Carica_papaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 797
- 1,297
Hivi Heche anajua Katiba ya Tanzania na Uhuru wa Kufanya Kazi yoyote ili mradi hauvunji Katiba ya nchi? Au ndio wanataka kuleta Udikteta
Shida hujamulewa M/mwenyekiti ,mtu abet kama sehem ya burudani ila sio kama mfumo wa ajira rasmiHivi Heche anajua Katiba ya Tanzania na Uhuru wa Kufanya Kazi yoyote ili mradi hauvunji Katiba ya nchi? Au ndio wanataka kuleta Udikteta
Mtu kama Makalla (Amos Makalla, Katibu Mwenezi wa CCM Taifa) ambaye anawasababisha mnakuwa masikini, utajiri wenu wanawagawia wachina na waarabu anakuja kuwaambia Heche, anapinga betting. Mimi ninataka betting isifanyike, mmiliki uchumi wa nchi hii kwasababu wote mnaweza kuwa matajiri, wote mnaweza kufanya kazi ya kuzalisha.
Wakati hawa watu (CCM) wanawaambia vijana mfanye betting si kulikuwa na kiwanda cha kukata almasi, si kilikuwa kinawaajiri nyie, wameua kile kiwanda kisiwaajiri nyie halafu wanawaambia mkafanye betting. Uhimilivu wa betting ni nini? Ukizeeka utapata mafao kwenye betting? Ukiwa umejiriwa ukizeeka si utapata mafao? Makalla anaongea kitu gani huyo?
Haya magodauni yaliyopo hapa nchini si ya National Milling? National Milling iliajiri watu wa Iringa, halafu nyinyi wanawaambia mfanye betting. Hawa watu wanawaambia vijana wa Tanzania wafanye betting wakati wanaagiza kutoka nje ngano ya Shilingi bilioni 504. Vijana wa Tanzania wanachohitaji uwape trekta, uwape mashine za kuvuna, mbegu, soko, waunde vikundi, waingie kulima ngano, uwape soko wauze wawe matajiri siyo unawaambia kwamba wafanye betting wakati unaagiza ngano kutoka Ukraine, unachukua fedha za ndani unapeleka Ukraine kuagiza ngano"
Nawe wasema haya?Huku kwenye kuchana mikeka angeachana napo kabisa hii ni ajira kamili