Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 5,352
- 7,668
Vijana, kumbe tukithubutu tunaweza! Wakati nikiwa nasubiri ajira rasmi nikaona si vema kukaa nyumbani idle, nikakodisha shamba la takribani hekari 12 maeneo ya huku kwetu Tanga, lakini kwasababu naanza nikatumia hekari 08 tu kwa kupanda mahindi, nashukuru kwamba karibu asilimia 99 ya sehemu niliyoitumia imekua ni ya mafanikio kwani mahindi yamechomoza vizuri sana yakisaidiwa na mvua za rasharasha zinazoendelea Wilayani kwetu. Sasa naielewa vema dhana ya Kilimo Kwanza.
Ushauri kwa Vijana wenzangu wa humu JF: Kwa wale mliomaliza Vyuo Vikuu kama mimi (bila kuzingati fani uliyosomea) na bado hamjaajiriwa, au hata kama hukufanikiwa kufikia level hiyo ya elimu ya Chuo Kikuu, tafadhali usibweteke nyumbani, unaweza kujaribu na kwenye kilimo tena bila kuona haya (weka ubishoo/ulimbwende pembeni). Kilimo ndio habari ya mujini...
Mimi nimemaliza degree ya Sheria Chuo Kikuu Mzumbe lakini nimejiajiri kwenye Kilimo, wewe mtoto uliyesoma Diploma ya Sociology Ustawi wa Jamii unaleta Uyoyoo! Shauri lako!