Haya tena ndugu zangu leo hii tena ndio My Happy birthday yangu

Happy Birthday Mkuu... MziziMkavu
Hebu na mie nidadavulie nyota yangu ya Mizani...............LOL

happy_birthday_candles-2010.jpg
 
Last edited by a moderator:
Happy Birthday Mkuu... MziziMkavu
Hebu na mie nidadavulie nyota yangu ya Mizani...............LOL

happy_birthday_candles-2010.jpg
Mkuu Mtambuzi una nyota nzuri sana ungelifaa kuwa Hakimu wewe asante kwa mishumaa ya HappyBirthday angalia Maelezo ya nyota yako ya Mizani hapo chini.

NYOTA YA MIZANI (LIBRA)

  • Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni VENUS (ZUHURA).
  • Siku yao ya Bahati ni Ijumaa.
  • Namba ya Bahati ni 6.
  • Rangi ya Bahati ni Kijani isiyoiva.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.

KIPAJI CHA MIZANI


(Extra Sensory Perception)

Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa.

TABIA ZA MIZANI:

Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.

Ni watu wastraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.
TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI

Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda

mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.


Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.


Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa

mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.


Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu

yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.

Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.

TABIA YA MIZANI KATIKA FEDHA


Watu wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kutokuwa na maamuzi katika masuala ya fedha. Lakini hiyo siyo sababu ya wewe kufikiri kwamba wao ni wajinga.


Wanapofanya hivyo huwa wanapima au kufikiria kuona uwezekano wa fedha kutumika vizuri.


Ni watu wenye mipango mizuri na mara nyingi kwa kutumia uzoefu na kipaji chao kidiplomasia na upole, huwa wanapata mafanikio katika biashara zao.


Wana kipaji cha kuelewa watu wengine wanahitaji nini na wanatumia maneno matamu kuwashawishi wawape wanachokitaka na wanafanikiwa.


Wanapenda sana vitu vizuri na vyenye thamani na wako tayari kutumia fedha yeyote kutekeleza malengo yao.

Kwa ujumla ni watumiaji wazuri na wenye ubinafsi mkubwa.

{mospagebreak}
MAVAZI YA MIZANI

Wenye nyota ya Mizani wanatakiwa wavae nguo yenye kupendeza zenye mapambo na zenye kuashira mahaba.

Nguo ziwe za rangi ya Pinki au rangi ya udongo.

Kitambaa kiwe cha
kotoni chepesi na chenye picha picha, kisiwe kile ambacho hakikuchorwa kitu.

Wavae sana mikanda na wapende kuvaa nakshi za maua pamoja na skafu au mitandio iliyoingia. Wanapendelea mavazi ya ushanga na mikufu.


MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala figo, sehemu ya utumbo mkubwa, kiuno, mpaka sehemu ya juu ya makalio nyuma

Sababu kubwa ya maradhi yao ni kwamba wanapenda sana kutafuta amani na suluhu hata wakiudhiwa au kukasirishwa. Matokeo yake

wanavunjika moyo na kujinyima yale wanayoyapenda. Sana na hiyo inawafanya waudhike na wajisikie vibaya na inawasababishia
maradhi.

Magonjwa yao makubwa ni
figo, kibofu cha mkojo, ugonjwa usioambukiza wa ngozi unaowasha na unapojikuna huvimba (Eczema),maradhi ya misuli ya kiuno na matoki.

Tatizo lingine kubwa ni unene.Watu wa mizani wanapenda sana kula na hiyo inatokea sana wanapokuwa wameudhiwa. Wao wanaona ni bora zaidi kuondoa hasira zao kwa kula chakula.


KAZI ZA WENYE NYOTA YA MIZANI


Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia uwezo wao wa kuzaliwa na inawawia vigumu wakati mwingine kutafuta kazi wanazozipenda.


Wanapenda kufanya kazi katika mazingira ya amani na yasiyo na usumbufu.

Kazi zao hasa zinakuwa za uhusiano wa jamii ushauri wa ndoa, biashara ya sanaa, ushauri wa mambo ya urembo au mwanasheria.
FAMILIA ZA MIZANI

Wazazi wenye nyota ya mizani wanapenda sana unadhifu na wanapenda watoto wao wawe nadhifu na wenye mavazi mazuri.

Wanapenda kutumia muda mwingi na fedha nyingi kuwafunza watoto wao tabia nzuri. Kwao ni muhimu sana mtoto akikubalika na kila mtu.
Wanapenda amani katika nyumba zao na wana tabia ya kuwapangia watoto wao namna ya kuishi na kufanya vitu ambavyo wao wnyewe wameshindwa kuvifanya.
MADINI YA MIZANI

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa
LAPIS LAZULI. Mawe kama nye rangi ya Bluu iliyokoza, wamisri wanayaita mawe ya peponi. Yakiwekwa kama kito kwenye pete ya dhahabu yanaleta mizani kwa wenye nyota hii.

UHUSIANO WA KIMAPENZI


(Punda na Mizani)


Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

VYAKULA VYA MIZANI:

Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula au Matunda yafuatayo ambayo ndio yanayotawaliwa na nyota yao,Tufaha
(Apple), viazi Mviringo (Potatoes), Chaza (Oyster) na Nyama ya Njiwa.
NCHI ZA KUISHI ZA MIZANI:

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii ya Mizani.

