Special Thread ya Dar Mpya: Paul Makonda afanya Ziara Jijini la Dar kusikiliza kero za wananchi

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,071
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.

Hii thread itakuwa Maalum kwa ajili ya kujuzana na kufahamishana kile kinachoendelea Dar Es Salaam.

Ziara hiyo ilianzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.

Hili la Dar Mpya naliunga mkono, na nadhani kuwa, wakazi wa Dar es Salaam sasa wanapaswa kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto kuliko kuwa wapiga domo!

Ndani ya Dar Mpya program, tunatarajia mazuri ambapo naomba nizungumzie machache!

  1. Usalama wa raia
    • Dar mpya inakuja na uhamasishaji wa ujenzi wa vituo vikubwa, vya kati na vya chini vya polisi. lengo ni kuhakikisha usalama unapewa kipaumbele kwa sasa!

    • Tazama kwa makini, jinsi wana mzizima wanavyoteseka kwa kugharamia masuala ya ulinzi kwa pesa nyingi sana na yet hawaishi eneo salama.

    • Ukiwa mkazi wa Dar es Salaam, tazama nyumba ngapi zimewekwa grills, electric fence, zile waya za miba, security cameras, walinzi milangoni na ulinzi shirikishi! tunaingia gharama zote hizi kwa kuwa suala la ulinzi hatujakaa na kulifikiria kuwa ni suala lenye kuhitaji ushirikiano. fence ya umeme haizuii mwizi anayekuwinda mlangoni kwako, haiondoi vibaka mtaani kwako na uhalifu mwingine! kama tutamuunga mkono makonda na kuamua kushiriki ktk ujenzi wa polisi posts, au vituo vya level nyingine, then Dar itakuwa salaama kwetu

  2. Mipango miji
    • Hawa jamaa nao ni moja kati ya watu wanaoliangusha jiji hili! Ujenzi holela ni miongoni mwa changamoto namba moja ktk issues za usalama na maisha bora kwa raia!

    • Kuna uhalifu mwingi tandale kuliko masaki, lkn pesa inayozunguka au kuishi masaki ni karibu mara 1000 Zaidi ya pesa zote zilizopo tandale (thamani ya nyumba, magari, cash na asserts nyingine)! kwanini Tandale inauhalifu Zaidi ni kwa kuwa ujenzi holela huwa ni maficho mazuri ya waharifu!

    • Huduma za jamii ni ngumu kupata ukiwa ktk makazi duni, kupitisha miundo mbinu ni gharama Zaidi, maana ukileta umeme hakuna pa kuchomeka nguzo, ukileta maji huna pa kuchimba mabomba, na ukitaka kuleta barabara then utakuwa na nyumba nyingi za kuzifidia!

    • Mipango miji, nyinyi nao ni tatizo sawa na lile la usalama! makonda anapaswa awatizame kwa makini!

  3. Usafi wa mazingira
    • Balaa hili linakuzwa Zaidi na ukosefu wa misingi maalum ya ukusanyaji na uzoaji wa taka. hata wananchi wakijitahidi vipi, kushindikana uzoaji taka utarejesha nyuma sana zoezi husika.

    • Pia wananchi kuwa wapingaji Zaidi ya watu wa kujitolea kunaleta changamoto ktk hili

  4. Kuzingatia sharia
    • Hakuna jambo baya ktk jiji hili kama kutozingatia sharia na taratibu za ukaazi.

    • Kuna Bar na Groceries barabarani, nje ya kuta za shule na makazi ya watu. ingawa sharia za nchi zinataka shughuli zote za vilezi ziwe ktk muda maalum na lazima ziwe ndani na sio nje!

    • Bodaboda wanajitengenezea vituo holela na hawawi regulated, so wezi wanaongezeka na hii inaathiri wote, abiria na wafanyabiashara wa bodaboda.

    • Biashara holela

    • Matumizi mabaya ya viwanja vya wazi au kubadili matumizi ya maeneo yaliyotengwa rasmi kwa shughuli za kijamii!
Karibuni kwa Michango.

