Headmaster Karatu boys; Serikali ya CCM inastahili grade F

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
329
500
Akichangia katika Mkutano Mkuu wa Taifa wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania Bara _ TAHOSSA unaoendelea mjini Dodoma katika ukumbi wa Chuo cha Mipango.

Mkuu huyo alisema Serikali ya CCM imeshidwa kabisa kutoa ruzuku za kuendesha shule zake kwa wakati na kwa kiwango kinachositahili na kusababisha wanafunzi kuishi maisha magumu, akiongea kwa uchungu huku akishangiliwa na wakuu wa shule wenzake aliwakosoa kwa kiwango kikubwa watendaji wa Wizara ya Elimu na Halmashauri nchini kwa kushindwa kuzihudumia shule.

Baada ya kumaliza kuongea aliombwa na Mkurugenzi wa Elimu Sekondari kutaja jina lake na shule anayofundisha.

Baada ya kumueleza kuwa yupo Karatu Sekondari, wajumbe walizidi kumshangia na wengine kumpa mikono ya kumpongeza baada ya kumaliza kuongea.

Akifungua Mkutano huo wa siku 3, Waziri wa Elimu Dr. Kawambwa aliwaambia kuwa Mbowe na wenzake hawasitahili kumbebesha lawama juu ya kufanya vibaya kwa shule za sekondari kwani walishazikabidhi TAMISEMI tangu 2008.

Aidha aliwakumbusha kuwa kuendelea kumuita ni mzigo katika wizara hiyo kunatokana na watendaji wa wizara yake kuwa mizigo na atahakikisha anasafisha wizara kabla ya kusafishwa yeye.

Mkutano huo utamalizika kesho jumamosi mchana.
 

Lokissa

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
7,444
2,000
Wizara ya elimu ina mawaziri mzigo wasiojua hata Tanzania ni muungano wa nchi gani
Watendaji kuwa mzigo sitoshangaa
Maana baba na mama wakiwa mizigo hata watoto hufuata nyayo zao

Ningefurahi kama kungekuwa na mkutano wa aina hiyo katika vyo vikuu
Watu ndo wangejua nini kinachofanyika Tz
Elimu sio tuu imeanguka mashuleni hata vyuo vikuu
Lacturers na wanafunzi wa vyuo vikuu wako kwenye wakati mgumu sana
Hiyo ndo Taz
Elimu ya wakenya kwa sasa huwezi kuifananisha na tz kamwe wenzetu wako mbali mno
 

MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,258
0
kwishaaaaa!!!!! mwambieni akakamate chaki maana washamtoa kwenye "bank of Headmasters"
 

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
329
500
Amewaambia wajumbe aliwahi kuwaambia wanafunzi wamgrade wakampa F akawauliza niwafanye nini ili mnipandishe wakumueleza, akafanya marekebisho kama walivyomshauri, baada ya muda akaomba wamgrade tena wakampa B, akawauliza kwa nini hamjanipa A wakadai bado, akaomba wampe muda tena afanyie marekebisho dosari walizomwambia zipo. Walivyomgrade tena wakampa A. ameshauri wizara na serikali iwape nafasi wananchi waigrade.
 

Kyaiyembe

JF-Expert Member
Dec 1, 2011
1,693
2,000
Ha!kwamba aseme jina lake ili mjue dini yake na kabila lake?..Anaitwa HamadJoseph RafaelAhmed Mwandambalala
Kuna Hotuba moja ya Hayati J. K. Nyerere alisema "ukila nyama ya mtu huwezi kuacha" sasa na wewe naona huwezi kuacha Ubaguzi ndio unaowazia kwa kila kitu. Wewe ni mbaguzi = mla nyama za watu.
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,835
2,000
Karatu High School enzi za Dr Laurent Kibatala! Mkuu wa shule alafu ni PHD holder! Huyu mzee alikuwa mkorofi sijawahi ona!
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
Huyo lazima wata mkolimba!TATIZO ELIMU KWA SASA HAIJULIKANI IPO WIZARA GANI kuna waziri mkuu,tamisemi,elimu,utumishi,fedha
 

Onduru Ogy

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
1,136
2,000
Kwa serikali hi mtapata majibu si muda..... hamujiulizi kwanini kaombwa jina na huyo kenge? mtapata majibu wallah
Z


Wanamjua na misimamo yake toka kitambo.
Anaetaka kumjua zaidi amuulize Mulongo (RC) na REO wa Arusha.
 

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
892
195
Duh umenikumbusha mkuu wa zamani anaitwa KITEMANGU alinipiga kofi moja la usoni, nikapoteza network kwa dak 5
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom