Ama kweli wema usizidi uwezo;msemo huu nilipokuwa nikiusikia nilifikiri wanaoutumia msemo huu either walikuwa hawawatakii mema wenzao,lkn nimeona ni ukweli mtupu,watu hawa(wakimbizi)kwa muda sasa wamekuwa wakiripotiwa kuua wenyeji wao bila huruma,wamekuwa wakiweka sumu kwenye mizoga ya wanyamapori na kuua wanyama walao nyama kama simba,chui,fisi,tai na wengineo na kupelekea nchi yetu kupoteza rasilimali hii adimu inayotuletea fedha za kigeni,wamekuwa wakiharibu mazingira kwa kukata miti hovyo, huku wakigoma kurudi makwao kwa visingizio vya kuwa kwao kuna vita,sasa najiuliza maswali mengi ambayo sijapata majibu sahihi,1;ni kwanini watu hawa wanatuua huku wako kwetu na vyombo vya usalama vimekaa kimya?,2;hivi ni lazima kuendelea kuwa na wakimbizi wasio na shukrani katika nchi yetu? kwa kutaja machache.ukienda kigoma na ukanda mzima wa maziwa makuu utawakuta wageni hawa wanafanya shughuli mbalimbali kama uvuvi,na biashara,watu hawa wamekuwa wakiwapiga na hata kuwauwa watanzania wenyeji wa maeneo hayo na kufanya matukio ya kijambazi kwa kukata watu mikono yao maarufu kama ''kaoshi''hakuna lolote linalofanyika kuwafikisha kwenye mamlaka husika,je tuwafanyeje watu hawa? imefika wakati watanzania wamekuwa kama wamkimbizi ndani ya nchi yao.sasa ndugu watanzania wenzangu tuwafanyeje watu hawa wasio na shukrani?...naomba kuwasilisha.