Hebu ona mwenzako nilivyoanza kujiajiri!

Hongera kwa uthubutu ila hujatuambia hizo pesa za kulima heka 8 nani kakuwezesha
 
Vijana, kumbe tukithubutu tunaweza! Wakati nikiwa nasubiri ajira rasmi nikaona si vema kukaa nyumbani idle, nikakodisha shamba la takribani hekari 12 maeneo ya huku kwetu Tanga, lakini kwasababu naanza nikatumia hekari 08 tu kwa kupanda mahindi, nashukuru kwamba karibu asilimia 99 ya sehemu niliyoitumia imekua ni ya mafanikio kwani mahindi yamechomoza vizuri sana yakisaidiwa na mvua za rasharasha zinazoendelea Wilayani kwetu. Sasa naielewa vema dhana ya Kilimo Kwanza.

Ushauri kwa Vijana wenzangu wa humu JF: Kwa wale mliomaliza Vyuo Vikuu kama mimi (bila kuzingati fani uliyosomea) na bado hamjaajiriwa, au hata kama hukufanikiwa kufikia level hiyo ya elimu ya Chuo Kikuu, tafadhali usibweteke nyumbani, unaweza kujaribu na kwenye kilimo tena bila kuona haya (weka ubishoo/ulimbwende pembeni). Kilimo ndio habari ya mujini...

Mimi nimemaliza degree ya Sheria Chuo Kikuu Mzumbe lakini nimejiajiri kwenye Kilimo, wewe mtoto uliyesoma Diploma ya Sociology Ustawi wa Jamii unaleta Uyoyoo! Shauri lako!
mkuu kwanza hongera kwa kuthubutu!ila bado hujaweza! nakuomba urejee stick thread ya kwanza kwenye jukwaa la business /sub forum ujasiriamali kuna mtu anaitwa @elnino alikuja na mikwara zaidi yako alafu kilichompata huko kwenye kilimo utakisoma mwenyewe!maana alikuwa anatupatia mrejesho
jambo kubwa nikukumbusha kuwa kilimo sio lelemama jitahidi muombe Mungu utafanikiwa na usiwatukane wala kuwakejeli wenzako ambao hawajathubutu! Hata mimi nipo kwenye kilimo ila upande wa ufugaji najaribu nami ili nipunguze ukali wa maisha hasa kwa sisi waajiriwa
i wish best of luck! Mungu akutangulie ktk yote
 
Kila mtu anang'ang'ania "bado sijavuna bado sijavuna", jamani utavunaje bila kupanda? mm najivunia kwasababu NIMETHUBUTU (kwa kupanda), na ww umeshathubutu kwenye eneo lipi???

Wasikukatishe tamaa hawa ndo unawasema mtu kumaliza form IV anajiona star jembe hataki kushika. Mimi kama wewe nilimaliza Form VI wakati nasubiri chuo nikaanza kulima mchicha (ikumbukwe ni ktk eneo maarufu hapa mjini ambapo maji hayakati ovyo na wanakaa wakubwa mimi sikujali hayo) kwani nilitafuta tempo maofisini mpaka nikaishiwa nauli iliyotokana na zawadi za kumaliza Form six na kufaulu. Watu walisema sana lakini pesa niliyoipata ilinisaidia sana mpaka hapa nilipofikia. Mimi ndo najua.

Pia nilipomaliza chuo kabla ya kupata kazi niliyosomea nikaanza kujipaka chaki, watu wakaosha vinywa vyao kama kawaida, nakwambia kama siyo tempo ile sijui ningekuwa wapi hivi sasa maana gazeti lenye tangazo niliipata pae shuleni na pia nilipewa mbinu na walimu wazoefu za interview nikashinda na baadaye nilianza kubadilisha kazi kama nipendavyo. Jamaa waliojifanya MABISHOO walilijua jiji. Siyo kama najivunia bali naeleza ukweli mtupu.

Naendelea kukupa MOYO kuwa "Something is better than nothing" na kumbuku kuwa "Jembe alimtupi mkulima"
 
Vijana, kumbe tukithubutu tunaweza! Wakati nikiwa nasubiri ajira rasmi nikaona si vema kukaa nyumbani idle, nikakodisha shamba la takribani hekari 12 maeneo ya huku kwetu Tanga, lakini kwasababu naanza nikatumia hekari 08 tu kwa kupanda mahindi, nashukuru kwamba karibu asilimia 99 ya sehemu niliyoitumia imekua ni ya mafanikio kwani mahindi yamechomoza vizuri sana yakisaidiwa na mvua za rasharasha zinazoendelea Wilayani kwetu. Sasa naielewa vema dhana ya Kilimo Kwanza. Ushauri kwa Vijana wenzangu wa humu JF: Kwa wale mliomaliza Vyuo Vikuu kama mimi (bila kuzingati fani uliyosomea) na bado hamjaajiriwa, au hata kama hukufanikiwa kufikia level hiyo ya elimu ya Chuo Kikuu, tafadhali usibweteke nyumbani, unaweza kujaribu na kwenye kilimo tena bila kuona haya (weka ubishoo/ulimbwende pembeni). Kilimo ndio habari ya mujini...Mimi nimemaliza degree ya Sheria Chuo Kikuu Mzumbe lakini nimejiajiri kwenye Kilimo, wewe mtoto uliyesoma Diploma ya Sociology Ustawi wa Jamii unaleta Uyoyoo! Shauri lako!
Mungu akusaidie mwanasheria wangu....ni mfano mzuri wa kuiga
 
Nawashukuru sana Nyati na Sir M.D Andrew kwa kunipa moyo
 
Wingu, nilibahatika kuwepo kwenye zoezi la sensa kama msimamizi, ile ela nilipoipata niliiweka kwenye fixed account crdb, ndo nimeitoa hivi majuzi ikawa imeongezeka kdg na ndio hiyo nimewekeza kwenye Kilimo kwanza
 
ila kumbuka kuwa kila binadamu ananjia yake pekee ya mafanikio,ulipo pitia wewe siyo sawa na atapo pitia mwingine,kwahiyo huwedhi tambua yawedha kuwa mwingine "ubishoo" ndiyo njia yake ya mafanikio na wala siyo kilimo

Umeongea Ujinga saana. Nadhni hujui maana ya Neno UBISHOO. Hakuna ajira inaitwa Ubishoo . Kama una Mtoto wako au ndugu yako Embu Jaribu Kumpa Nguvu ya kufanya Ubishoo ili afanikiwe. Acha Kuongea Ujinga ..
 
Hahahah...mkuu unatokea Mkoa wa Ziwa Magharibi?...naona majivuno mengiiii
Halafu nadhani umesahau kuwa huko ulikolima ni TANGA...
 
Vijana, kumbe tukithubutu tunaweza! Wakati nikiwa nasubiri ajira rasmi nikaona si vema kukaa nyumbani idle, nikakodisha shamba la takribani hekari 12 maeneo ya huku kwetu Tanga, lakini kwasababu naanza nikatumia hekari 08 tu kwa kupanda mahindi, nashukuru kwamba karibu asilimia 99 ya sehemu niliyoitumia imekua ni ya mafanikio kwani mahindi yamechomoza vizuri sana yakisaidiwa na mvua za rasharasha zinazoendelea Wilayani kwetu. Sasa naielewa vema dhana ya Kilimo Kwanza.

Ushauri kwa Vijana wenzangu wa humu JF: Kwa wale mliomaliza Vyuo Vikuu kama mimi (bila kuzingati fani uliyosomea) na bado hamjaajiriwa, au hata kama hukufanikiwa kufikia level hiyo ya elimu ya Chuo Kikuu, tafadhali usibweteke nyumbani, unaweza kujaribu na kwenye kilimo tena bila kuona haya (weka ubishoo/ulimbwende pembeni). Kilimo ndio habari ya mujini...

