Hekima na busara

Kwa kweli inakuwa ngumu sana kuyatofautisha maneno haya ingawa bado naamini kuna tofauti hata kama itakuwa ndogo. Mie nafikiri uzoefu uchangia mtu kuwa na hekima. Yaani mtu anafanya maamuzi kwa kuangalia mifano aliyokwishaiona huko nyuma.

Na ndiyo maana jamii zetu zinaamini hekima inamahusiano makubwa na umri wa mtu.

Busara kwa fikra zangu haijalishi una umri gani,hata mtoto mdogo kabisa anaweza kuwa na busara.

Busara nafikiri ni ile hali ya kuwa na utulivu wa mawazo na siku zote kufikiri kabla ya kusema.
 
Naomba msaada wenu wa kujua maana na tofauti ya maneno Hekima na Busara pia ni wakati gani yafaa kutumika.
Kweli nakubaliana na wadau kuwa hekima na busara yana maana zinazokaribiana sana. Unaweza kuyatumia kama "synonyms"-(naomba neno lake la kiswahili kama unajua). Ingawa wapo wanaodhani kuwa hekima mara nyingi mtu huzaliwa nayo ilihali busara mtu hujifunza kutokana na mazingira anayoishi. Inawezekana ikawa kweli lakini bado haitoshi (nionavyo mimi) kuwa tofauti kubwa sana.
 
Neno ilo kwa kiswahili linaitwa: Visawe.
 
Naomba msaada wenu wa kujua maana na tofauti ya maneno Hekima na Busara pia ni wakati gani yafaa kutumika.

kama wadau walivyosema hapo juu..
nafikiri hekima inaweza kuhusishwa na elimu au ujuzi wa jambo fulani. Inaweza kuwa kwa kusomea au kwa kulifanya kwa muda mrefu.

Busara unaweza ukawa umezaliwa nayo, uwezo wako wa asili, unaweza kuwa hujasomea.
ila kwa ujumla maana zinafanana..
 
Kwa mwenye hekima anaweza kuamua shauri gumu linalohitaji ushahidi ambao kwa bahati mbaya inakuwa si rahisi kubaini ukweli juu ya upande wowote katika pande mbili za wahusika wa shauri husika. Hekima za Mfalme (Daudi?) katika biblia alibaini mzazi halisi wa mtoto aliyekuwa akigombewa na akinamama wawili ambao kila mmoja alidai kuwa mtoto ni wake. kwa kutumia hekima aliwaambia 'kwa kuwa kila mama anadai mtoto ni wake inabidi akatwe katikati ili kila mama apate sehemu yake'. mama ambaye mtoto si wake alikubali haraka sana ushauri huo wa kumkata mtoto vipande viwili. Lakini mama ambaye mtoto ni wake alimwambia mfalme "mtoto huyo asikatwe bali aachwe na kupewa yule mama mwingine". Hapo kwa kutumia hekima iliweza kubainika mzazi halisi ni yule aliyekataa mtoto kutenganishwa. Hiyo ndiyo HEKIMA.

Busara ni katika vitendo vya kila siku vya mtu anapowasilina hasa anapojibu hoja mbalimbali. hapo unaweza 'kumjaji' mtu huyo kuwa ana BUSARA au la.
 
Naomba msaada wenu wa kujua maana na tofauti ya maneno Hekima na Busara pia ni wakati gani yafaa kutumika.
Hekima = Wisdom, Knowledge, common sense, Philosophy, Discernment, intelligence

Busara = Wisdom, Astuteness, Foresight, Sagacity, Prudence, common sense, Acumen, Skill, Adroitness, Stratagem, Plan, Intention, Trick, Diplomacy, Tact,
 
Dah! Binafsi bado nachanganya sana busara, hekima. Ni vitu vinavyoenda pamoja na maarifa! Au
 
Hekima ni ule uwezo wa mwanadamu kuwa na maarifa ya kufahamu kipi cha kufanya, kwanini afanye, wapi na kwa wakati gani na Busara ni uwezo wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia hasa uzoefu wa maisha
 
Hekima ni ule uwezo wa mwanadamu kuwa na maarifa ya kufahamu kipi cha kufanya, kwanini afanye, wapi na kwa wakati gani na Busara ni uwezo wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia hasa uzoefu wa maisha
umezunguka pale pale mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom