Hayati Rais Magufuli aliunda bodi ya mishahara, iliishia wapi? Leo tena Rais Samia anaunda bodi ya mishahara

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Miaka ya 2016 hayati Rais Magufuli aliunda bodi ya mishahara lakini hakuna matokeo chanya yaliyoonekana.

Leo tena Rais Samia amesema iundwe bodi ya mishahara, hivi watumishi hamuoni hii ni danadana na danganya toto?

Hivi kama HESLB wanaweka value retention fee ya 6% (imeondolewa), serikali haioni kuwa thamani ya pesa ya 2013 si sawa na ya 2021?
 
Miaka ya 2016 hayati Rais Magufuli aliunda bodi ya mishahara lakini hakuna matokeo chanya yaliyoonekana...
Kama uchumi ulikuwa kwa kasi ile retention fee ilikuwa ya nini,au ndiyo iliyokuza uchumi.
 
Magufuli alikuwa Rais muongo kuwahi kutokea katika historia ya Tanzania.
 
We are all trapped in vicious cycle 0f poverty.. kwahiyo tupo kwenye tragedy 9f the commons
 
Nililelewa sana lile andiko la Mchungaji Peter Msigwa la kumuelezea Magufuli kama Rais bora sana aliyetakiwa kuishi karne nyingi zilizopita, badala ya karne hii ya 21!

Hakika alikuwa ni kiumbe mwenye fikra za kizamani sana.
 
Kama umesikia iundwe, ujue haikuwepo. Tulikuwa tunapigwa porojo tu!
Bodi za Mishahara na Maslahi ktk utumishi wa umma zilikuwepo kuanzia kipindi cha Kikwete hadi Cha Magufuli 2020 zilimaliza muda wake na kuvunjwa na majukumu yake kuhamishiwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili kupunguza gharama na ili kwenda na maelekezo ya kuuhisha miundo ya serikali. Inawezekana Ndiyo maana Rais anaelekeza hivyo zianzishwe tena ili kumshauri ipasavyo kwa weledi, umakini na bila kuegemea upande wowote kuhusu masuala ya mishahara na maslahi ya watumishi. Ushauri:Waziri Mohamed Mchengerwa afuatilie kwa karibu utekelezaji wa maelekezo haya.
 
Back
Top Bottom