Hayati Magufuli aliwezaje kutunyamazisha Watanzania milioni 60?

Kwamba kwa sasa wao ndio wangekuwa madereva wa magari
Ndio hivyo ,wale madereva wa kwenye msafara wa kagame,mobutu,magu,sadam hawasemwi vibaya ila kazi wanayofanya ni ileile tu
 
Makosa makubwa yalifanyika 2015 .

Itachukua muda walau miaka 10+ nchi irudi vile ilikua.
 
Ridhiwani Kikwete aliwahi kuhojiwa na Millard Ayo kuhusu mzee wake JK alipokuwa madarakani na alikuwa anatukanwa na kuchorwa vibaya yeye alikuwa anaichukuliaje??

Riz alisema ukweli ni kwamba ilikuwa inamkera sana kiasi ya kwamba alienda kumhoji mzee wake kwa nini anawaacha watu wanamkejeli na kumdhalilisha namna Ile na kwa nini hawashughulikii?

Mzee Kikwete alimwambia kwamba laiti angejua madaraka na nguvu aliyonayo Rais na akiamua kuyatumia basi hakuna atakayekuwa salama hata kidogo. Alimaanisha kwamba ana nguvu kubwa sana yeye kama Rais Ila wacha tu watu wamdhihaki sababu mtu anayeweza kumshika sharubu Simba hakika hajui Simba anaweza kumfanya kitu gani ndani ya sekunde moja tu.

Sasa Magufuli alikuwa ana ambition kubwa ya kuongoza nchi kwa kupeleka mambo haraka na the way anavyotaka, alipokuja kugundua hayo madaraka na nguvu aliyonayo akatamani kuzitumia na akaona namna watu wanavyotetemeka akipita sehemu akatamani atumie hizo nguvu kupeleka Mambo yaende.

Akazima bunge, Mahakama, waandishi au vyombo vya habari, akafumua mfumo wa utumishi wa umma, Yani akavuruga kila anachotaka hii sasa ilitokana na kujua kwamba Rais anaweza kufanya chochote.

Kwa nguvu hiyohiyo akageuka kuabudiwa sababu walitaka wale pesa yake waligundua ili waweze kula lazima wamsifie na kumhonga cheo Cha Mungu, wengine Kama sheikh Alhad wa Dar alisema Magufuli ni zaidi ya Yesu na jamaa likawa linaenjoy sana vile vyeo.

Mwishowe akalewa ule ukuu akataka atukuzwe maana walishamzoesha kumtukuza Hadi makanisani, viongozi wa dini karibu wote walimtukuza na aliyejaribu kumkosoa aliipata kisawasawa. Na pale ndipo kila aliyemkosoa alikuwa anapotezwa maana aliona yeye hawezi kukosolewa na hakutaka kukosolewa maana alishalewa ushamba wa madaraka.

Utaona kile kikosi kilichoundwa na Makonda kikiwa na jukumu la kutesa na kuua wote waliompinga na kumkosoa Magufuli kilianzishwa kwa usiri sana na kutekelezwa ushenzi mkubwa mno.

Kwa namna Ile hakuna ambaye angeweza kujitetea mbele yake ndio maana hakuwa anasikiliza hoja ya mtu yeyote akija anataka yeye aongee na mtekeleze whether you like it or not.

Hii ndio ilipelekea Hadi akataka aongoze milele lakini Mungu wa Watanzania ni Mungu wa Kweli, mnamo tarehe 17/3/2021 historia ikaanza kuandikwa upya baada ya kumpatia kifo yule fedhuli.

Sasa ukiangalia history ya madikteta wote Kama Hitler, Stalin, Pinnochet akina Mobutu, Idd Amin, Bokasa nk walikuwa na style ya kutengeneza watu wanaowapraise na wale waliowapraise waliishi vizuri sana .

Hiyo ilikuwa lazima wawepo ili waweze kusurvive kiunafiki sababu Hawa madikteta walijua kabisa hawakubaliki na hawapendwi nje na ndani ya nchi zao. Na ndio maana wanafanana kila kitu mfano, hawakusafiri nje ya nchi zao hovyo, hawakuruhusu mtu aripoti mambo ya nchini kwao na waliruhusu ripoti zinazowasifia na kuonyesha mambo ni shwari sana, nk.

Magufuli was one hell of the dictator ukifuatilia tabia za madikteta.

It’s better to live on a house top than to live in a house full of confusion…

JPM alifanya house cleaning ni characters za baba mzuri wazungu wanauita udikteta…na nyie wasomi mmeucopy mnajiona mnaakili kumbe mmekremishwa upumbavu…

Baba mzuri akikuta nyumba ina panya wengi watoto wamekonda wanaishi duni sababu ya uharibifu wa panya huwa anafanya lile aliwezalo kuwa eliminate panya ili japo watoto waelewe jinsi nyumba yao ilivyo nzuri na ilivyojaa neema tele…

Sasa ukiona mtu analialia baba huyu ni dikteta ujue alikuwa ni panya either kwa kujua au kutokujua…

Rest in peace JPM wachache tulikuelewa…na watoto waliokuwa wengi maskini walifaidika na wamefahamu kwamba hakika nyumba ina neema tele ila ni panya wanaofanya uharibifu…na tumewashuhudia punde ulipolala hawakusubiri hata tupoe majonzi yakukupoteza wametuvamia tena na tabu zimerudi palepale…
 
Inahitaji busara sana ndugu... vinginevyo Rais akiwa mshenzi hata huyo JPM atakuwa na nafuu kwa jinsi katiba ilivyompa mwanya wa kufanya lolote atakalo. Na kibaya hashtakiwi kwa makosa yake wakati akiwa kiongozi
Wala hakuna ajabu kama atatokea mwingine miaka ijayo na akafanya kuliko hayo yaliyofanywa na aliyepita !! Rohoni kwa MTU ni mbali !!!
 
