Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,548
- 860,660
Kama Imethibitishwa kuwa kuna watumishi elfu arobaini waliogushi umri, mnafanya uhakiki wa nini tena. Sio kwa vituko hivi!
Tunajua kizungumkuti kilichotokea kwenye kusaka watumishi hewa, halafu likafuatia zoezi lenye makengeza mengi la walioghushi vyeti... Zoezi hili lilifeli vibaya kwakuwa kuna maeneo hawakuthubutu kuyagusa kabisa huku baadhi ya watumishi wakiachwa ilihali wamethibitika kughushi.
Haya ya kupandishwa mshahara tuyaache kama yalivyo lakini hili la KUHAKIKI UMRI..... HAPANA si la kukalia kimya!
Umetumika mtambo gani huo kung'amua hili? Hili zoezi limechukua muda gani? Kwahiyo sio watumishi hewa na hawajaghushi vyeti ila wameghushi UMRI.... na mnataka kufanya uhakiki tena! Wa nini sasa wakati tayari mna takwimu zake?
OK huu uhakiki utachukua muda gani? Mnaua morali wa kazi kwa watumishi kwa kasi kubwa mno halafu bila sababu za msingi... Kwa hali hii tusitegemee matokeo makubwa yenye ufanisi huko serikalini... Maana watumishi wa uma wamekuwa kama vibaka....!!! Kibaka ni mtu wa kusingiziwa kila kitu.
Nina wasiwasi zoezi la kuhakiki umri likiisha litafuata la kuhakiki nyeti/jinsia... Hili litafanyika 2018, halafu 2019 litakuja la kuhakiki makabila na rangi..
Tupumzisheni kidogo tuwaze mengine sasa.. Hizi hakiki zimetukifu pomoni..