Hekaya: Kunguru

Hekaya: Kunguru

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,515
Reaction score
20,328
Hapo kale paliondoka ndugu wawili, mmoja ana mke, mmoja hana, wakakaa. Yule asiye na mke, akamwambia mwenziwe, “Nimejua, hapana mke awezaye kusitiri neno. Kama hujui mjaribie mke, wako.” Akamwambia, “Njema.”

Basi katika usiku walikuwako wawili, yeye na mkewe, peke yao, akamwambia yule mwanamke, na uso wake kama akifadhaika sana, “Ee bibi wangu, mpenzi wangu, jambo kubwa la kusitirika limenipata; nataka kukupasha habari nisithubutu.

Hakika yako utafunua. Ukifunua, nimeharibika." Akamwambia, “Hapana hofu. Sisi mwili mmoja na roho mmoja? Faida yako faida kwangu, hasara yako hasara kwangu." Akamwambia, “Haya, sikilize tu. Nilipotoka chumbani leo asubuhi, hashikwa sana na ugonjwa, hataka kutapika, hakakamuka-kakamuka, kumbe hatoka kunguru mkubwa mkubwa kinywani, akaruka kwenda zake, nami ni hofu na kutetemeka.” “Ee Bwana, ajabu hiyo kweli. Lakini hofu hapana. Shukrani tu, kwani kitu kibaya sana kimekwisha kukutoka.

Ilipokuwa asubuhi, wakaamka, mara yule mwanamke fikara zake zote kunguru tu, akamkimbilia jirani, akamwambia, “Ee Rafiki, nimesikia neno la kusitirika sana, lakini wee, ah! sijui, nikuwekee utatoa, hutoi?” "Nitoe wapi? hapana hofu. Sema basi.” "Neno kubwa sana limempata mume wangu. “Neno gani hilo?

Haya sema.” Usiku leo, aliugua sana, akashikwa na maumivu mengi, kumbe kunguru wawili wakubwa wakamtoka kinywani wakaruka dirishani wakaenda zao.” Alipokwisha kutoa maneno yake, yule mwanamke roho yake kama haijambo kidogo, akarudi nyumbani.

Mara hiyo yule jirani amemkimbilia mwenziwe wa tatu, akamsimulia vilevile, ila hii tu, alimwongezea kunguru watatu. Hadithi ikaenea sana. Kila iliposumuliwa, hutia kunguru mmoja juu.

Hatimaye ujirani wote wamesikia yule maskini ametokwa na kunguru hamsini tumboni, hata pana watu wamewaona kundi zima la ndege wakubwa weusi wakiruka dirishani. Wote wakasema, “Mtu huyo mbaya sana, mchawi mkubwa. Tumfukuze kabisa.” Wakaanza kumsumbua sana.

Hana budi kuwaita wote na kueleza asili ya hadithi. Mkewe akapata aibu sana na kuchekwa, watu wa mjini wakafahamu kama. “Mwanamke hasitiri hata neno.”
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom