He! Kumbe Kikwete Alimtapeli Lowassa?

gambatoto

Senior Member
May 25, 2011
175
28
Nimeshtushwa na habari iliyo katika Mwanahalisi ya Leo Toleo namba 249 yenye Kichwa "Mzozo wa Lowassa na Pinda: Ni uamuzi Mgumu, Utapeli au ajali ya kisiasa?" Ukurasa wa 11. Nanukuu baadhi ya vifungu:-

"Baada ya kusomwa kwa ripoti , (Ya Richmond) taarifa zinasema Lowassa alikwenda Chamwino kuonana na bosi wake ili kupanga mkakati wa kuzima maasi ya wabunge wa CCM waliokuwa wamesisimka ili kummaliza Lowassa, rais Kikwete na serikali yao. Katika mazungumzo yao usiku ule, Rais Kikwete na swahiba wake huyo wa zamani-Edward Lowassa-walipima upepo na kuona pendekezo la Lowassa kuwa rais aende upesi kukutana na wabunge wa CCM ili kuwaonya wasiiangushe serikali yao, lilionekana halifai kwa hofu ya mihimili hiyo miwili kuingiliana. Ndipo mpango ukasukwa kuwa Lowassa aandike barua ya kujiuzuru, lakini rais AICHELEWESHE kuijibu na Bunge liahirishwe ili kumpa nafasi rais kuonana na wabunge wa CCM ili kuzima maasi ya wabunge kabla ya mkutano mwingine wa Bunge wa April haujafanyika."

"Mpango ukakubaliwa na bila ajizi Edward Lowassa aliamini na kuandika barua ya "KUIGIZA" kujiuzuru na kisha akaondoka kurudi Dodoma mjini usiku ule. Yaliyotokea Chamwino baada ya Lowassa kuondoka inabakia kuwa siri ya Kikwete mwenyewe na aliokutana nao."
 
asante kwa kutujuza, sijabahatika kulisoma hilo gazeti.
 
Mwanahalisi sasa watafute habari nyingine za Lowassa sasa ni kama marudio tu kila siku ripoti za Richmond na Lowassa.Wakuelewa wameelewa Lowassa ni nani na amelitendea Taifa unyama gani,
 
I used to respect Kubenea, he was my hero... but he has changed his colors.... I group his in the same group with "International criminal gang of bustards"
 
habari hii ya mwanahalisi nimeisoma imeandikwa na kondo tutindaga kwa kweli inasikitisha
na ni yakweli mkweli mtupu na tanzania imepata wasaniii tusubiri tutajua mengi mpaka kufika
2004 kazi kweli kweli
 
Kwani hii 2000 na ngapi????.........labda mie nipo mars
habari hii ya mwanahalisi nimeisoma imeandikwa na kondo tutindaga kwa kweli inasikitisha na ni yakweli mkweli mtupu na tanzania imepata wasaniii tusubiri tutajua mengi mpaka kufika2004 kazi kweli kweli
 
Hizi ni habari za kufikirika. Kwanza isingetarajiwa Rais amuunge mkono mtu aliyejiuzulu kutokana na maovu yake mwenyewe. Hayo ni maneno ya wapambe wa Lowassa ambao bado wanashikilia kwamba bwana huyu hakuwa na kosa na kwamba kajiuzulu kuikoa serikali. Bullshit!
 
He, he, hee, halafu anasikika akimwambia Zitto kuwa sasa ni zamu ya vijana kuwa marais. Mswahili kishamtosha Mmasai. He, he, hee!
 
ukiangalia kwa 3D,unaona wazi kwamba lowassa alikuwa "kondoo wa kafara"...!

na hakika aliiokoa serikali!...
 
He, he, hee, halafu anasikika akimwambia Zitto kuwa sasa ni zamu ya vijana kuwa marais. Mswahili kishamtosha Mmasai. He, he, hee!
<br><br>

Mmasai kajimaliza mwenyewe na sasa gari iko kwenye gia namba 5 akipiga reverse tu ameua injini.
 
EL kama anataka tuamini kama alionewa basi ajitokeze hadharani amwage mboga ili ijulikane kama yeye ni kondoo wa kafara tu.

Lakini kitu cha msingi hapa ni kwamba marumbano ya EL na JK hayataibakiza ccm vyovyote itakvyokuwa ccm itakufa tu na wala EL asijidanganye kwamba kwa kusemaukweli wa mambo atapona na kustahili hata kugombea urais. Anaweza akawa mgombea tu lakini siyo Raisi wa Tanzania hii.

Vyovyote atakavyofanya haitasaidia maana alishiriki katika hilo deal na hakuna namna ya kutufanya tuamini kuwa hakuwa na dhamira ya kutuibia. So long as alikubali kushiriki huo wizi basi wote ni wezi pamoja na bosi wake period
 
Ni kweli kabisa. Wakati Lowasa akisimama mbele ya Bunge na kusema katuma barua ya kujiuzulu wala hiyo barua alikua hajaiandika rasmi. Alicho fanya JK ni "kuaccept" "barua" hiyo na baada ya hapo EL akawa hana chakufanya. Legally EL should still be prime minister kwa maana hakuna ushahidi hiyo barua ilishawahi kutumwa rasmi.
 
Mambo ni mengi sana! Kila siku Mwanahalisi na mambo ya Lowassa Lowassa ina maana magamba wengine wa chama hawapo? Hii ni 2000 na ngapi? Maana mi naona karibu 2nasomaga mambo ya EL kwenye Mwanahalisi sana. KUBENEA,hebu fanya seach kwa magamba wengine maana lazima kuna wengi walishirikiana nao kwa namna moja ama nyingine. Aluta Continue!
 
Back
Top Bottom