Haya yalisababisha nikaichukia CCM lakini upinzani umeniangusha

FURY BORN

JF-Expert Member
Jul 11, 2020
638
1,145
Nakumbuka nilianza kupiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1990, nikiri pia mwaka huo nilikuwa sijafikisha umri halisi wa kupiga kura lakini mwalimu mkuu wa shule niliyokuwa nikisoma alituandikisha wanafunzi wote tuliokuwa darasa la saba ili tupige kura kumsaidia aliyekuwa mgombea ubunge wilaya ya Musoma vijijini Dr Charles Magoti Chinuno (marehemu kwa sasa) aliyekuwa akichuana na Herman Kirigini

Nakumbuka Charles Maghoti akiwa na alama ya nyumba na Herman Kyanzi Daniel Kirigini akiwa na alama ya Jembe. Baada ya uchaguzi Dr Charles alishinda ubunge wa wilaya ya Musoma vijijini.

Tangu kipindi hicho nimekuwa nikishiriki chaguzi zote na sikuwahi kuipigia CCM kura au mgombea yeyote wa CCM. Nilichukia CCM baada kuanzisha shule zake kila tarafa ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jumuiya ya wazazi. Nikiwa miongoni wa wanafunzi wengi waliotupwa kwenye hizo shule ambazo hazikuwa na walimu wala miundo mbinu ya kutosha kutoa elimu bora. Mfano shule niliyosoma kwa miaka yote minne hatukuwahi kuwa na mwalimu wa hesabu na physics isipokuwa mara moja tulikuwa tukipata vijana wa JKT waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wakitumikia jeshi kwa mjibu wa sheria.

Nilichukia CCM kwa sababu ilisababisha mzazi wangu kuona ni nafuu kulipa ada ya shilingi elfu mbili mia tano(2500) ambayo ilipanda na kufikia shilingi elfu tano, kuliko kulipa shilingi elfu 16 shule binafsi. Kwa wale vijana wa leo mnaweza kushangaa kusikia ada ya shilingi elfu mbili, ila huo ndo ukweli na ada ilikuwa hiyo.

Nikiri kuwa sikuwa au sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote mpaka dakika hii ninapoandika bandiko hili japo nilikuwa muumini mzuri wa upinzani kutokana na chuki zangu kwa CCM.

Niliamini upinzani unaweza kuleta mabadiliko ya kweli ktk taifa letu, nikiri pia kwamba kwa namna moja au nyingine upinzani ulifanya kazi yake vizuri nje ya boksi, lakini ndani ya boksi wapinzani wamekuwa na malengo yao binafsi. Mifano iko mingi hasa kwa wale tuliowamini tukawapigia kura baada ya kupata majina wakaunga mkono juhudi hasa pale walipoahidiwa donge nono. Hii kidogo imenistua na kugundua kwamba kumbe hakuna mwana siasa aliyesimama na mimi, bali kila mtu yupo kwa ajili ya maslahi binafsi.

Rasmi kuanzia mwaka huu nimetangaza kuwa kwenye uwanja huru (neutral ground) siyo upinzani wala chama tawala. Nitasubiri atakayetoka CHUMBANI na taulo huyo ndio baba. Natambua kuna hoja itaibuka ya haki yangu kama mpiga kura, hiyo nayo ni mojawapo ya haki nilizoridhia kuzipoteza kiroho safi.

Wapinzani mmeniangusha kwa kuunga mkono juhudi. Kuanzia leo natangaza sitopiga kura tena mpaka naenda kaburini kiongozi bora wa maisha yangu na familia yangu nitaendelea kubaki mimi mwenyewe. Nitaheshimu na kutii sheria na kulipa kodi kwa kadiri itakavyobidi. Niwatakie uchaguzi mwema mimi tayari ni miongoni mwa wale ambao hawatopiga KURA.

Hivyo nami niungane nanyi kuunga mkono juhudi.

Asanteni
 
Huwezi kuhukumu watu wote kwa ujinga wa watu wachache, mbona husemi wapinzani ambao wamefungwa kwa ajili ya misimamo yao?
 
Sasa kura yako moja ndo ingesaidia nini? Pia Mbowe kaijenga sana Chadema hivyo mm binafsi ntapiga kura kivyovyote panapo uzima.
 
Umenikumbusha ada ya 2500 tulikuwa tunalipa mhasibu wa shule anazipiga. anaandika majina kwenye register , siku unaenda kuchukua cheti unakutana na deni lako
 
Duh nimeikumbuka ada ya elfu 4 kabla ya kupanda mpaka elfu 8 na mpaka namaliza O'level ilikuwa elfu 40
 
1990 ni uchaguzi gani huo wakati hata vyama vingi havijaanzishwa mwaka huo
Uchaguzi haukuanza baada ya vyama vingi yawezekana hata elimu tu ndogo na historia ya darasa nne hauna, sasa nakusaidiaje. Kwa taarifa yako uchaguzi ulikuwepo hata kabla ya vyama vingi wabunge wa CCM walikuwa wanachaguliwa kama kawaida, isipokuwa kwa kura ya Rais alikuwa anapambana na kivuli. Ndio maana kama umesoma maelezo yangu Charles alipambanishwa na Kirigini mpaka hapo hujaona kama kulikuwa na uchaguzi?
 
