Haya ya kweli kuhusu Rock City Mall?

Haya ya kweli kuhusu Rock City Mall?

((( SITOSAHAU ))))
SIKU MCHEPUKO" ULIPONIACHIA MTOTO KWENYE DALADALA.
soma story hii.

Mke wangu MARY aliamka mapema na kuniomba niende nikamsaidie badhi ya majukumu sokoni, kwani yeye siku hiyo alikuwa akijisikia vibaya, Hakukuwa na wakumtuma kwani tangu Tuoane tuliishi sisi Wawili hatukubahatika kumpata MTOTO KWA MIAKA ZAIDI YA MI TANO YA NDOA YETU".
Nikaenda mpaka kituo cha DALADALA ingawa nilikuwa na mawazo mengi sasa" kutokana na badhi ya mambo yangu kuenda ndivyo sivyo.

Nikiwa kiwa katika DIMBWI LA MAWAZO daladala iko kituo cha mbele mara MAMA MMOJA akiwa na MTOTO MCHANGA akaniita dirishani na kuniomba NIM'BEBEE MTOTO kwani daladala ilijaa naye alihitaji kupanda.
Nilimpokea mtoto na baada ya hapo nikamwona akizinguka upande wa pili apande, nami nikaendelea kuwaza lakini safari hii nikasali kimoyomoyo kuwa MUNGU Anipe nami Baraka ya mke wangu kuzaa.

Mawazo mchanganyiko yaliendelea kwa muda mpaka nilipokuja kugundua kuwa Daladala ndio inaingia kituo cha mwisho.
Nikakaa pale kusubiri watu washuke ili nimkabazi mtoto yule kwa mama yake lakini CHA KUSHANGAZA ni kwamba kila MTU ALISHUKA NA KUJIKUTA NIPO MIMI NA KONDA TWAANGALIANA.
Nikamuuliza mama wa mtoto yuko wapi?
Akadai yeye hajuwi wala hakuona mama mwenye mtoto.....

Nikamhadithia jinsi ilivyo akaniambia MJOMBA HAPO NENDA POLISI TU.
Nikaenda polisi na kutoa maelekezo nikiwa na konda pamoja na mtoto yule. Baada ya maelezo wakanambia sasa wewe baki na mtoto na sisi tunaendelea na UPELELEZI".
Nikaahirisha kufanya yale niliyodhamiria na kurudi nyumbani MKE WANGU ALINISHANGAA!!!! na hata nilipojaribu kuelezea hakunielewa zaidi ya kudai MTOTO YULE LAZIMA AWE NA MAHUSIANO NAMI"
akazidi kusema kuwa lazima NIMEZAA NA MTU NA KANISUSIA BAADA YA KUTOMJALI AU ANATAKA NIOANE NAE AU MAMBO MENGINE AMBAYO YAWEZEKANA KUWA SIRI ZA MIMI NA HUYO MAMA YAKE.
Na mke wangu alikasirika aliondoka na kwenda kwao.
Ikanilazimu niende kituo cha kulelea WATOTO YATIMA nilichoambiwa kiko pale mtaani kwetu, na baada ya kufika pale na kutoa maelezo wakakubali na kumchukuwa mtoto jambo lililofanyika ndani ya siku nne maana ilinibidi niende pia na polisi wathibitishe.

Baada ya hapo nikaanza safari ya kwenda kijijini kwa mke wangu mary, kufika kule BABA NA MAMA wa mke wangu wakadai kuwa kwa UNYAMA NILIOMFANYIA MWANAWAO HAWATANIRUHUSU NIRUDI NAE TENA NA SASA WATAMRUHUSU AOLEWE NA MTU MUNGINE.

Nililia kama mtoto mdogo nikiomba WANISAMEHE NA HAWAKUNIELEWA, Kwani mkasa huu hata mimi wanipa wakati mgumu lakini hawakuelewa.
Nikakumbuka sisi Kwa KABILA LETU tukiwa tunahasira tuna asili moja ya KUJINYONGA".

Jioni ile nikanunua kamba yangu na nilipohakikisha kila mtu kalala, nikapanda juu ya mti kamba yangu shingoni na kisha kujitupa chini ili kama ile ininyonge...
Nilitapatapa pale na taratibu nikahisi haja kubwa ikinitoka kwa shida ikiashiria ndio nilikuwa NAKATA ROHO NIKALIA KILIO CHANGU CHA MWISHO KWA UCHUNGU" kabla kunaswa kibao na DEMU niliyelala naye GUEST BUBU huku akinisema" MWANAUME hauna haya wewe mimi nakuangalia hapa warusha rusha miguu na kujifanya unalia kumbe UNAKUNYA KITANDANI??
Mwanaharamu mkubwa wewee!!!!

