Haya shime tujiandae kuhesabiwa!

Haya shime tujiandae kuhesabiwa!

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,192
Reaction score
6,144
Haya kumekucha!

Wale ndugu zangu wapogoro wanaoshinda na kuweka kambi kwenye misitu wakichanja mbao! TUKAHESABIWE

wale Dada zetu wa biashara poa kwenye madanguro kuanzia Sinza,Uwanja wa fisi mpaka kwa wahaya ndani ndani huko! TUKAHESABIWE

wale ombaomba wakukesha barabarani maeneo ya Chamwino mpaka area D
TUKAHESABIWE

wale watoto wapambanaji wasio na makazi wanaolowea kwenye vibanda usiku na kudamkia maeneo ya Mwenge kwenye mataa! TUKAHESABIWE!

wale madereva wa masafa marefu... Maporter a.k.a wabeba mizigo kuanzia machame pale getini mpaka kibo kileleni wazamiaji migodini mashimoni haya tokeni TUKAHESABIWE

SENSA KWA MAENDELEO! JIANDAE KUHESABIWA!
 
Sensa ya Tz ya siku 3 itakuwa na double counting.
 
Asante kwa kutukumbusha mkuu. Lakini mbona kama una hasira vile? 🙂
 
Back
Top Bottom