Hebu tuzungumzie scientific research | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu tuzungumzie scientific research

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by mamanalia, Nov 16, 2009.

 1. m

  mamanalia JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 671
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapa kwetu TZ siku hizi kuna watu wengi wanaitwa Dr. somebody au Prof. somebody. Lakini ukienda kwenye strong journals duniani huwakuti kabisa majina yao katika articles. Hivi huwa wanapata hizo PhDs na uProf. vipi? Yani mtu anajiita Prof halafu anakaa miaka hajafanya publication? hata wanafunzi wa masters tu amewakosa ili waweze kuproduce papers! Inabidi tuchunguze au nako huko vyuoni kuna ufisadi wa kuinuana tu na kupeana u prof kwa reports za hapa na pale na vijiconference vya morogoro, arusha na dar?
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mama... hilo umeligundua leo? Lipo tena kwa sana. Jaribu kuchukua majina ya walimu wako (Ma-Dr na Ma-Prof) halafu uyachape kwenye search engine za maana kama Pubmed, usishangae kukuta mtu hayumo! Kuna mwalimu wangu ana paper moja tu kwenye Pubmed!!

  Hata hivyo mambo ya Sayansi hayana mshiko hapa JF. Ni siasa kwa kwenda mbele!!:rolleyes:
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kabisa Mkuu hivi hii inakuaje?
   
 4. Mpogoro

  Mpogoro JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 361
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yeah,JF haina mshiko sana kwenye Science.Siasa imezidi sana humu ndani.Hata hivyo ili ku-improve ushiriki wa watu kwenye category ya science and technology....wakuu wangevunja badala ya kuwa na science and technology tungekuwa na categories nyingi nyingi ndogo ndogo ambazo ziko very particular mfano MEDICINE,COMPUTER SCIENCE etc.....yaani maeneo ya namna au tunaweza ku-break down further ili mtu achague interest yake....

  Mtazamo tu...
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Labda hiyo inaweza kusaidia lakini uzoefu wangu wa hapa jamvini unaonesha kuwa ni watu wachache sana wanapenda kusoma mambo ya kisayansi hata kama ni habari tu! Inasikitisha sana kwa sababu post za siasa zinapaa sana kuliko nyingine zote. Hata mambo ya mapenzi yana washabiki wengi tu lakini siyo sayansi ya aina yoyote (be it social or natural science)!! Labda tupate maoni ya wadau wengine ila kama ingewezekana huu ukumbi ungesaidia sana kuwa tunapeana habari kuhusu breakthroughs zinazofanyika katika anga mbali mbali za S&T.
   
 6. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,189
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Wasomi wengi wamegeuka wanasiasa!
  Sasa watu kama Prof. Msola ndio hao wameamia kwenye siasa, huo utafiti utafanywa saa ngapi?! Tatizo letu bongo ni misallocation of resources (ikiwemo rasilimali watu) na kushindwa kutofautisha politik na academics.

  Utafiti wa kisayansi unahitaji kuwekeza pesa nyingi sana jambo ambalo Tz hatujalipa kipaumbele. Nadhani kama kungekuwa na tafiti za kutosha, ugonjwa kama malaria lisigekua tatizo kwa sasa!
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Professor Majimarefu,Professor Vulata(RIP),Dr Remmy Ongala...hawana research papers
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  wengi hapa bongo ni vyakupewa kisiasa siunajua tumetawaliwa kisiasa zaidi
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwi kwi kwi,
  Nafasi ya kupenya BOT kama wewe mwanasayansi utaipata wapi? Hata hiyo ya kufundisha tu huipati hata kama uwezo unao kama wewe sio ndiyo mzee! Kamulize Prof Baregu!

  Wakati wenzenu wanagawana keki mil 30, 50, 100, nyie mnagawana mmba kwa ajili ya kukuna kichwa, eti sayansi!

