Hayati Dkt. Magufuli hakuisaidia Chato

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania.

Lakini maendeleo ni nini?

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alijitanabaisha kama mtu anayependa maendeleo, lakini kuna uwezekano mkubwa hakujua tafsiri ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine, Magufuli alitamani maendeleo ya nyumbani kwao Chato, na hivyo alifanya mengi huko nyumbani kwao, lakini pengine hakupasaidia inavyotakikana.

Magufuli alijenga uwanja wa ndege wa kutua ndege kubwa wilayani Chato, wakati kuna majiji (mfano Tanga), manispaa na miji mikubwa kuliko Chato ambako hakuna viwanja vya ndege vya maana au vilivyopo havina hadhi ya maeneo hayo. Kwanini Chato?

Hoteli ya Nyota Tano ilikwisha anza kujengwa Chato. Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa ulikuwa kwenye mpango wa kujengwa Chato. Alilazimisha CRDB wapeleke huduma wilayani Chato ingawa hakuna tija ya kibiashara. Na Jengo walilopangisha CRDB huko Chato ni jengo lake huyo Magufuli.

Je! Magufuli aliipenda Chato? Jibu ni Ndiyo. Na sio kosa kupenda kwenu, sio kosa kupenda maendeleo ya kwenu. Shida inakuja kwenye tafsiri ya maendeleo.

Magufuli angetambua maana ya maendeleo; Angeanza kuboresha elimu wilayani Chato kabla ya kujenga Hotel ya Nyota Tano. Moja kati ya wilaya zenye mazingira magumu kwa wanafunzi na walimu ni Wilaya ya Chato. Hoteli ya Nyota tano ya nini wakati wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika? Nani ataijenga Chato wakati idadi kubwa ya vijana hawapati elimu yenye tija katika dunia ya leo (Na hili ni kwa maeneo mengi ya Tanzania).

Kanda ya Ziwa kuna Ng'ombe wengi sana, lakini hawana afya. Pesa ya kujenga uwanja wa ndege ingetosha kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna ya kufuga kwa faida pamoja na kujenga viwanda vidogodogo vya kusindika Nyama na Maziwa ambavyo vingetoa ajira ya kudumu kwa vijana wa Chato. Wafanyabiashara wangemiminika Chato kutoka maeneo ya jirani kwa ajili ya biashara ya Nyama, na mazao ya maziwa. Kwanini mwenyeji wa Geita anunue maziwa ya Tanga Fresh, au Asas kutoka Iringa wakati kuna Ng'ombe wengi ndani ya kanda ya ziwa kuliko Iringa na Tanga kwa pamoja?

Kuna ardhi kubwa wilayani Chato. Magufuli angeweza kupeleka wataalamu wa kilimo kutoa mafunzo kwa vijana juu ya kilimo chenye tija ya kiuchumi na kibiashara. Wakulima wangelima kibiashara zaidi na kuvutia masoko kutoka mikoa jirani na nchi jirani. Watu wangemiminika Chato na kuchangamsha shughuli za maendeleo.

Kuna Ziwa Viktoria. Angeweza kuwekeza kwenye kilimo cha samaki (kuzalisha samaki ndani ya vitalu vya Ziwani) ambacho kingewanufaisha watanzania wanaoishi Chato. Ajira zingepatikana, wafanyabiashara kutoka mikoa jirani na hata nchi jirani za Rwanda, Burundi na DRC wangefika Chato kufungasha mizigo.

Angeweza kujenga Chuo Kikuu au hata matawi mawili matatu ya vyuo vikuu. Mji wa Iringa ni miongoni mwa miji iliyochangamshwa na uwepo vyuo vikuu. Chato ingechangamka pia.

Hayo yote yangewezekana kirahisi kutokana na nguvu aliyokuwa nayo kama Rais. Lakini nguvu ili iwe na tija sharti iambatane na akili.
Halafu yangefuata hayo ya kujenga uwanja wa ndege na mahoteli kwa kuwa sasa watu wenye uwezo wa kuvitumia (labda) wangekuwapo.

Lakini hawapo. Na sasa shirika la Ndege limesitisha safari za ndege Chato kwa sababu aliyekuwa anautumia uwanja wa ndege wa Chato hayupo. Nyasi zina tabia ya kuota hata juu ya zege. Baada ya muda kidogo ile hoteli ya nyota tano ambayo haijamalizika itabaki gofu. Uwanja wa mpira wa kisasa hautajengwa. Benki ya CRDB itaondoka kwa sababu wakazi wa Chato wanaoweka pesa benki ni walimu na watumishi wengine wa serikali - ambao wanatumia NMB. Majengo mazuri ya mahakama na vituo vya polisi hayawezi kuchochea maendeleo.

Kuna suala la Hospitali kubwa ya kanda iliyojengwa Chato. Huduma za afya ni suala zuri lakini jengo pekee halitoshi. Huduma zitakapoanza zitapaswa kufanana na jengo lenyewe. Hata hivyo haikuwa lazima kujenga hospitali kubwa Chato kabla ya kuboresha huduma za zahanati (Primary Health Care) vijijini. Hakuna maana ya kujenga hospitali kubwa eneo moja wakati zahanati katika vijiji mia au zaidi hazina ubora. Huduma za zahanati nyingi zikiwa bora, faida yake ni kubwa zaidi kuliko huduma ya hospitali kubwa moja. Kwahiyo, pamoja na hatua nzuri ya kujenga hospitali ile, naamini haikupaswa kuwa jambo la kwanza.

Magufuli hakuisaidia Chato kwasababu aliamini zaidi katika vitu (hardware) badala ya watu (Software). Angeanza kuwajenga watu kwa elimu na maarifa halafu akawajengea nyenzo za kuboresha elimu na maarifa yao; shule, vyuo, viwanda kwa ajili ya ajira, na mbinu zingine za kuvutia uwekezaji.

Lakini wapi! Aliwaza matokeo badala ya mchakato. Alichojenga Chato kitabaki kuwa makazi ya popo na mijusi kwa sababu hakuna wa kukitumia.

172785163_4150745731657299_2314085963338368612_n.jpg


Nawasilisha!

Dr Cyrilo
 
Kulikuwa kuna haja hivyo vyote kuwepo kwa level ya Raisi maendeleo makubwa ndiyo yaliyotakiwa Kama unavyotamani yangefika na mikoa uliyotaja, hizo issue za elimu muulizeni waziri mkuu ndo ziko chini yake na bajeti yake ndo anaomba kila waziri mkuu anatakiwa kuonyesha tija yake kwenye elimu Kama Lowasa alivyoleta shule za Kata na mawaziri wakuu wengine hatukuona walichofanya, waziri mkuu anatakiwa azungukie nchi nzima kukagua miundo mbinu ya shule maana ndo kumebeba future ya Taifa la kesho akishindwa hapo na yeye atakuwa ameshindwa Kama wengine na legacy hiyo itabaki kwa Lowasa.

Kufungua miradi irudi kwa mawaziri na makamu wa Raisi na Raisi abaki kutatua mahitaji ya mifumo kujiendesha na kutafuta pesa za kuendesha nchi na kuwezesha miradi mikubwa na matumizi yake yalivyotumika.
 
Hayo unayosema ni kweli. Hakukuwa na haja ya kubadili kijiji kuwa mji. Alichotakiwa ni kuwainua watu wake ili waweze kuongeza productivity.

Kufanya Chato kuwa mji ni kuleta wageni ambao ndiyo watakuwa wafaidikaji zaidi ya wenyeji ambao hawana kitu hivyo kuwafanya wawe servants kwenye ardhi yao.
 
Muda si mrefu Chato itasahaulika kama mwenye Chato yake.

Hakuna Wilaya iliyopata umaarufu kwa ghafla kama Chato. Wengi hawajui wilaya walizotoka Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya wala Samia.

Bwana yule alikuwa mbinafsi, mbaguzi , dhalimu na fashisti sana.

Ahsante Mungu kwa matendo yako makuu. Sisi ni nani tusiushukuru uamuzi wako na mapenzi yako kwetu?
 
Magufuli hakuisaidia Chato kwasababu aliamini zaidi katika vitu (hardware) badala ya watu (Software). Angeanza kuwajenga watu kwa elimu na maarifa halafu akawajengea nyenzo za kuboresha elimu na maarifa yao; shule, vyuo, viwanda kwa ajili ya ajira, na mbinu zingine za kuvutia
Yote haya tulishayaweka humu JF mara kadhaa toka zamani, mkuu, Dr Cyrillo.

Labda iwe ni kukumbushana tu.

Hivi karibuni tu kwenye msiba wake tuligusia swala la mafuta ya kula, ambalo ni uhaba mkubwa sana hapa nchini. Tukauliza, sijui ingekuwaje, kama angekumbuka kuwawezesha wananchi wa wilaya ya Chato wakalima alizeti wakitumia njia zote za uzalishaji wenye tija. Soko la mafuta hayo,na mashudu yake lisingetosheleza soko la eneo lote la Kanda ya Ziwa, Brundi, Rwanda, DRC, na kwingine kote.

Sijui maisha ya wananchi hao yangekuwaje katika muda mfupi sana wa mradi kama huo!

Na siyo hivyo tu, iwe kilimo, ufugaji na shughuli nyingine yoyote ambayo wananchi hao wangefaidika nayo, isingeishia tu hapo Chato pekee, maanake wilaya ya Chato ingegeuzwa na kuwa darasa muhimu kwa wilaya na mikoa jirani.

Mashamba ya kilimo bora ya alizeti kwa mfano, yangetumika kuwafundisha wananchi wa Singida na Dodoma namna nzuri zaidi ya kuzalisha alizeti; pamoja na mnyororo mzima unaoambatana na zao hilo.

