Heche apondwa na kuitwa mnafiki na Elius Ndabila

Heche apondwa na kuitwa mnafiki na Elius Ndabila

Imefika mahali kila mtu huko ccm akitaka kupata mileage ni lazima amtaje kiongozi yeyote wa Chadema ama aitaje Chadema.

Hata mambo ambayo yako dhahiri kabisa kama hili la wanafunzi kufeli vibaya maccm yanajaribu kuitupia lawama Chadema na wazazi as if huko nyuma wazazi hawakuwepo hadi mwaka 2012 ndio watoto walikuwa na wazazi. Haya ni mawazo na utetezi wa kipumbavu kabisa wakati iko wazi kwamba ccm na serikali yake ndio chanzo cha haya madudu yote.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Anasema, "pamoja na Tanzania kuwa na Mfumo usio na tija kwa watanzania kunatakiwa iundwe tume ya Marekebisho ya Msimbo wa Elimu.Tatizo la watu kukosa fikira wanajua maandano ndiyo mwisho wa Matatizo, badala ya kutafta ufumbuzi wa mda mrefu.
.

Huyu bwana anatuambia kuwa 'mfumo wa elimu hauna tija' na anataka iundwe tume Marekebisho ya Msimbo wa Elimu. Je, Kawambwa na Mulugo wanasema nini? Na kwa miaka yote hiyo 3 wameleta nini jipya, au wamefanya nini ili kuinua kiwango cha elimu? Why should Tanzanians wawaamini hawa watu ambao hawaonekani kuguswa na kushuka kwa kiwango cha elimu?

Dr Shukuru Kawambwa na Mulugo wameajiriwa ili kuongoza Wizara ya Elimu Tanzania (Bara). Wanalipwa, monthly, kwa kazi ya kuongoza wizara ya elimu. Kwa mwaka wa 3 sasa mfululuzo, matokeo yamekuwa mabaya. 3years in a row! Still tuwaamini hao watu?

Kabla ya tume au mjomba wake na tume, wawili hawa wanatakiwa waondoke ofisini.
 
Waambieni watoto wenu/ wetu waache kujifanya wanatumia computa kwenye hizo facebook zitawaangamiza.matokeo ya mwaka huu yamechangiwa sana na mitandao ya kijamii kuwa hivi
 
Waambieni watoto wenu/ wetu waache kujifanya wanatumia computa kwenye hizo facebook zitawaangamiza.matokeo ya mwaka huu yamechangiwa sana na mitandao ya kijamii kuwa hivi

Unachosema utaifakwanza ni kwamba Tanzania sasa hivi iko mbele kwa matumizi ya computer, na access ya internet iko juu! That is what your post says!

Sasa useme, hizo computer wanawashaje wakati umeme unapatikana na asimilia 14 (14%)? Pili, asilimia 75 mpaka 80 ya watanzania wanaishi vijijini. Kwa statitics za sasa, ni asilimia 6.6 tu ndio wana access ya umeme vijijini. Sasa wanafunzi wa shule za kata - ambazo nyingi ziko vijijini- wanawashaje computer?

Na kama kweli tatizo ni computer au hiyo facebook argument yako, iweje watoto wanaosoma shule za International wafaulu zaidi, wakati tunajuwa hawa ndio wana better access na gadget zote -compitur, facebook etc?
 
Ndio maana wanashinikiza Waziri ajiuzulu kwa sababu wao wanazitaja sababu za kufeli kwa uwazi.....hii inaonesha sababu wanazijua tangu zamani ila wameshindwa kupambana nazo kuinua kiwango cha ufaulu........
Kama kiongozi lazima awajibike kwa kukaa kando.....Kawambwa bana sijui wanampendea nini,hakuna wizara aliyoweza kuimudu zaidi ya kuvurunda.
 
Tuitisheni maandamano ya kuuliza jengo walilopanga chadema Kinondoni linamilikiwa na nani na linalipiwa sh. ngapi kwa mwezi...

Do not divert from the true line, hoja yako maina mashiko na inaonyesha jinsi ulivyo na upeo finyu katika kujadili hoja za kitaifa. hata maccm wenzio na mataifa mengine wameguswa na swala hili la ufaulu wa watoto. au hujui kuwa elimu ndo msingi wa maendeleo ya taifa lolote?

unamwasisha nani aandamame kwa ajili ya jengo la chadema, ili iwe nn na kwa faida ya nani?, mali za chama siku zote n faida ya wanachama wa chama husika tu. hapa linaongelewa swala la kitaifa. jaribu kuwa makini unapochangia hoja.
 
Imefika mahali kila mtu huko ccm akitaka kupata mileage ni lazima amtaje kiongozi yeyote wa Chadema ama aitaje Chadema.

Hata mambo ambayo yako dhahiri kabisa kama hili la wanafunzi kufeli vibaya maccm yanajaribu kuitupia lawama Chadema na wazazi as if huko nyuma wazazi hawakuwepo hadi mwaka 2012 ndio watoto walikuwa na wazazi. Haya ni mawazo na utetezi wa kipumbavu kabisa wakati iko wazi kwamba ccm na serikali yake ndio chanzo cha haya madudu yote.


