kwenda kufanya utafiti katika nchi yenye sheria kama hii. Kama watakuwepo, basi ni lazima watapeleka data ambazo siyo halisi

3) Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, ndiyo unapata uhakika ule ukweli kuwa academicians are poor managers and poor entrepreneurs. Wanashindwa kutafsiri nadharia walizo nazo kwenye uhalisia. Mabadiliko yale yanamtaka mwekezaji kutoa 16% free carried shares (nchi nyingi zinapata 0 - 10% free carried shares), mrabaha 7% (inajumuisha inspection ya 1%; Dunia nzima ni Mugabe pekee yake anatoza 7% royalty lakini wao wana corporate tax ndogo kuliko Tanzania. Mataifa mengi mrabaha ni 0 - 5%). Bahati mbaya sana Rais wetu amejenga imani kubwa sana kwa academicians, kuna siku atakuja kugundua kuwa they were WRONG PEOPLE FOR THE RIGHT JOB. By then it will be too late.

Kwa mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, tutaendelea kuwa na kampuni ambazo tayari zina migodi Tanzania, lakini hatutapata miradi mipya wala wawekezaji wapya. Leo Tanzania inatajwa kama eneo hatari kwa mitaji ya nje. Baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, makampuni yote yaliyowekeza katika eneo hatari la Tanzania, hisa zao katika soko la fedha Sydney yalipoteza 30 - 50%.

Kupanga ni kuchagua, lakini kwa nini tufurahie matunda ya sera nzuri za uwekezaji za Uganda wakati sisi kwetu hatutaki kuwa na sera rafiki za uwekezaji? Leo makampuni ya utafiti wa madini yanaondoka Tanzania yanaenda Kenya, Angola, Mali, Uganda, Amerika Kusini na Asia, halafu baada ya miaka 5 tutaanza kushangilia miradi iliyopo Kenya na Uganda.

Wawekezaji wasipopata madini toka Tanzania, watapata mahali pengine Duniani. Katika dhahabu sisi hatupo katika top 15, lakini kuna mataifa zaidi ya 100 yenye dhahabu. Kwa nickel na iron hatupo hata katika top 20. Katika copper, silver, PGEs hatupo hata katika top 50. Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini hii ni saphire yenye vanadium, saphire ya kawaida ipo mataifa mengi Duniani. Zaidi ya yote ni kuwa tanzanite ni kwaajili ya urembo. Kwa nini tuna fikra kuwa ni sisi pekee yetu?

Dunia inaweza kuendelea bila ya Tanzania lakini Tanzania haiwezi bila ya Dunia. Tufanye jitihada mbalimbali lakini tusisahau tumo ndani ya Dunia yenye kila kitu.
 
3) Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, ndiyo unapata uhakika ule ukweli kuwa academicians are poor managers and poor intrepreneurs. Wanashindwa kutafsiri nadharia walizo nazo kwenye uhalisia. Mabadiliko yale yanamtaka mwekezaji kutoa 16% free carried shares (nchi nyingi zinapata 0 - 10% free carried shares), mrabaha 7% (inajumuisha inspection ya 1%; Dunia nzima ni Mugabe pekee yake anatoza 7% royalty lakini wao wana corporate tax ndogo kuliko Tanzania. Mataifa mengi mrabaha ni 0 - 5%). Bahati mbaya sana Rais wetu amejenga imani kubwa sana kwa academicians, kuna siku atakuja kugundua kuwa they were WRONG PEIPLE FOR THE RIGHT JOB. By then it will be too late.

Kwa mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, tutaendelea kuwa na kampuni ambazo tayari zina migodi Tanzania, lakini hatutapata miradi mipya wala wawekezaji wapya. Leo Tanzania inatajwa kama eneo hatari kwa mitaji ya nje. Baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, makampuni yote yaliyowekeza katika eneo hatari la Tanzania, hisa zao katika soko la fedha Sydney yalipoteza 30 - 50%.

Kupanga ni kuchagua, lakini kwa nini tufurahie matunda ya sera nzuri za uwekezaji za Uganda wakati sisi kwetu hatutaki kuwa na sera rafiki za uwekezaji? Leo makampuni ya utafiti wa madini yanaondoka Tanzania yanaenda Kenya, Angola, Mali, Uganda, Amerika Kusini na Asia, halafu baada ya miaka 5 tutaanza kushangilia miradi iliyopo Kenya na Uganda.