Mimi nimemaliza degree ya Sheria Chuo Kikuu Mzumbe lakini nimejiajiri kwenye Kilimo, wewe mtoto uliyesoma Diploma ya Sociology Ustawi wa Jamii unaleta Uyoyoo! Shauri lako!
hongera sana,ila Mungu akuepushe na ugonjwa mpya wa mahindi kwa maana ni majanga
 
Ushauri wa bure: Ukifanikiwa kuvuna next time usitegemee mvua, tafuta namna ya kumwagilia shamba lako. Vinginevyo.......!
 
Hongera kwa kuthubutu. Wanaozungumzia kuhusu kuvuna hawana nia mbaya kabisa. Unategema mvua hivyo mvua kama zitaacha kunyesha au zikinyesha nyingi kupita kiasi basi unaweza kutoambulia kitu kutoka shambani kwako na hii ndio maana wanasema subiri uvune ndio ujipige kifua.

Kila mtu anang'ang'ania "bado sijavuna bado sijavuna", jamani utavunaje bila kupanda? mm najivunia kwasababu NIMETHUBUTU (kwa kupanda), na ww umeshathubutu kwenye eneo lipi???
 
Umekosea sana kwa kudharau mtu anadiploma ya ustawi wa jamii kajibweteka, na ww unadegree ni mkulima, haijalishi unaweza kuawa na hata masters umesoma Oxford university na ukawa muuza matunda!! Kila mtu anastyle yake yakutafta maisha bana!! Usiwe hivyo fikiria kwanza!! Mwanzo wa mada ulikua mzuri sanaaa ila mwishoni ukaanza kuboronga!! Anyway all the best!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Vijana, kumbe tukithubutu tunaweza! Wakati nikiwa nasubiri ajira rasmi nikaona si vema kukaa nyumbani idle, nikakodisha shamba la takribani hekari 12 maeneo ya huku kwetu Tanga, lakini kwasababu naanza nikatumia hekari 08 tu kwa kupanda mahindi, nashukuru kwamba karibu asilimia 99 ya sehemu niliyoitumia imekua ni ya mafanikio kwani mahindi yamechomoza vizuri sana yakisaidiwa na mvua za rasharasha zinazoendelea Wilayani kwetu. Sasa naielewa vema dhana ya Kilimo Kwanza. Ushauri kwa Vijana wenzangu wa humu JF: Kwa wale mliomaliza Vyuo Vikuu kama mimi (bila kuzingati fani uliyosomea) na bado hamjaajiriwa, au hata kama hukufanikiwa kufikia level hiyo ya elimu ya Chuo Kikuu, tafadhali usibweteke nyumbani, unaweza kujaribu na kwenye kilimo tena bila kuona haya (weka ubishoo/ulimbwende pembeni). Kilimo ndio habari ya mujini...Mimi nimemaliza degree ya Sheria Chuo Kikuu Mzumbe lakini nimejiajiri kwenye Kilimo, wewe mtoto uliyesoma Diploma ya Sociology Ustawi wa Jamii unaleta Uyoyoo! Shauri lako!
pamoja na kuwa watu wengi wamekusifia umethubutu lakini mi sijakusoma halaf naona kama vile unaleta stori za maskani au ni mtu ambaye una support kutoka sehemu nyingine aidha kwa wazazi au watu fulani, unapoleta thread kama hizi fikiria wale watu ambao walisoma shule za serikali au alilipiwa lakini baada ya kumaliza hamna msaada mwingine mkubwa wa kifedha atakaopewa zaidi ya nauli ya kwenda mjini ambayo ni buku, haya ngoja nikuulize halaf tuone kama dizain ya watu niliowataja watamudu au kw wataziweza izo gharama sio kuishia kutukana watu ovyo1. Hilo shamba la ekari 12 umekodi kwa kiasi gani ? So unafikiri watu wote waliomaliza chuo wanazo ?2. Na izo ekari 8 uliingia shambaoi mwenyewe kupiga jembe,? Kitu ambacho siamini. Au ulikodi vibarua au ng'ombe au trekta na kwa kiasi gani ? Nayo unafikiri wote waliomaliza chuo wanazo ?3. Gharama nyinginezo upaliliaji, mbegu.Haya gharama zote hizo ulipata wapi ? Your learned brother
 
Back
Top Bottom