Ha ha ha ha ndoto nyingine buana laana tupu.
 
Ya kawaida sana kulinganisha na ipi??!!! Acheni kujidai mnajua na kuponda kila kitu...hio mall wamejitahidi sana.

Kweli mkuu! humu kuna mijitu inajidai inafahamu sana vitu, yaani badala ya kukubali kuwa angalau tunapiga hatua, wao ni kuponda tu.
 
Yaani daah inasikitisha sana..huku jamvini kuna watu hawana hata ethics za uzalendo na kusifia maendeleo wao ni kuponda tuuuuu utafikiri ni wahamiaji waliopewa vibali vya kuwa watz...ma intarahamwe...

Ukisifiwa huku haifai itakusaidia nini? Unajivunia kitu ambacho ni cha kawaida kwa wenzio o au wewe una hisa unatangaza biashara
 
Ngoja nipite tu..wamejitahid ila ni shopping mall ya kawaida..nimependa tu wana parking kubwa sana..na bado wanaendelea kuamisha watu hivyo in the near future wakiendelea na expansion huenda ikawa kubwa East Africa..
Japo ni hakika haitofanya vizuri kama Mlimani city coz watz wengi hawana mazoea ya kufanya shopping kwenye mall zenye ghorofa mbili tatu au zaidi...Mlimani City ni flat mall na ndio desturi zetu za shopping tulizozoea watz.. Machinga complex ina ghorofa nne kama sio tano na imefail kabisa sababu sio desturi yetu kupanda ghorofa kwenda kufanya shopping.

mkuu inatefemea na mandhari yake,msasani mall inafanya vizuri sana na ni ghorofa pale pembeni ya o'bay police
 
Iwe nzuri ama mbaya,watanzania wengi hawatanufaika nayo,wamezoea shoping magengeni kununua nyanachungu,bamia,mbilimbi, mchunga na matembele kwa mafungu.
 
Iwe nzuri ama mbaya,watanzania wengi hawatanufaika nayo,wamezoea shoping magengeni kununua nyanachungu,bamia,mbilimbi, mchunga na matembele kwa mafungu.

Umezoea wewe sisi tushabadilika...ilikuwa ivo zaman bt not now
 
Mall kama hizi target yake sio wapanda madaladala, target ni middle class citizens ambao kibongo bongo hawezi kukosa hata Vitz au hela ya kupanda daladala mbili at least. Hao wanaoshindwa kupanda daladala mbili waende Nyakato Sokoni au Makoroboi au lah wasubiri gulio la Jumamosi pale Nyakato.Unaambiwa bei ya square meter moja ni dola 22 kwa mwezi floor ya chini na dola 20 ukipanda juu, kwa hiyo bei ya bidhaa nyingi humo sio kila mtu atamudu
Apande daladala mbili kwenda huko kufuata huduma ambayo anaipata mjini kwa kupanda daladala moja?(hapa ndipo hoja yangu ilipo)Ukweli unabaki palepale kwamba hiyo Mall ingekuwa busy zaidi kama ingejengwa town kuliko huko iliko sasa.Hata Petrol stations zinalenga hao middle class wenye magari lakini zimebanana mjini siyo Nyasaka,unadhani ni bahati mbaya tu au hawawajui wateja wao?Hicho kiherehere cha kwenda huko nakipa mwezi mmoja tu then watu wataendelea kufanya shopping zao mjini walikokuwa wanafanyia awali huko wataenda mara mojamoja mno kama picnic tu labda ma-middle class wa huko.Kama mtu anauwezo wa kupata huduma hiyo town unadhani atadrive ama kupanda daladala kuelekea huko?Ili akafanye nini? Labda masharobaro wasio na kazi.
 
Middle class ni wanaopata sh ngapi kwa mwezi?
Petrol station ziko pasians, Iloganzala, sabasaba,nyasaka, reli (pasiansi), nyingine inanengwa kifua wazi.