Kwahiyo huko nyuma kulikuwa hakuna CCM na serikali yake mpaka 2012???
 
Kwahiyo huko nyuma kulikuwa hakuna CCM na serikali yake mpaka 2012???
CCM ilikuwepo,ila kila uchao inazidi kudidimia maana badala ya kufanya kazi yenyewe inapambana na Chadema. Kwa mwendo huu wa serikali hii ya CCM, 2013 kiwango cha kufeli chaweza kuwa 80% na 2014 kuwa 90%.
Ona sasa hivi eti tatizo la kufeli ni wazazi,ujinga gani huo?
 
ELIUS NDABILA, yupo Sahihi. Watu mnataka kuingiza siasa kwa vile jamaa ni ccm? Huyo Dogo ninamkubali sana kwa hoja zake. Namfaham tangu akiwa katibu wa fedha UDOM NA SASA KATIBU. Maandamano hayana tija. Hoja hapa ni kuanda sera nzuri ya kuongoza Elimu.
 
Ccm!!!! Kichaa kapewa rungu katikati ya soko. Yaani hamkutaka kumsukiliza Mbatia sasa mnaunda tume. Yaani siwaelewi Ccm wala sitaki kuwaelewa. Hamko madarakani kwa manufaa ya wananchi. Mko kwa ajili ya matumbo yenu. Mlaaniwe milele
 
Angelishauri hio wazo lake kwa jk na wadhaifu wengine walipo serikalini na sio kumueleza heche.kwani heche ana serikali?
 
Haya nayo ni maajabu ya Tanzania. Jamga hili la wanafunzi wa kidato cha nne kufeli, kila mwana-CCM anaelekeza lawama kwa wazazi. Kwa maana kwamba Mawaziri na watendaji wa Wizara ya Elimu hawahusiki.

Mimi ninachokiona ni kwamba, serikali imeshindwa kupata majibu ya kuondokana na tatizo hili. Kwa vile lawama zote zinatupiwa wazazi ni vyema serikali ikawakabidhi rasmi wazazi hii wizara.

Sasa waTanzania kwa macho yetu tunaona jinsi nchi isivyo tawalika. Maana kila kiongozi anakuja na sababu zake kila serikali inapo onyesha kushindwa ki uongozi.

Ni wakati wa kuyaamini yale Dr. Slaa aliyosema kwamba tutafika mahali nchi haitatawalika. wakati wenyewe ndiyo huu.

Mkuu wanaCCM wanafiki, ni aghalabu kumsikia mwanaCCM akikerwa na hali ya mambo ilivyo nchini, wamekalia unafiki tu kulitetea lichama lao hata kama linaboronga wao hawajali, bora mitumbo yao inavimbiwa kila siku. Wako tayari kuuza nchi kwa uroho wa hela na madaraka, tu lichama lao liendelee kuwepo. Limekuwa kokoro la kufichia madhambi yao, wako tayari kulilinda kwa gharama yoyote ile!
 
huyu jamaaa K.....a kweli kweli yaani Magamba hata yaone nchi hii inazama kwenye na inaonekana kwa kila mtu hata mtoto wa miaka 5 lkn yenyewe yatasema no mbna maji yenyewe hata magotini hayajafika njaa zenu Magamba zitawauwa,mwisho wenu ni sasa hebu mtupishe sie tuwaongoze Watanganyika na si kuwatawala kama mfanyavyo kazi kulindana tu.Hapo huyu njaa kapewa chake aende redion kutoa huu Us...h.....u.....zi
 
Tuitisheni maandamano ya kuuliza jengo walilopanga chadema Kinondoni linamilikiwa na nani na linalipiwa sh. ngapi kwa mwezi...
hapa ndipo mnapoonesha MLIVYO WACHUMIA TUMBO KWANI MAANDAMANO YA CHADEMA KUPANGA YANAMADHARA GANI?
 
HALAFU WATOTO WA mama mlao pilau msijipime na dogo heche yule ni jembe sana
 
ELIUS NDABILA, yupo Sahihi. Watu mnataka kuingiza siasa kwa vile jamaa ni ccm? Huyo Dogo ninamkubali sana kwa hoja zake. Namfaham tangu akiwa katibu wa fedha UDOM NA SASA KATIBU. Maandamano hayana tija. Hoja hapa ni kuanda sera nzuri ya kuongoza Elimu.
kaa lenu la moto ni heche akizungumza mnasajili id fake kumi za kujibu japo napo mnachemka hivi hiyo hoja ya kujipanga itakamilika lini maa na sasa mi nao na kama tunabomoka nyie hamuoni au ndio kusema mmeshiba posho ya nape
 
Mfumo wa utawala wa nchi hii ni kwamba ukijiuzulu
1. Umeshajiua kisiasa
2. Umeshakiharibia chama chako
3. Unaonekana ni dhaifu
4. Unaonekana fisadi
Mara ya mwisho kujiuzuru kwa kiongozi alikuwa lowasa na yeye nadhani alijuta kwa nn alikubali kubwaga manyanga. Haitatokea tena kiongozi wa ccm kujiuzuru mpaka 2015
 
Back
Top Bottom