Nakumbuka nilianza kupiga kura kwa mara ya kwanza mwaka 1990, nikiri pia mwaka huo nilikuwa sijafikisha umri halisi wa kupiga kura lakini mwalimu mkuu wa shule niliyokuwa nikisoma alituandikisha wanafunzi wote tuliokuwa darasa la saba ili tupige kura kumsaidia aliyekuwa mgombea ubunge wilaya ya Musoma vijijini Dr Charles Magoti Chinuno (marehemu kwa sasa) aliyekuwa akichuana na Herman Kirigini

Nakumbuka Charles Maghoti akiwa na alama ya nyumba na Herman Kyanzi Daniel Kirigini akiwa na alama ya Jembe. Baada ya uchaguzi Dr Charles alishinda ubunge wa wilaya ya Musoma vijijini.

Tangu kipindi hicho nimekuwa nikishiriki chaguzi zote na sikuwahi kuipigia CCM kura au mgombea yeyote wa CCM. Nilichukia CCM baada kuanzisha shule zake kila tarafa ambazo zilikuwa zinamilikiwa na jumuiya ya wazazi. Nikiwa miongoni wa wanafunzi wengi waliotupwa kwenye hizo shule ambazo hazikuwa na walimu wala miundo mbinu ya kutosha kutoa elimu bora. Mfano shule niliyosoma kwa miaka yote minne hatukuwahi kuwa na mwalimu wa hesabu na physics isipokuwa mara moja tulikuwa tukipata vijana wa JKT waliokuwa wamemaliza kidato cha sita wakitumikia jeshi kwa mjibu wa sheria.

Nilichukia CCM kwa sababu ilisababisha mzazi wangu kuona ni nafuu kulipa ada ya shilingi elfu mbili mia tano(2500) ambayo ilipanda na kufikia shilingi elfu tano, kuliko kulipa shilingi elfu 16 shule binafsi. Kwa wale vijana wa leo mnaweza kushangaa kusikia ada ya shilingi elfu mbili, ila huo ndo ukweli na ada ilikuwa hiyo.

Nikiri kuwa sikuwa au sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote mpaka dakika hii ninapoandika bandiko hili japo nilikuwa muumini mzuri wa upinzani kutokana na chuki zangu kwa CCM.

Niliamini upinzani unaweza kuleta mabadiliko ya kweli ktk taifa letu, nikiri pia kwamba kwa namna moja au nyingine upinzani ulifanya kazi yake vizuri nje ya boksi, lakini ndani ya boksi wapinzani wamekuwa na malengo yao binafsi. Mifano iko mingi hasa kwa wale tuliowamini tukawapigia kura baada ya kupata majina wakaunga mkono juhudi hasa pale walipoahidiwa donge nono. Hii kidogo imenistua na kugundua kwamba kumbe hakuna mwana siasa aliyesimama na mimi, bali kila mtu yupo kwa ajili ya maslahi binafsi.

Rasmi kuanzia mwaka huu nimetangaza kuwa kwenye uwanja huru (neutral ground) siyo upinzani wala chama tawala. Nitasubiri atakayetoka CHUMBANI na taulo huyo ndio baba. Natambua kuna hoja itaibuka ya haki yangu kama mpiga kura, hiyo nayo ni mojawapo ya haki nilizoridhia kuzipoteza kiroho safi.

Wapinzani mmeniangusha kwa kuunga mkono juhudi. Kuanzia leo natangaza sitopiga kura tena mpaka naenda kaburini kiongozi bora wa maisha yangu na familia yangu nitaendelea kubaki mimi mwenyewe. Nitaheshimu na kutii sheria na kulipa kodi kwa kadiri itakavyobidi. Niwatakie uchaguzi mwema mimi tayari ni miongoni mwa wale ambao hawatopiga KURA.

Hivyo nami niungane nanyi kuunga mkono juhudi.

Asanteni
Usifanye siasa kwa hisia (feelings) utaumia sana na utafanya maamuzi mabaya, ndio maana unakuta mtu leo CCM, kesho CDM, keshokutwa NCCR, mtondogoo ACT, siku nyingine CUF. Kuwa na sababu au itikadi. Hii ndiyo itakuongoza uwe wapi. Tatizo la wanasiasa wetu ni kwamba hawajui wanataka nini. Wanaishia kuhama na mtu, au kuhama chama kwa hasira. Acha kutafuta maslahi binafsi ndani ya chama, ni makosa. Simamia itikadi unayoamini hata chama kikiyumba simama imara.
 
Back
Top Bottom