  Hadhi Tz itarudi pale wasomi watakapoona nafasi yao na kuacha kuwabeba wanasiasa kwa mbeleko. Wajisikie huru kusimama popote sio ndani ya ccm tu, na hapo ndipo wanapoweza kuwa na nguvu ya kuanisha pumba na mchele uko wapi! Hatujiulizi ni kwanini wanasiasa uchwara wana nguvu ya kupindukia?
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Nono, nimekupa senksi na kama ingeruhusiwa ningekuongezea.

  Tz ni nchi ya ajabu. Juzi nilisikia Pinda anamfokea Injinia huko A-town. Heshima kwa wataalamu hakuna na wasomi badala ya kupigania haki yao ili waheshimiwe na kuthaminiwa wameingia mkenge wa kukimbizana na kura ili wakapige porojo. Wakati Sarungi alipoikimbia MOI pale Muhimbili na kuwa mwanasiasa tulimshangaa sana. Kwa sasa hakuna tatizo tena. Baraza la mawaziri tu lina maprofesa kibao na PhD za kumwaga (ingawa nyingine ni za kichina). Hapa hatutoki kabisa. Tumetumbukia kwenye matope!!
   
 11. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  very funny...
   
 12. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  habari ndiyo hiyo! katika nchi za wenzetu mtu anakuwa Dr. lkn sio prof. kwani unaweza kuwa Dr. kwa kusomea degree tu (baada ya masters), baada ya hapo kama hujafanya mambo ya risachi zaidi wewe utabakkia Dr. fulani tu...ukifanya risachi na ukafanikiwa ku publish 'journals', kuhudhuria international conferences ndio wanaangalia namna ya kukupandisha kwenda assnt prof, assoc prof na prof. hatua hizi zote ni mpaka uwe na uzoefu kazini na publication za maana. lkn bongo sivyo...kamati zinakaa tu na kuamua aaah fulani sasa ni Prof teh teh teh teh...
   
 13. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mzee, nimelazimika kuchangia baada ya kuona hilo nililokoleza wino! hujatembea wewe!!!!!!!, ukifika china na kuona maendeleo waliyopata kwa miaka 60 ya uhuru wao, hutadharau tena elimu yao na wala hutasaga bidhaa za china kwa greda eti "feki".

  china leo wanamalizia kuweka metro kwenye tu-miji tudogotudogo, tena bila msaaada wa kiufundi, wala wa kifedha toka kokote nje ya china!!! we hapo bongo tunaweza kufanya nini??? hata barabara korofi hazitengenezwi hadi tutemewe mate na wazungu!!

  hata huyo sijui sarungi aliyekuwa na elimu unayoiabudu, alipokuwa moi alifanya nini? wagonjwa walikuwa hawapelekwi nje kwa matibabu ya mifupa? ndi maana alipoona hafanyi kitu akajisalimisha kwenye siasa! tafakari kidogo ndugu kabla hujaingia jamvini!
   
 14. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Naona unajaribu kuchukulia issue hii personal wakati mimi nimechangia kiujumla. Kama unaishi Tanzania kwa sasa utakuwa unaelewa maana mtu anaposema kitu ni cha kichina. Kama hujakutana na hilo neno basi pole na omba watu wakusaidie, badala ya kuanza mashambulizi yasiyo ya lazima. Kwani bidhaa za feki za kichina hazipo Kariakoo na kwingineko? Kama ulitaka kueleza kuwa wachina wanafanya vitu genuine basi tueleze viko wako wapi katika soko letu? Watu wanaongelea wanachokiona na siyo hadithi. Kama kwao wanatenegeneza vitu vya maana wakati sisi tunaletewa feki bado tutawaponda tu!
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mimi siwalaumu sana kwenye ku-publish, maana hata huko kwenye majournal 'siasa' imeshaingia na ku-dominate kwa kiasi flani. Tatizo ninaloliona mimi ni mchango wao ktk fani husika. Je wana input yeyote hata kama ni ndogo? Wana-website kuonesha currently wanafanya nini? au wapo kwenye initiative ipi? wanaendaje na mabadiliko ya haraka ktk uvumbuzi..etc..
   
 16. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa sasa siko tz lakini huo msemo naufahamu, nieshawishika kutahadharisha baada ya kuona hata great thinker anaponda bidhaa za china!

  labda nikuulize, kama kitu ni feki na kinafanya kazi iliyokusudiwa na kinauzwa kwa bei nafuu ili kila mtu amudu kununua, kuna madhara gani? ningefurahi kama wangefanya kazi ya kuvi-study vtu ivyo ili kuangalia namna ya kukopy technolojia rahsi badala ya kuviponda ukiwa huna kitu katika soko lako cha kujivunia!

  tunapaswa kuacha kasumba ya kushabikia vitu vya ulaya kwani hata huko nako kunatoka feki.

  ili utengeneze genuine unaanza na na kitu (whether feki or otherwise) kisha unaendelea kuboresha. ndivyo walivyofanya hata ulaya na wanaerndelea kufanya hivyo hadi leo. hivi vitu mnavyoita feki huwa vinatolewa kwa bei nafuu ili kila mtu amudu kununua. ndivyo ilivyo hata kwa magari yaliyotumika. wangecrash magari yote ya mitumba, wangapi dar wangekuwa na magari? achilia mbali nguo!

  tuamke,tujitetee,

  hao wanaocrash vitu kwa madai ni feki wamo kwenye payrol ya mafisadi na wanwasafishia njia wauze mizigo bila ushindani, kama ulikuwa hujui, habai ndiyo hiyo!
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi sina ugomvi na vitu vya bei rahisi au vya kutoka china. Kwenye ile post yangu nilitumia neno kama wanavyotumia wengine (loose meaning). Hata hivyo napata shida kwa jinsi hali ilivyo sasa hapa Tz ambapo mtu unahahikikishiwa na wauzaji kuwa kitu ni genuine kumbe ni feki toka china. Hapo ndipo ugomvi unapoanzia. You pay deally to get fake stuff! Kama tungeletewa genuine kama bidhaa zinazopelekwa Ulaya na US hayo huo ugomvi usingekuwepo. Wachina kushirikiana na wahuni na mafisadi kutuibia kunaleta damage kwa pande zote mbili. Kwa hiyo Wachina hawawezi kukwepa lawama ingawa ujinga ni wetu na sisi (Watanzania) ndio tunabeba lawama kubwa!

  Hapo tuko pamoja. Ndio maana tunalalama kuwa kama siyo kutelekeza sayansi na elimu kwa ujumla tusingekuwa tunaagiza hata viberiti toka China.
   
 18. shejele

  shejele Senior Member

  #18
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Unachosema ni kweli kabisa. Kuna mkanganyiko mkubwa sana, kila kitu kinawekwa kisiasa zaidi kuanzia uandikaji wa proposal hadi kupata permit ya kufanya research sasa haishangazi kuona hata wanascience wenyewe wamegeuka wanasiasa.
  Ukweli ni kuwa watu tuko after money zaidi,na hizi pesa za tafiti za kisayansi mara nyingi zote zinaishia hukohuko kwenye tafiti kwa hivyo haziwapi watu ushawishi.
   
 19. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thread na posts nimezipenda.
  Kila mdau afanye homework vizuri,tusiridhike na tulipofikia,tuzidishe kusoma,kufikiri ,ku share idea...tuondoe kubaniana vyuoni,tuwe more practical na tujiamini kuwa tunaweza kufanya.
   
 20. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekupata vizuri sana mkuu, sasa tumewekana sawa. muhimu tuendeleze harakati za kuleta mapinduzi ya technolojia ya viwanda nchini mwetu..............

  asante pia kwa kujadili nami kwa lugha njema
   
Loading...