Hekalu la Gaddafi labomolewa na mabuldoza!

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,598
1,233
Bab al-Aziziya kwishnehi

Lililokuwa hekalu/Ikulu ya Kanali Gaddafi, Bab al Aziziya, limebomolewa rasmi leo Jumapili 16 Oktoba kwa kutumia mabuldoza, nyundo na sepetu. Kwa mujibu wa kongozi mmoja wapo wa serikali ya mpito TNC, "wakati muafaka umefika wa kuanza kubomoa ishara zote za udikteta wa utawala wa Gaddafi". Mtandao wa BBC umemnukuu Afisa Mwandamizi wa jeshi la serikali ya mpito Ahmad Ghargory akisema kuwa eneo la Bab al-Aziziya litageuzwa kuwa hifadhi ya umma

Hadi sasa sehemu ya uwani ya hekalu hilo imekwisha badilishwa kuwa soko la kila wiki ambapo raia kutoka Tripoli na vitongoji vyake huuza bidhaa zao. Sehemu hiyo hapo awali, wakati wa utawala wa Gaddafi, ilitumika kama uwanja wa kuwapokea wageni wa heshima na ndipo mahala Gaddafi alikita hema lake.

Bab al-Aziziya ni jengo mojawapo ambalo lililengwa na mabomu ya NATO karibuni kila siku wakati NATO waliposhambulia Tripoli kwa nia ya kumng'oa Gaddafi toka madarakani.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zilizopigwa wakati zoezi hilo la kubomoa Bab al-Aziziya likiendelea. (Hisani ya Getty Images)
610vvx.jpg
610bbx.jpg
61022x.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mkuu

Hilo lilikuwa ni hekalu?

Champs Elysee analoishi Sarkozy au White house utaliita nini?
Au hata IKulu yetu utasema ni hekalu la Kikwete?

Mbona kulikuwa na gofu pia ambalo ni matunda ya mabomu na missiles za US?

Kweli kasumba za wakoloni zimetuingia. Ilipasa ikulu anayoishi Kwikwete leo tuibomoe, kwani ni jumba(hekalu) alilolijenga Mkoloni.

NTC wameamua tu kwa kushirikiana na US-NATO kuibomoa nchi yao.
Kuna msemo huu. "wajinga ndio ............" Na hivyo ndivyo wafanyavyo NTC.
Ilikuwa hilo "hekalu" walitunze na waligeuze makumbusho.
 
Mkuu hapa unanichanganya kilivyo. Yaani mara kasumba za wakoloni, Champ Elyesee, hekalu la Kikwete au White House. Hivi vinahusianaje na Bab al-Aziziya? Ukisoma vizuri niliandika hekalu/Ikulu. Huwezi kufananisha magogoni, Champ Elyesee au White House na Bab al-Aziziya. Hivyo ni vitu tofauti. Gaddafi alikita Bab al-Aziziya kwa miaka arobaini na mbili, kwa mfano.

Kuhusu kubomoa ikulu anayoishi Kikwete hayo ni maneno yako. Swala hili sijawahi kuligusia kwa kweli!
 
Hawa NATIONAL TERRORISM COUNCIL Wanapigwa sana saiv kwa hiyo wanatafuta sehem ya kudivert mawazo yawatu ili wasijue kuhusu kipigo wanachopata... ni kundi la watu wajinga ambao hawataweza kuitawala hii nchi ya Libya..haikubaliki kabisa eti unavunja ikulu na kufanya soko huu ni ujuha..mbona wameshindwa kuichukua Sirte?!! sasa wanazusha tu habari kwa kushirikiana na majuha wenzao wa BBC,CNN,AFP,AL JAZEERA na wengine ambao wananufaika kwa kuiba mafuta Libya...

Hawataiongoza ile nchi kamwe n u will see...labda NATO ije ikae mle kabisaa otherwise sioni serikali pale..
 
ndio tatizo (on red) la kutokuwa na mfumo wa utawala na kuuheshimu matokeo yake viongozi wanaotawala kuwa wajinga kwa sababu ya kufikiri kwa ajiri ya maslahi yao na mwishowe warithi wao wanakuwa wajinga pia.
Lakini hakuna jinsi nyingine mbali na hiyo mkuu
Hawa NATIONAL TERRORISM COUNCIL Wanapigwa sana saiv kwa hiyo wanatafuta sehem ya kudivert mawazo yawatu ili wasijue kuhusu kipigo wanachopata... ni kundi la watu wajinga ambao hawataweza kuitawala hii nchi ya Libya..haikubaliki kabisa eti unavunja ikulu na kufanya soko huu ni ujuha..mbona wameshindwa kuichukua Sirte?!! sasa wanazusha tu habari kwa kushirikiana na majuha wenzao wa BBC,CNN,AFP,AL JAZEERA na wengine ambao wananufaika kwa kuiba mafuta Libya...

Hawataiongoza ile nchi kamwe n u will see...labda NATO ije ikae mle kabisaa otherwise sioni serikali pale..
 
long live my colonel popote ulipo, ntc wanaprove ujinga wao kwa mara nyingine. wasiishie ikulu tu, wabomoe na majengo yote ya serikali yaliyojengwa na kanali, bila kusahau nyumba alizojengea raia na miundo mbinu yote serikali yake ilijenge ukiwemo ule mradi wa maji kutoka jangwani kwenda sijui ni benghazi, nimesahau pia washushe ile satelite iliyorushwa miaka ya 90! pumbav zao....
 
Ningefurahi zaidi kama NTC wangezira hata kuvichukua visima vya mafuta na badala yake wavikabithi nchi masikini duniani kujikimu. Hapo Tz nasi tungefahidi dume.
.
 
Hawa Jamaa wanadhihirisha ujinga wa wazawa wote wa africa.
wamemfukuza ghadafi, sawa, what the hell do they benefit in coppupting
these structures, au wanadhani ghadafi alikuwa anasema hili liwepo na linakuwapo.

sidhani kama wataweza kujenga hata moja kati ya haya wanayobomoa kijuha namna hii.
 
lntc wanaprove ujinga wao kwa mara nyingine. wasiishie ikulu tu, wabomoe na majengo yote ya serikali yaliyojengwa na kanali, bila kusahau nyumba alizojengea raia na miundo mbinu yote serikali yake .... pumbav zao....

Hili wanalifanya huko Sirte. Jionee hapa

Last edited by a moderator:
Mkuu

Hilo lilikuwa ni hekalu?

Champs Elysee analoishi Sarkozy au White house utaliita nini?
Au hata IKulu yetu utasema ni hekalu la Kikwete?

Mbona kulikuwa na gofu pia ambalo ni matunda ya mabomu na missiles za US?

Kweli kasumba za wakoloni zimetuingia. Ilipasa ikulu anayoishi Kwikwete leo tuibomoe, kwani ni jumba(hekalu) alilolijenga Mkoloni.

NTC wameamua tu kwa kushirikiana na US-NATO kuibomoa nchi yao.
Kuna msemo huu. "wajinga ndio ............" Na hivyo ndivyo wafanyavyo NTC.
Ilikuwa hilo "hekalu" walitunze na waligeuze makumbusho.

Gadhafi is done!
Gadhafi is history just like Saadam Hussein, Osama na Al Awlaki
 
Ni ujinga unaosukumwa na chuki za kikabila.Una eliminate badala ya ku i occupy labda na kuifanyia changes?Kuibomoa ni ujinga mtupu given the fact that zilijengwa kwa pesa zao wenyewe.
Sana sana watakuwa wamefanya hivyo kama vita ya kisaikolojia.However ni ujinga coz it wont work.
 
kupata rais mwenye maono haina maana kuwa na the rest nao wako vivyo hivyo. nadhani tunajionea kwa walibya!
 
Gadhafi is done!
Gadhafi is history just like Saadam Hussein, Osama na Al Awlaki

never, ever! when the libyans will crash into fire and hunger they will realise the absence of col. by tha way banza said, "ikiwa unaona elimu ni ghali...."
 
Ni ujinga unaosukumwa na chuki za kikabila.Una eliminate badala ya ku i occupy labda na kuifanyia changes?Kuibomoa ni ujinga mtupu given the fact that zilijengwa kwa pesa zao wenyewe.
Sana sana watakuwa wamefanya hivyo kama vita ya kisaikolojia.However ni ujinga coz it wont work.

Mkuu wanachofanya kina maana kubwa sana kwa wa-Libya wengi. Haswa hii ni vita ya kisaikolojia, while Gaddafi is at large, walibya wengi bado hawajaamini kuwa jamaa hatorudi tena. kuna jamaa yangu mmoja Mlibya ananiambia hiyo ndiyo symbol ya Gaddafi. Kwa Mlibya yeyote akisikia Baab Al Aziziya ni lazima awe mpole.

Hii inanikubusha issue ya Abu Gharaib ya Iraq na utawala wa Saddam
 
Kam mwenyewe hayupo wataweza kufanya lolote. Bado wanaonyesha ubabe wao. Ngoja akusanye nguvu mpya. Wote watakimbia na watakosa pakujificha. Gadafi kawanyanyua watu wake na wa Africa kwa ujumla. Waje na Tanzania wabomoe msikiti aliojenga Dodoma. NTC wanafanya vitisho ili asjitokeze hata mpenzi mmoja wa Gadafi. Hadi sasa yeyote akijitokeza wanamshoot na wanafamilia wake wote. Dunia na ifahamu kuwa na wao wana siku yao.
 
Back
Top Bottom