Heche Suguta wa NEMC arejeshwa kazini!

Heche Suguta wa NEMC arejeshwa kazini!

Matokeo ya KUKURUPUKA..

Kijana wa UPARA alidhani Mr Suguta ni wale Pig wake aliokua anawapigia salute..
Maarifa kayaweka mfukoni anatumia visasii..
 
hii ni aibu mchana kweupe kwa marope. Kufanya kazi kwa fitina,sifa,na kujikweza aibu yake ndio kama hii, hyu marope buree kabisa.
 
Siku chache baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kuwasimamisha kazi, vigogo watatu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kigogo aliyekuwa akisimamia bomoabomoa amerudishwa kazini, imebainika.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia Nipashe zinaeleza kuwa, kigogo aliyerudishwa kazini siku nne tu mara baada ya kusimashwa kazi ni Mwanasheria Mkuu wa NEMC, Heche Suguta.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, Suguta alirudi kazini Januari 29, siku nne baada ya wizara hiyo kutangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha Kusindika Minofu ya Punda kilichopo mkoani Dodoma.

“Heche yuko kazini tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, alikaa nyumbani siku nne tu, ila hatufahamu nini kilitokea juu ya hilo,” kilibainisha.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, hawana taarifa za maofisa wengine kama watarudishwa kazini au laa. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bonventure Baya, alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala la ofisa huyo kurudishwa kazini, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake.

“Jambo hilo siwezi kulizungumza liko juu ya mabosi wangu, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema Baya.

Nipashe pia lilimtafuta Suguta ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake iliita bila majibu na baadaye ilizimwa. Maofisa wa wizara hiyo nao walitafutwa ili kuzungumzia jambo hilo, bila ya mafanikio, hadi Nipashe linakwenda mitamboni.

Wengine waliokuwa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Ofisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.

Katika adhabu hiyo, pia Baya, alitakiwa kuandikiwa barua ya onyo kali la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa Nemc, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.

Kuhusu kiwanda cha Kusindika Minofu, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa Nemc.

Aidha, wizara iliagiza kuwa ndani ya wiki moja Nemc ipitie upya orodha ya wataalam na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalam na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
Chanzo: Gazeti la Nipashe.
serikali ya kukurupuka
 
Huyu walitaka kumuonea. Awe tu na busara katika kutekeleza majukumu yake. Enthusiasm yake isiwe ya kupitiliza. Tunamtakia kila la kheri.

Sisi huyo waziri anashughulikiwaje?
 
heche chapa kazi bana...../
zipo fitina zilikupitia but....!?/ hatoweza onekana kuwa ni mwema kwa kukusimamisha ww..!!
 
hii ni aibu mchana kweupe kwa marope. Kufanya kazi kwa fitina,sifa,na kujikweza aibu yake ndio kama hii, hyu marope buree kabisa.
Alaaa!!!!! Kila nikionaga neno 'marope' nilidhani watu wanakosea tu nikifikiri walimaanisha 'Malope' - mwimbaji fulani wa nyimbo za injili.
Kumbe ni 'February'!!!!!!!!""
 
Heche kama Ndalichako! Ndalichako alisimamia Taaluma na weledi akiwa Necta na ikamgharimu kwa muda lakini, watu walimkubali! Ndalichako ana nafasi ya kuwa Magufuli wa kesho akiendelea kusimamia ukweli na weledi hata kama wanasiasa hawatapenda!
Kumwondoa Heche ilikuwa ni dhihaka kwa Rais Magufuli na vitisho kwa wote wanaosimamia bomoa bomoa dhidi ya mafisadi waliovamia maeneo ya wazi na fukwe!
Kurudi kwa Heche ni salam tosha dhidi ya wote waliojenga sehemu zisizoruhusiwa!
 
Alaaa!!!!! Kila nikionaga neno 'marope' nilidhani watu wanakosea tu nikifikiri walimaanisha 'Malope' - mwimbaji fulani wa nyimbo za injili.
Kumbe ni 'February'!!!!!!!!""
kama Kweli huyu jamaa alifanya kazi NEMC miaka kama mitano tu sasa hata mtoto anaijua NEMC inaahughulika na nini na kuna idara nyingi sana za serikali ambazo zimelala ...Leo ilikuwa ni makosa sana kuokoteza majungu na kumuondoa badala ya kumuongeza nguvu ...
 
Heche ni mchapa kazi na kazi zake anazifanya kwa umakini mkubwa.
yule jamaa anaumwa sana kuona uharibifu wa mazingira
akienda kwenye viwanda mambo utayasikia hadharani...
kama wachina ukiwambia jamaa anakuja huwa wanaogopa kama nini niliwahi kuingia kiwanda Fulani nikawambia jamaa akifika hapa vipi walifurahi sana vibarua wakisema hapa akifika husimamia hata haki zetu...HECHE NI MTU WA KAZI
 
Kosa lake ni kuwa ndugu wa John Heche wa CHADEMA! Shame on you Makamba.
Nadhani kosa lake kubwa ni kufuata sheria! Wakubwa ni wavunja sheria pamoja na ndugu/jamaa zao!
Jamaa alikuwa haangalii USO wa MTU! Alikuwa anaangalia sheria inasema nini!
 
Magufuli ni msikivu...
Sio kwa ajili ya usikivu, ila ameogopa ukimfukuza kazi mwanasheria kwa kukurupuka utakula hasara kubwa. Hata hao wengine wakitafuta wanasheria wazuri wa kuwasimamia haki zao, serikali itakula hasara kubwa zaidi ya ile iliyopata katika ile ishu ya 'samaki wa Magufuli'. Nilisema hapa kuwa kuna mbwembwe nyingi zinafanyika katika kuwafukuza watumishi wa umma, lakini matokeo yake ni kwamba huwa wanarudishwa kimya kimya kwa aibu ya serikali. Tuwaombee na wote waliofukuzwa kwa kukurupuka kwa serikali hii warudi kazini
 
Ni usikivu mkuu!
Kuna watumishi wangapi wamepigwa chini ?
 
Siku chache baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kuwasimamisha kazi, vigogo watatu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Kigogo aliyekuwa akisimamia bomoabomoa amerudishwa kazini, imebainika.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia Nipashe zinaeleza kuwa, kigogo aliyerudishwa kazini siku nne tu mara baada ya kusimashwa kazi ni Mwanasheria Mkuu wa NEMC, Heche Suguta.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, Suguta alirudi kazini Januari 29, siku nne baada ya wizara hiyo kutangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha Kusindika Minofu ya Punda kilichopo mkoani Dodoma.

“Heche yuko kazini tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, alikaa nyumbani siku nne tu, ila hatufahamu nini kilitokea juu ya hilo,” kilibainisha.

Chanzo hicho kilieleza kuwa, hawana taarifa za maofisa wengine kama watarudishwa kazini au laa. Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bonventure Baya, alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala la ofisa huyo kurudishwa kazini, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake.

“Jambo hilo siwezi kulizungumza liko juu ya mabosi wangu, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema Baya.

Nipashe pia lilimtafuta Suguta ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake iliita bila majibu na baadaye ilizimwa. Maofisa wa wizara hiyo nao walitafutwa ili kuzungumzia jambo hilo, bila ya mafanikio, hadi Nipashe linakwenda mitamboni.

Wengine waliokuwa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Ofisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.

Katika adhabu hiyo, pia Baya, alitakiwa kuandikiwa barua ya onyo kali la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa Nemc, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.

Kuhusu kiwanda cha Kusindika Minofu, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa Nemc.

Aidha, wizara iliagiza kuwa ndani ya wiki moja Nemc ipitie upya orodha ya wataalam na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalam na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
Chanzo: Gazeti la Nipashe.
Mwanasheria anaelewa sheria jamani,Loh Jamaa angeileta serikali. Hapa mahakamani Angepata fidia si chini ya milioni 600!
 
Back
Top Bottom