Wawekezaji wasipopata madini toka Tanzania, watapata mahali pengine Duniani. Katika dhahabu sisi hatupo katika top 15, lakini kuna mataifa zaidi ya 100 yenye dhahabu. Kwa nickel na iron hatupo hata katika top 20. Katika copper, silver, PGEs hatupo hata katika top 50. Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini hii ni saphire yenye vanadium, saphire ya kawaida ipo mataifa mengi Duniani. Zaidi ya yote ni kuwa tanzanite ni kwaajili ya urembo. Kwa nini tuna fikra kuwa ni sisi pekee yetu?

Dunia inaweza kuendelea bila ya Tanzania lakini Tanzania haiwezi bila ya Dunia. Tufanye jitihada mbalimbali lakini tusisahau tumo ndani ya Dunia yenye kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahahaaahahahahaaaaaaa
 
Mtoa mada nataka kujua elimu yako kuhusu upande wa madini

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimefanya kazi kwenye sekta hii kwa zaidi ya miaka ishirini ndani na nje ya Tanzania. Kwangu mimi miaka hii imekuwa ni muda wa kukusanya maarifa, uzoefu na umakini. Nimefanya kuanzia ngazi ya chini mpaka kwenye top management level. Class knowledge ni Masters degree.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Bams umekuja na aandiko linalofikirisha sana. Ukiwasikikiza viongozi wetu ni kama wamelogwa na mchawi mmoja. Wanaamini tuna raslimali adimu ambazo haziko pengine popote duniani. Ukiwasikia wanaongelea dhahabu unaweza ukadhani ni Tanzania tu ipo. Njoo kwenye wanyama pori, tuliaminishwa tuna mbuga zenye wanyama ambai hawapo pengine dunia hii. Kumbe wala usiende mbali, nenda hapo Mozambique, Zambia na Drc ndio usiseme. Kuna wanyama makundi kwa makundi.

Anyway inabidi tujilaumu wenyewe kwa kuongozwa na watu wenye elimu ya darasani lakini wenye uwezo duni kiubunifu.
 
Wakati wa bomba la gesi kulikuwa na mbwembwe nyingi jinsi litakavyomwaga mamilioni ya ajira kwa (hasa) vijana wa Kitanzania. Sisikii tena mtu akiliongelea hilo baadla yake wanaongelea ajira za bomba la mafuta.
Ujinga ni kitu kibaya na ndio maana Vitabu vitakatifu vikatuasa kuwa kumuomba Mungu hekima (akili) ni jambo jema zaidi. Tuna mfano wa bomba la TAZAMA na tungeangalia linatoa ajiri kwa watu wangapi (ambao kimsingi ni 'walewale') kabla ya kuliangalia hili ambapo na wenye nalo (Uganda) vijana wao wanafukuzia ajira hizo hizo!
 
Uwekezaji usio na tija ni sawa na jipu la kalio.Huwezi kukaa kwa raha.Kama wawekezaji wenyewe hawana maana watimuliwe tu
Mabadiliko ni muhimu lakini mabadiliko ni lazima yazingatie uhalisia bila ya kupoteza lengo kuu ambalo ni kuongeza mapato, kutengeneza ajira na kujenga uwezo wa ndani wa maarifa. By killing the industry you get none.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M
Katika jambo linaloshangaza ni jinsi Tanzania inavyoonesha kushabikia na kufurahia mradi wa bomba la mafuta ya Uganda. Bomba hili la mafuta ni matokeo ya sera za nchi ya Uganda kuvutia wawekezaji katika utafiti na ujenzi wa miradi ya uvunaji mali za asili za Uganda. Ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu. Uganda imefanya hivyo kwa kupitia sera, sheria na ushirikiano wa moja kwa moja na makampuni ya nje yanayowekeza Uganda.

Tunafurahia mradi wa mafuta ya Uganda wakati kwetu tunafanya kila jitihada za kufukuza wawekezaji kwa maelezo kuwa tunaibiwa. Tunafanya hivyo kwa kupitia sheria zetu mbovu zinazosimamia utafiti wa mali za asili, uvunaji na kauli za viongozi wakuu. Leo karibu makampuni 160 yaliyokuwa yanafanya utafiti Tanzania yamesimama, lakini yanaendelea kufanya utafiti katika mataifa mengine.

Leo kwa kupitia mabadiliko ya sheria zetu mbovu za Prof. Kabudi, hakuna kampuni ya nje itakayokuja kufanya utafiti wa madini ya Tanzania. Vipengere vinavyozuia wawekezaji kuja Tanzania kufanya utafiti wa madini ni pamoja na:

1) Sampuli za madini huwezi kupeleka nje mpaka upate kibali toka GST. Wenzetu wanapunguza urasimu, sisi tunaongeza urasimu. Sheria hiyo imewekwa na watu wasiojua chochote kuhusu utafiti wakifikiria kuwa madini yanaibiwa kupitia sampuli. Huo ni ujinga wa hali ya juu. Unajiuliza ni dhahabu gani inaweza kuwepo ndani ya sampuli ya 1kg mpaka kuwepo wizi wa madini kupitia sampuli! Hivi unapokuwa na grade ya 15g/t, ndani ya kilo moja ya sampuli? Dhahabu itakayowepo ni 15÷1000=0.015g. Gramu 1 ya dhahabu ni kama TZS 50,000. Kwa hiyo 0.015g itakuwa na thamani ya 0.015×50,000=TZS750. Hivi kuna mwekezaji anayeweza kuja kuiba Tanzania TZS 750 kwa kila sampuli? Sheria kama hii inaifanya Tanzania kuonekana nchi ya wajinga watupu.

2) Majibu ya maabara ya sampuli (database) za mwekezaji yapelekwe GST. Unajiuliza kama walioandika sheria hiyo wana uelewa japo mdogo wa biashara ya madini. Utafiti haumwingizii pesa mtafiti hata shilingi moja. Thamani ya mradi anaoutafiti ipo katika data. Ni data hizi, kama zikiwa nzuri ndiyo anaweza kuuza ili kurudisha sehemu ya pesa aliyotumia au ikarudisha gharama na kumpa faida, au asirudishe hata shilingi 1. Serikali inalazimisha ipate data mapema bure!!. Data ni taarifa ya siri ya kampuni kwa sababu usipokuwa makini ya namna ya kuzitoa zinaweza kuua kampuni kwenye share markets. Lazima hiyo kampuni iwe ya wajinga watupu ili kuweza kwenda kufanya utafiti katika nchi yenye sheria kama hii. Kama watakuwepo, basi ni lazima watapeleka data ambazo siyo halisi

3) Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, ndiyo unapata uhakika ule ukweli kuwa academicians are poor managers and poor entrepreneurs. Wanashindwa kutafsiri nadharia walizo nazo kwenye uhalisia. Mabadiliko yale yanamtaka mwekezaji kutoa 16% free carried shares (nchi nyingi zinapata 0 - 10% free carried shares), mrabaha 7% (inajumuisha inspection ya 1%; Dunia nzima ni Mugabe pekee yake anatoza 7% royalty lakini wao wana corporate tax ndogo kuliko Tanzania. Mataifa mengi mrabaha ni 0 - 5%). Bahati mbaya sana Rais wetu amejenga imani kubwa sana kwa academicians, kuna siku atakuja kugundua kuwa they were WRONG PEOPLE FOR THE RIGHT JOB. By then it will be too late.

Kwa mabadiliko ya sheria ya madini ya Kabudi, tutaendelea kuwa na kampuni ambazo tayari zina migodi Tanzania, lakini hatutapata miradi mipya wala wawekezaji wapya. Leo Tanzania inatajwa kama eneo hatari kwa mitaji ya nje. Baada ya mabadiliko ya sheria ya madini, makampuni yote yaliyowekeza katika eneo hatari la Tanzania, hisa zao katika soko la fedha Sydney yalipoteza 30 - 50%.

Kupanga ni kuchagua, lakini kwa nini tufurahie matunda ya sera nzuri za uwekezaji za Uganda wakati sisi kwetu hatutaki kuwa na sera rafiki za uwekezaji? Leo makampuni ya utafiti wa madini yanaondoka Tanzania yanaenda Kenya, Angola, Mali, Uganda, Amerika Kusini na Asia, halafu baada ya miaka 5 tutaanza kushangilia miradi iliyopo Kenya na Uganda.

Wawekezaji wasipopata madini toka Tanzania, watapata mahali pengine Duniani. Katika dhahabu sisi hatupo katika top 15, lakini kuna mataifa zaidi ya 100 yenye dhahabu. Kwa nickel na iron hatupo hata katika top 20. Katika copper, silver, PGEs hatupo hata katika top 50. Tanzanite inapatikana Tanzania tu lakini hii ni saphire yenye vanadium, saphire ya kawaida ipo mataifa mengi Duniani. Zaidi ya yote ni kuwa tanzanite ni kwaajili ya urembo. Kwa nini tuna fikra kuwa ni sisi pekee yetu?

Dunia inaweza kuendelea bila ya Tanzania lakini Tanzania haiwezi bila ya Dunia. Tufanye jitihada mbalimbali lakini tusisahau tumo ndani ya Dunia yenye kila kitu.

Mada ndeeeefu ukweli punje.Tuambie Uganda walitaka bomba hilo lipitie wapi? nini kilifanya lipitie Tanzania na siyo lilikotarajiwa?
 
Tunahitaji wawekezaji wenye FAIDA kwa taifa letu na sio WANYONYAJI wa rasilimali zetu.
 
Tanzania tunashangilia kwa sababu hata bomba la mafuta ni uwekezaji.

Au hujui kuwa huu pia ni uwekezaji ambao serikali imevutia wawekezaji ndio maana wakaamua kupitisha bomba lao nchini.

Teh teh teh!

Kuna TAZAMA. Nadhani hili linatoka Dar kwenda Zambia. Kuna tofauti na hili la kutoka Tanga kwenda Uganda?

Naomba nami nishangiliwe kwani nimefungua restaurant mpya huko Nakapanya. Natarajia kutoa ajira kwa watu kama 20 hivi.
 
Hoja yako ni nini?

Kwa hiyo kama kuna TAZAMA ndio taifa lisishangilie kwa sababu kuna TAZAMA. Hujui kama huu pia ni uwekezaji ambayo makubaliano kibiashara ni tofauti na TAZAMA.

Mama akijifungua hata kama ana watoto wengine lazima hushangilia na kufurahia na familia yake.
 
Nami restaurant yangu ni uwekezaji pia. Hata wewe ukiwa na cherehani tano ni uwekezaji pia.
 
UWEKEZAJI NI NINI?

UWEKEZAJI ni njia ya kufanya fedha zako kuzaa fedha zaidi. Ili uweze kuwa MWEKEZAJI unapaswa kuwa na shughuli inayokuingizia KIPATO KWANZA halafu ndipo unaweza KUWEKEZA sehemu ya kipato chako ambacho kinaweza kutokana na mshahara, kufanya biashara na kadhalika.

Ili uweze kuwekeza unapaswa kuweka akiba ya mapato yako. Tunaweza kujifunza kutoka kwa WABABILON ambapo walitumia HEKIMA YA KUWEKA AKIBA angalau asilimia 10 ya mapato yao ya kila mwezi kwa lengo la KUWEKEZA ifikapo mwanzoni mwa mwaka mpya. NIDHAMU hiyo ilifanya wengi wao kuwa MATAJIRI na BABILON kuwa JIJ TAJIRI zaidi duniani kwa wakati ule na hasa sasa imebakia kuwa SHERIA muhimu ya FEDHA inayomfanya mtu yeyote anayeifuata kuweza KUTAJIRIKA.
 
Katika jambo linaloshangaza ni jinsi Tanzania inavyoonesha kushabikia na kufurahia mradi wa bomba la mafuta ya Uganda. Bomba hili la mafuta ni matokeo ya sera za nchi ya Uganda kuvutia wawekezaji katika utafiti na ujenzi wa miradi ya uvunaji mali za asili za Uganda. Ni matokeo ya utafiti wa muda mrefu. Uganda imefanya hivyo kwa kupitia sera, sheria na ushirikiano wa moja kwa moja na makampuni ya nje yanayowekeza Uganda.
We're too optimistic with oil pipeline kuliko Waganda wenyewe walivyo optimistic with mafuta yenyewe!!!

Mbaya zaidi, ni kama tumesahau kwamba sisi wenyewe kule Lindi kuna mradi wa zaidi ya $30 Billion kwa ajili ya gas processing plant... zaidi ya mara kumi ya ule wa Uganda!!!

Hata hivyo, kinachoendelea hivi sasa only God knows!!!
 
Back
Top Bottom