Marehemu Magufuli alikuwa na tabia za kilimbukeni. Zile taa za barabarani ambako usafiri mkuu ulikuwa ni wa punda ziliwasilisha kungali mapema sana mfano mzuri wa tabia hiyo.
 
Mliofika Chato tuhabarisheni zaidi;nilikuwa nasikia (kuanzia miaka ya mwishoni wa 1990s) kwamba Chato ni sehemu iliyoendelea kuliko hats Biharamulo penyewe (ambapo ndio palikuwa makao makuu ya Wilaya ya Biharamulo). Na kwamba Chato palikuwa panayazidi maeneo mengi tu nchini kwa maendeleo.

Leo wengi wanaopaongelea Chato wanaonyesha kwamba ni sehemu moja primitive sana iliyokuja kupendelewa awamu ya 5. Mliofika huko tujulisheni,halo halisi ikoje huko mkilinganisha na wilaya nyingine?
 
Mliofika Chato tuhabarisheni zaidi;nilikuwa nasikia (kuanzia miaka ya mwishoni wa 1990s) kwamba Chato ni sehemu iliyoendelea kuliko hats Biharamulo penyewe (ambapo ndio palikuwa makao makuu ya Wilaya ya Biharamulo). Na kwamba Chato palikuwa panayazidi maeneo mengi tu nchini kwa maendeleo.

Leo wengi wanaopaongelea Chato wanaonyesha kwamba ni sehemu moja primitive sana iliyokuja kupendelewa awamu ya 5. Mliofika huko tujulisheni,halo halisi ikoje huko mkilinganisha na wilaya nyingine?
Watu wake ni primitive hata ufanyaje hawaendelei.
 
Je! Magufuli aliipenda Chato? Jibu ni Ndiyo. Na sio kosa kupenda kwenu, sio kosa kupenda maendeleo ya kwenu. Shida inakuja kwenye tafsiri ya maendeleo.
Unajiita doctor ila unaandika vitu kama mtoto mdogo alievaa pampas ambae hajui la kufanya!Unasema Magufuli kupenda kwao siyo kosa,unaelewa kuwa Magufuli alikuwa ni Rais wa nchi na wala siyo mwananchi wa kawaida?

Unaelewa kuwa Rais wa nchi anatakiwa kupeleka miundombinu mahali kutokana na economic viability pamoja na economic strategic ya eneo husika na wala siyo kupeleka miundombinu eneo fulani kisa ni nyumbani kwao?

Unaelewa kuwa Rais kupeleka miundombinu eneo fulani kwa sababu tu ni nyumbani kwake hata kama hilo eneo siyo strategic economic area itachochea ukabila na ukanda?Kama kila rais atakomaa kupeleka miundombinu kwake,maeneo mengine ya Tanzania yatapewa maendeleo na nani?

Kama Rais atapeleka maendeleo eneo fulani kisa tu ni nyumbani kwake kama unavyodai,je yale maeneo ya kiuchumi ambayo huchangia pato la Taifa yatakuzwa na nani?Wewe ni doctor wa wapi unajenga hoja kama mtoto mdogo wa chekechea?
 
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania...
Mwanza Airport ni kubwa amabayo inaweza kuhudumia mikoa hata mitatu bila shida .
 
Mliofika Chato tuhabarisheni zaidi;nilikuwa nasikia (kuanzia miaka ya mwishoni wa 1990s) kwamba Chato ni sehemu iliyoendelea kuliko hats Biharamulo penyewe (ambapo ndio palikuwa makao makuu ya Wilaya ya Biharamulo). Na kwamba Chato palikuwa panayazidi maeneo mengi tu nchini kwa maendeleo..
Mkuu ukiamini yanayosemwa na nyumbu wa Ufipa, utaamini kweli Mbowe ni "mwekezaji" Dubai na Chadema ni chama kikuu cha upinzani wakati hakina mwenyekiti wa mtaa, wala diwani wala mbunge nchi nzima!!
 
Ninadhani tatizo kubwa la kilimo Tanzania licha ya ujuzi wa kilimo cha kisasa ni masoko. Awamu ya kwanza vyama vya ushirika vilisimamia masoko, mfano Tanzania Coffee Curing ya Kilimanjaro kilikua chama cha ushirika chenye nguvu na kiliweza kusafirisha kahawa mpaka Ulaya.

Vyama vya ushirika vinatakiwa kuwa na watalaamu wa purchasing, marketing, logistics na public relations. Kukiwa na vyama vya ushirika chenye faida hata mazao mfano wa jamii ya maharage yanaweza kuleta faida kwa mkulima wa kawaida.

Haya ndiyo yanayohitajika sehemu kama Chato.
 
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania...
Nina uhakika hii ni moja ya mada bora kabisa ambayo haiko biased. Analysis imekwenda shule. Yeyote kutoka Serikali anaweza kuitumia kama rejea juu ya hatma ya uwekezaji wa kijinga ambao Mwendazake amefanya Chato. Hongera
 
Back
Top Bottom