Hivi hapo kuna parking ya baskeli? Sijafikamo bado
 
Middle class ni wanaopata sh ngapi kwa mwezi?Petrol station ziko pasians, Iloganzala, sabasaba,nyasaka, reli (pasiansi), nyingine inanengwa kifua wazi. Hivi hapo kuna parking ya baskeli? Sijafikamo bado
Suala la income ya middle class ya bongo nadhani Ulukolokwitanga ndo atakuwa na data zaidi na atakujibu maanake ndo kalileta hapa.Sikatai uwepo wa Petrol stations huko lakini zilizoko town ndo ziko busy zaidi tofauti na huko Nyasaka zikifuatiwa na Lango(Mlango Mmoja) Barnaba (Buzuluga) labda na Mkuyuni.Chombo chochote kinachoweza kufika hapo hakiwezi kosa sehemu ya ku-park.We kama una phonex or Avon,njoo nayo.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nipite tu..wamejitahid ila ni shopping mall ya kawaida..nimependa tu wana parking kubwa sana..na bado wanaendelea kuamisha watu hivyo in the near future wakiendelea na expansion huenda ikawa kubwa East Africa..
Japo ni hakika haitofanya vizuri kama Mlimani city coz watz wengi hawana mazoea ya kufanya shopping kwenye mall zenye ghorofa mbili tatu au zaidi...Mlimani City ni flat mall na ndio desturi zetu za shopping tulizozoea watz.. Machinga complex ina ghorofa nne kama sio tano na imefail kabisa sababu sio desturi yetu kupanda ghorofa kwenda kufanya shopping.

Sawa kabisa, nimeipenda hii.
 
Sasa hapo cha kushangaza ni nini? Wasukuma wamesafiri aftica mashariki yote?
 
Kwa Mza ninayojifahamu they have a long journey to go culture ya watz kufanya shopping hasa kwenye maduka yaliyopo magorofani na malls bado ni changamoto hata maduka yaliyopo katikati ya miji , ikumbukwe supermakerts kubwa kufunguliwa tz ilikuwa ni za shoprite zilizokuwa Dar na Arusha kwa Kenya malls wakuwa nazo kitambo na tendes ya kufanya shopping supermarkets ishakuwa kawaida yao
Rc mall itawatoa tongotongo wakina Shija na Mabula
 
(GAZETI LA TANZANIA DAIMA)

Ya kwanza na kipekee Afrika Mashariki

Ujenzi wa Rocky City Shopping Mall, umeanza Agosti mwaka 2012, ambapo jengo limegawanyika katika maeneo makubwa matatu. Eneo la kwanza ni jengo, eneo la maegesho ya kucheza watoto (Children Park) na maegesho ya magari.
Eneo la jengo lina ukubwa wa mita za mraba 48,250, lina ghorofa tano kushuka chini ya ardhi na nyingine nne juu ya usawa wa ardhi.
Eneo la maegesho linabeba magari 600, pikipiki na baiskeli 150, huku eneo la watoto lina mita za mraba 15,200, jumla ya eneo ni mita za mraba 71,990.
Kwa mujibu Magazini, gharama za mradi wa ujenzi wa kitega uchumi hicho zilikadiriwa kuwa shilingi bilioni 60.45, lakini jumla halisi ya mradi itapatikana baada ya kufunga mradi kamili. Kuna sehemu zimeongezeka kuna sehemu zimepungua.
Ndani ya jengo kuna maeneo ya benki, ambapo hivi sasa kuna benki tano za CRDB, NMB, NBC, Stanbic na FNB, ambazo zimekwisha kuomba nafasi.
"Tuna mwekezaji mkubwa, ambaye ni TSN, ndiye mkubwa kwa sababu anaongoza kwa kuchukua eneo kubwa. Amechukua mita za mraba 3,320, lakini kwa kadri tulivyogawanya mpaka sasa tuna vyumba 145, ndani yake kutakuwa na maduka ya nguo, vifaa vya umeme, sehemu za chakula na kumbi mbalimbali, haya ndiyo madhumuni makubwa ya hili jengo. Chumba cha chini kabisa kina mita za mraba 30 na chumba cha juu kina mita za mraba 1,660," anasema Mhandisi Magazini.
Mhandisi huyo anafafanua kuwa, jengo hili linazidi ukubwa maeneo ya maduka makubwa ‘shopping malls' zilizopo sasa zinazofanya kazi nchini.
Rocky City Mall inaizidi kidogo Westgate ya Nairobi. Ukubwa wake unatofautishwa kwa mita za mraba zilizomo ndani ya jengo lenyewe.
"Mlimani City ya Dar es Salaam wana futi za mraba 12,000 kama mita za mraba 11,500, Westgate ilikuwa na mita za mraba 30,000, wakati hili lina mita za mraba 48,250 kwa maana ya jengo lenyewe. Lakini kinachotoa ukubwa zaidi ni eneo la kupangisha (ratable space), hapa tuna 32,250, hicho ndiyo kinatofautisha ukubwa kati ya mall na mall," alisema.
Alisema kwa sasa hakuna shopping mall inayoweza kulingana na Rocky City lakini zipo nyingine zinajengwa ambazo zitaizidi. Alisema Kenya wanajenga ambayo itakuwa kubwa zaidi ya hiyo.
 
