Heche Suguta wa NEMC arejeshwa kazini!

Heche Suguta wa NEMC arejeshwa kazini!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Posts
13,185
Reaction score
24,055
Siku chache baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kuwasimamisha kazi, vigogo watatu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kigogo aliyekuwa akisimamia bomoabomoa amerudishwa kazini, imebainika.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia Nipashe zinaeleza kuwa, kigogo aliyerudishwa kazini siku nne tu mara baada ya kusimashwa kazi ni Mwanasheria Mkuu wa NEMC, Heche Suguta.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, Suguta alirudi kazini Januari 29, siku nne baada ya wizara hiyo kutangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha Kusindika Minofu ya Punda kilichopo mkoani Dodoma.

“Heche yuko kazini tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, alikaa nyumbani siku nne tu, ila hatufahamu nini kilitokea juu ya hilo,” kilibainisha.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, hawana taarifa za maofisa wengine kama watarudishwa kazini au laa. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bonventure Baya, alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala la ofisa huyo kurudishwa kazini, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake.

“Jambo hilo siwezi kulizungumza liko juu ya mabosi wangu, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema Baya.

Nipashe pia lilimtafuta Suguta ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake iliita bila majibu na baadaye ilizimwa. Maofisa wa wizara hiyo nao walitafutwa ili kuzungumzia jambo hilo, bila ya mafanikio, hadi Nipashe linakwenda mitamboni.

Wengine waliokuwa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Ofisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.

Katika adhabu hiyo, pia Baya, alitakiwa kuandikiwa barua ya onyo kali la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa Nemc, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.

Kuhusu kiwanda cha Kusindika Minofu, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa Nemc.

Aidha, wizara iliagiza kuwa ndani ya wiki moja Nemc ipitie upya orodha ya wataalam na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalam na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
Chanzo: Gazeti la Nipashe.
 
Something, somewhere went terribly wrong at The Ministry of State in the Vice President’s Office for Union Affairs and Environment.

Inawezekana pia kilio cha wananchi ambao walikuwa wanamlilia Heche kimewafanya wakuu wake wa kazi wakabadili ‘’gear angani’’. In other word, this is people’s power!

Never underestimate the power of the crying majority!

What happened to January Makamba? Is this classic decision u-turn?
 
Heche ni mchapa kazi na kazi zake anazifanya kwa umakini mkubwa.
 
Yaani kumsimamisha yule ilikuwa kosa sana... leo hii pale Mkwajuni watu washarudi tayari na maisha yanasonga, wangempa makali uone ambavo angesafisha nchi
 
Alisimamishwa kwa kuwa ni ndugu wa Mh.John Suguta Heche kutoka CHADEMA nadhani.
Aliyemsimamisha na yeye asimamishwe kwa utendaji dhaifu,February Marope a.k.a mzee wa kupigia salute pig na kuota moto wa ngazi.
Huyu ni Jipu
 
Mmeona udhaifu wa waziri aliyemsimamisha Heche Suguta Manchare? Nilimlilia sana ofisa huyu wa NEMC na nilisema kama ni suala la visasi na majungu Magufuli atamrejesha kazini na kweli karudi, nilisema pia kwamba kwa aina ya utendaji kazi anaouonyesha Makamba hatamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais Magufuli, ama atakuwa wa kwanza kufukuzwa ama ataachia uwaziri mwenyewe kwa kushindwa kazi. Tusubiri.
 
Hah hah hah yule jamaa apewe NEMC awe mkurugenzi, anajua anafanya Nini
 
Mmeona udhaifu wa waziri aliyemsimamisha Heche Suguta Manchare? Nilimlilia sana ofisa huyu wa NEMC na nilisema kama ni suala la visasi na majungu Magufuli atamrejesha kazini na kweli karudi, nilisema pia kwamba kwa aina ya utendaji kazi anaouonyesha Makamba hatamaliza miaka mitano ya kwanza ya Rais Magufuli, ama atakuwa wa kwanza kufukuzwa ama ataachia uwaziri mwenyewe kwa kushindwa kazi. Tusubiri.
Jamaa ni jasiri sana, kazi yake anaijua vizuri.
Tatizo anapenda haki
 
Niliandika siku ile Heche ni shujaa,narudia tena... viva Heche.
 
Back
Top Bottom