Watanzania hawakuzoea uongo WA Aina Ile, yule mtu alijigeuza police, mahakama, Bunge, mhubiro nk,. Kwa kifupi vyeo vyote alijipachika yeye.
Lakini Kwa sababu Mungu aliyaona mateso ya watu wake, akaamua kumchukua aliye mwovu ili watanzania wapate Amani kwenye mioyo Yao.
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin mobutu ,kagame,bokassa na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe
Alitumia vizuri udhaifu wa katiba,
 
Watanzania hawakuzoea uongo WA Aina Ile, yule mtu alijigeuza police, mahakama, Bunge, mhubiro nk,. Kwa kifupi vyeo vyote alijipachika yeye.
Lakini Kwa sababu Mungu aliyaona mateso ya watu wake, akaamua kumchukua aliye mwovu ili watanzania wapate Amani kwenye mioyo Yao.
Ameen
 
Yule mwamba noma japo na mimi niliufyata
Sisi kimsingi tulifyatishwa na washika mitutu.
Raia hawajawahi kubaki salama palewashika mitutu wanapotii kila asemalo mfalme.
Nguvu za mfalme zi wapi ikiwa washika mtutu watataka iliyo haki.
 
Kuna idadi kubwa ya watu miongoni mwetu wanaopenda utumwa (subservience) mbele ya mtu mbabe na katili wakiamini ndio fursa ya kujipatia upendeleo, ulaji na kushindana usnitch ili kukubalika zaidi na mtemi huyo. Watamnyenyekea na kumtukuza kwa majina kama mwamba, jiwe, chuma - bila aibu. Wakifokewa na kutukanwa hadharani na mtu wa aina hiyo wanaona sawa. Ndio asili ya wengi wetu hasa waliojaa kwenye chama tawala. Wachache wasiokubaliana na hali hiyo watapata tabu sana kupambana na hilo jeshi la misukule.

Historia ya utumwa na ukoloni Afrika inafichua kuwa waafrika weusi ndio walikuwa watu rahisi sana kukamatwa na kuuzwa utumwani na pia kufanywa makoloni, kwa vile kwa kiasi kikubwa, mbele ya wavamizi walikuwa na hulka ya "kusarenda" kirahisi na kushindana kujipendekeza kama njia ya kuepuka maafa na kujipatia upendeleo. Hata watawala wao wa jadi wengi walikuwa wakinunuliwa kirahisi ili wawauze watu wao utumwani. Hii nimeisikia mara nyingi kwa washirika wangu hasa wa Afrika magharibi na kaskazini kwa waarabu. Ingawa siioni mantiki yake lakini inafikirisha sana na haifuraishi.

Tofauti, waarabu na watu waliochanganya damu kama wasomali na wahabeshi hadi leo ni wapambanaji hadi kifo linapokuja suala la uhuru na haki zao. Walikuwa wakisumbua sana huko zamani. Haikuwa rahisi kuwafanya watumwa wala kuwatawala kirahisi kama koloni. Ndio maana kwenye nchi hizo, hadi leo hakuna kulala. Huku kwetu tunaambiwa "amani" ndio kila kitu. Eti bila amani, haki haiwezi kupatikana! Kubisha ni kujitakia tabu ya bure. No overt support from fellow citizens. Lissu tangu mwishoni mwa miaka ya 1990 ameteseka sana kupigania haki za wanyonge kwenye migodi na bungeni anaishia kushambuliwa kwa kauli za kizuzu za "kuunga mkono ushoga"!
Wafuasi na macombi ya watawala hawawezi kukuelewa. Na hii ndiyo maana mpaka leo hii, wa Tanganyika hawawezi kuhoji juu ya muungano feki waliotumbukizwa. KISA KUJIKOMBA kwa so called watawala.
 
Inahitaji busara sana ndugu... vinginevyo Rais akiwa mshenzi hata huyo JPM atakuwa na nafuu kwa jinsi katiba ilivyompa mwanya wa kufanya lolote atakalo. Na kibaya hashtakiwi kwa makosa yake wakati akiwa kiongozi
Na hata akistaafu hashtakiwi .
 
Tangu nikiwa mdogo nilipenda kufuatilia visa vya viongozi waliotawala kwa mkono wa chuma kama vile Stalin, Mussolini, Lenin, Hitler, Suharto Iddi Amin mobutu ,kagame,bokassa na wengineo.

Nikawa najiuliza hawa wababe waliwezaje kuwanyamazisha wananchi wao kirahisi wasipate watu wa kuwapinga?

Hata nikadhani labda wananchi wao ni mazezeta.

Ila alichotufanya bwana yule nilikuja kuelewa somo kwa vitendo,nilipenda sana story za hawa wababe ila ghafla nilijikuta nabadili mtazamo wangu.

Kiukweli kabisa watanzania wote tuliufyata kasoro mtu mmoja tu Tundu Lissu nadhani kwa sababu alishaonja kuzimu labda akaona kumbe hakutishi kivile, tuliobaki tukubali tuliufyata mpaka wengine kufikia kumuita Mungu, nikikumbuka nacheka mwenyewe
Waulize North Korea watakwambia kwann hawalalamiki na wanafurahia maisha na wako bega kwa bega na Mr. Kiduku
 
Back
Top Bottom