Kuna mall moja Uganda inaitwa ACACIA Mall hiyo haikaribii kabisa au westgate ya kenya lakini sio mbaya wamejitahidi sana

Nadhani ambao wamei-rank hvyo wamezingatia vigezo vinavyopimika na kuelezeka.Nadhanı mall kubwa kabisa East&Central Africa wanaenda kuijenga Kawe kupitia mradi wa National Houşing.
 
Hakuna kitu hiyo ni ndogo tu

Usijete ubishi wa kijinga,hilo jengo linamilikiwa na mfuko wa LAPF ni jengo bora na la kisasa afrika mashariki na kati,linauwezo wa kuegesha magari mia sita kwa wakati mmoja.
 
Of course unachosema ni sahahi, lakini kwa uzoefu wangu kwenye Mall zingine nilizofika ikiwemo Africa's biggest Mall, THE CANAL WALK ya Cape Town,,, na pia WaterFront ya Cape Town na pia WestGate ya kabla ya Ughaidi, Hii Rock City Mall ni kubwa kuliko Westgate, Space ya ndani kwa ghorofa zote ni mara nne ya Mlimani City. Parking space ina zaidi ya mita 500 pande zote. Naweza kusema iko sawa au inazidiwa kidogo na WaterFront ya Cape Town.

Ila kibiashara nina uhakika ndani ya miaka mitatu hadi mitano vyumba vingi havitakuwa na wapangaji kwa vile mji wa Mwanza hauna Middle Class ya kutosha ku support such a big investment na pia utamaduni wa watu wa kanda ya ziwa ni ubahili. Wanatoka home wamekula Ugali mkubwa na Samaki wakienda Mall ni kunywa soda tu

Nakubaliana nawe kiasi,ila sikubaliani na kwamba baada ya miaka3 vyumba vitakuwa vitupu,umefanya utafiti wowote?investment yoyote huanza kwa kusuasua na itafika hatua itaimarika.Kuhusu utamaduni nalo sikubaliani nawe Mimi nimekaa mwanza najua mji huo unamchanganyiko mkubwa wa watu kwa hiyo athali ya utamaduni unaouzungumzia so kubwa kama unavyofikiria.pia tukumbuke si watu wote hupenda Ku shop kwenye mall kuna class na kumbuka halo kuna taasisi za kifedha,huwezi toa pesa hapo harafu uende mjini kati uka shop wakati hapo kuna kila kitu.
 
Apande daladala mbili kwenda huko kufuata huduma ambayo anaipata mjini kwa kupanda daladala moja?(hapa ndipo hoja yangu ilipo)Ukweli unabaki palepale kwamba hiyo Mall ingekuwa busy zaidi kama ingejengwa town kuliko huko iliko sasa.Hata Petrol stations zinalenga hao middle class wenye magari lakini zimebanana mjini siyo Nyasaka,unadhani ni bahati mbaya tu au hawawajui wateja wao?Hicho kiherehere cha kwenda huko nakipa mwezi mmoja tu then watu wataendelea kufanya shopping zao mjini walikokuwa wanafanyia awali huko wataenda mara mojamoja mno kama picnic tu labda ma-middle class wa huko.Kama mtu anauwezo wa kupata huduma hiyo town unadhani atadrive ama kupanda daladala kuelekea huko?Ili akafanye nini? Labda masharobaro wasio na kazi.

daladala mbili za wapi wewe?! kutoka kisesa ambako ni nje kabisa ya mji hadi rock city mall ni gari moja, kutoka buhongwa hadi rock city mall ni gari moja, kutoka airport hadi rock city mall ni gari moja, sasa wewe umekazana wee gari mbili!
 
Back
Top Bottom