Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA-Taifa) Bara John Heche ni mgeni rasmi katika
kongamano la wasomi wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar Es Salaam Mei 25, 2025.
Pamoja na mambo mengine alieleza maazimio ya Kamati Kuu ya Chama kilichoketi kwa siku mbili Makao Makuu ya Chama tarehe 23 na 24 Mei 2025.
Madai
Baadhi ya watumiaji mbalimbali wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakisambaza grafiki yenye ujumbe unaoashiria kuwa Makamu mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ameeleza kuwa kampeni ya No reforms No election imesitishwa kwa muda. Ujumbe wa kwneye grafiki hiyo yenye nembo ya Jambo TV unasomeka;
“TUNASITISHA KAMPENI YA NO REFORM NO ELECTION KWA MUDA - HECHE” Tazama hapa
Uhaisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa taarifa hiyo
si ya kweli. JamiiCheck imefuatilia hotuba nzima aliyoitoa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche iliyorushwa na Tv mbalimbali za mtandaoni ikiwemo Jambo TV, na kubaini kuwa hakuna mahali aliposema kuwa wanasitisha ajenda au kampeni ya No reforms No election.
Heche alitoa maazimio waliyokubaliana kama kamati kuu ambapo miongoni mwa mwaazimio hayo ni kuwa ziara ya No reforms No election itaendelea kama kawaida. Heche alitoa pia ratiba ha tukio hilo kwa siku zinazofuata.
Heche alisema;
“Azimio la pili kamati kuu ya chama imeazimia kuwa ziara ya no reforms no election inayoendelea katika kanda zilizosalia. Sasa kamati kuu ya chama imepitisha ziara ya operesheni kwa kanda sita kama ifuatavyo. Kanda ya kaskazini ziara ya No reforms itaanza tarehe 28 Mei hadi tarehe 1 Juni kisha tuta break kurudi Dar es salaam kwa ajili ya kesi ya mwenyekiti”
JamiiCheck imefuatilia pia kurasa rasmi za mtandao wa X wa
CHADEMA ambapo hakuna taarifa yoyote kuhusiana na kustisha kampeni ya No reforms No election. Aidha hakuna pia taarifa hiyo katika kurasa rasmi za mtandao wa X
John Heche.
Grafiki inayoonekana kuwa na nembo ya Jambo TV pia haijachapishwa wala kutolewa na chombo hicho aidha
walikanusha kuhusika nayo.