Miji hiyo ni Copenhagen(Denmark) na Vienna (Austria) na nchi ni Canada na Japan.
RANGI ZA MIZANI

Wenye nyota hii wanapenda rangi zilizopakwa juu juu na laini hivyo wanashauriwa watumie rangi ya aina yeyote lakini iwe hafifu katika nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara.


(NYOTA ya Mizani ni Kwa wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 September na 22 Oktoba ya mwaka wowote.)
 
Thank you Mamndenyi

Ohooo Mzee mwenzangu MziziMkavu leo ndio unazaliwa bwana...Hongera sana mkuu miaka 48 sio mchezo...Mwenyezi Mungu akuzidishie na akujalie baraka na mafanikio katika mwaka wako mpya wa 48.
Asante sana mkuu wangu Young Master GOD Bless you..........

Mungu akupe maisha marefu akuepushe na mitihani ya duniani..."Epi bazidei" mtu wangu wa nguvu.
Mkuu Ritz asante sana na wewe pia Mwenyeezi mungu akupe afya njema na kila kitu unacho muomba akupe Mungu ameen.

Mwenyezi Mungu akujalie kila Jema. I wish you a peaceful and enjoyable happy birthday mdogo wangu Mzizi Mkavu

View attachment 73736
Asante sana Mama Mdogo Mungu akubariki ameen.

Shikamoo MK...Happy birthday to uuuuu..
Marahaba bibie Zion Daughter Thank you GOD Bless you ameen.
 
Last edited by a moderator:
Asante Mkuu.@Bujibuji Nina tamani laiti ningelikuwa huko nyumbani ni enjoy sana lakini wapi nipo ugenini si unajuwa Home is Best nyumbani ni kuzuri Bwana.......wacha tu ugenini ni ugenini ni sawas awa tu na Jogoo wa Shamba hawiki Mjini nitafanyaje na Mto wa maji ukiyavulia nguo itabidi uyakoge ....
 
ubarikiwe sana na mungu akupe maisha marefu upeo ,hekima na busara hongera sana kwa kuliona jua karibu sana mtoto mzuri nitakuletea nepi badae
 
hahahah bibie King'asti kwani unapomuomba Mungu unamuomba kitu gani zaidi ya uzima afya,Bahati ya maisha ipo ya aina nyingi kupata watoto wema kazi,kupata mume mwema hizo zote ni jami ya bahati kwani wewe unafikiriaje neno bahati? Katika maisha omba upate bahati sio Utajiri bibie bahati ni kitu kizuri kuliko utajiri upo pamoja na mimi bibie?

bahati nnayo basi kam ndo hivyo, cant complain. Natafuta bahati ya kupungua mwili. Afu unaniuzia chai, nangojea ofa ya ile products zako tuuuu, ndo bahati ilobakia, lol
 
Happy birthday brother, wish u God's blessings and joy!!!!
Mkuu Mentor Thank you and GOD Bless you......

ubarikiwe sana na mungu akupe maisha marefu upeo ,hekima na busara hongera sana kwa kuliona jua karibu sana mtoto mzuri nitakuletea nepi badae
Mkuu prianka asante sana sasa wataka kuniletea Nepi kulikoni? nimgeuka kamtoto kadogo hahahahahah umenichekesha weweeeeeeee

bahati nnayo basi kam ndo hivyo, cant complain. Natafuta bahati ya kupungua mwili. Afu unaniuzia chai, nangojea ofa ya ile products zako tuuuu, ndo bahati ilobakia, lol
Bibie King'asti Nikupe Ofa ya kupunguza unene pasipo na gharma? Fanya hivi kila siku ( Kwa ajili ya tiba hii ya asili, changanya kijiko moja ya asali mbichi (unheated) na vijiko viwili vya maji ya limau au ndimu katika glasi ya joto au maji vuguvugu (si kuchemsha maji!).

Kunywa mchanganyiko huu wa asali na limau/ndimu kila unapoamka asubuhi tumbo likiwa tupu. Pia unatakiwa kunywa mchanganyiko huu mara baada ya mlo kubwa na vyakula vya mafuta, hii inarahisisha kwenye digestion .


Ukiendelea na tiba asili ya kupunguza uzito unatakiwa kuzingatia kanuni kama vile kutengeneza tabia katoka milo unayokula pia kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.)


Mungu aendelee kukulinda, akupe maisha marefu yenye furaha na amani tele!!
HBD kaka yangu MziziMkavu !!!
Asante sana mama D Dada yangu Mwanvita hajambo lakini?Mpelekee salam zangu nyingi tu mwambie nime M miss sana...............
 
Last edited by a moderator:
Hongera zako MziziMkavu popote pale ulipo! Ni hongera tunakupa maana kuna wengi waliotamani angala kufika hapo ulipofikia leo ila imekuwa kama ndoto.
MUNGU MWENYE MAMLAKA PEKEE AKUVUSHE ZAIDI NA ZAIDI.
 
Last edited by a moderator:
To My fellow Saggitarius MziziMkavu; Here is to wishing you a very happy birthday and a bright future. Remember "The more the candles are, the more the wishes come true":rockon:
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom