Kafuta, sijui una maana gani unaposema 'tena kinaacha......' Zaidi ya hapo swali bado halijajitosheleza kwasababu maumivu ya kichwa yanategemea ni sehemu gani kwa namna gani, nyakati gani na vitu gani vinakuza au kupooza hali hiyo.
Hata hivyo napenda uelewe kuwa maumivu ya kichwa si ugonjwa bali ni dalili ya ugonjwa fulani. Ili kuweka sawa maelezo nina maana ya kuwa kitu kama homa si ugonjwa bali ni dalili ya tatizo flani (symptoms).
Maumivu ya kichwa yanategemea pia mambo mengi ili kupata picha halisi. Yanaweza kuwa ni kipanda uso (migraine), au shinikizo la damu (high blood pressure), yawezakutokana na macho (vision), maradhi kama tumour n.k sababu ni nyingi sana.
Ni hadi hapo utakapotupa maelezo kwa kina tunaweza kukushauri ufanye nini, kama ni ya muda mrefu ni vema ukapata ushauri wa vipimo hospitali