Mkuu wa mkoa Leo ameanza ziara rasmi ya kuzungukia jiji ili kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za maeneo ya jiji la Dar es salaam!
Mkuu Wa mkoa ameongozana na wataalamu na watumishi Wa idara mbalimbali ikiwemo TANESCO, police, ardhi, NEMC na idara zingine!
Ambapo watamsaidia kujibu maswali kuhusu idara mbalimbali

Kutokana na kuguswa na uwajibikaji Wa mkuu Wa mkoa; sikutaka kubaki kuwa mkosoaji Wa kila jambo; imenibidi nifunge safari alifajili na mapewa kwenda maeneo ya kigamboni kujumuika na mkuu Wa mkoa kusikia changamoto za wana kigamboni.

KERO ZITAKAZOHITAJI MAJIBU
Katika kupita hapa na pale watu Wa kigamboni wamejiandaa kuuliza hasa mambo yafuatayo.

1. Kwanini serikali isitoe mbadala Wa eneo la kuchimba vifusi kutokana na kupigwa marufuku machimbo ya Mjimwema na kwingineko kitu ambacho kimaathili sekta ya ujenzi Kwa kukosa vifusi?

2. Kwanini daladala zinazopita daraja la kigamboni zisiondolewe tozo au kupunguziwa ili ziwe nyingi zaidi kupunguza kero ya usafiri kigamboni?

3. Kwanini tozo ya daraja na kivuko Kwa nagari madogo hazitofautiani kwa kiwango angalau kuweka unafuu? Utaratibu Wa kodi za vivuko upoje?

4. Lini maeneo mapya na pembezoni yatapatiwa Umeme?

5. Wimbi la vibaka na wezi/ kuongezeka nini mikakati ya kutokomeza kero hii?

6. Wenyeviti na watendaji wanaouza maeneo Mara mbilimbili ni adhima ya kuwashughulikia?

Maswali na kero ni nyingi tupo hapa kusikia majibu ya mkuu Wa mkoa na jopo lake!
TUMUUNGE MKONO!

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, anaendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za Wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam.

Sasa katika moja ya mikutano yake Temeke, mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku uwepo wa Migambo katika vituo vya Polisi ambapo amedai kuwa maranyingi lawama zinazoelekezewa jeshi la Polisi husababishwa na utendaji wa Mgambo hao.\

“Ni marufuku kituo cha polisi kuwa na mgambo na mimi nitafanya operesheni zangu, nikikuta mkuu wa kituo ameacha mgambo kwenye kituo chake nitakula sahani moja na Kamishna Sirro, wakati mwingine Jeshi la polisi linapakwa matope kumbe ni matope ya mgambo” alisema.



Source:: Times Fm


DAR ES SALAAM: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul, Makonda amewataka wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ili wasiingie katika matukio ya kihalifu.

Akizungumza leo Jumanne, Novemba 22 katika uzinduzi wa madarasa nane ya Shule ya Msingi Mbande iliyoko wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Makonda amesema mtoto yeyote aliye chini ya umri wa miaka 17 atakayekamatwa kwa tuhuma za uhalifu, na wazazi wa mtoto huyo atakamatwa.

“Mtoto wa umri wa miaka 17 akikamatwa kwa kosa la uhalifu, uvamizi au akikamatwa kwa makosa ya uporaji au panya road nimewaambia polisi na wazazi wao akamatwe. Mtoto ni wakwako unatakiwa kuangalia muenendo wa mtoto wako, kwahiyo wazazi wanatakiwa kuwa karibu na watoto wao,” Makonda aliwaambia wazazi pamoja na wanafunzi wa shule ya Mbande.

RC Makonda amewataka wazazi hao kuwahimiza watoto wao kusoma pamoja na kufuatilia maendeleo yao ya kila siku. Haya sasa wale waswahili wa mitaa ya Buguruni, Mbagala na Kwamtogole na kwingineko wakae mkao wa kwenda kufia jela kwa nini wameshindwa kubana watoto wao.

Hiyo ni mupya ya Mukulu ya mukoa.
Nimeshangazwa kuona serikali imejenga soko maeneo ya Bunju B ( Sokoni), vibanda vipo tu bila ya kuwa na wamiliki, ili hali watu wanapanga vitu vyao pembezoni mwa barabara.

Usumbufu unakuwa ni mwingi kwa watembea kwa miguu na ata watumiaji wa magari. Kwanini hawa watu watusumbue wakati soko lipo?

Ombi langu kwa mheshimiwa Makonda tembelea na huku Bunju kama unavyotembelea masoko mengine huko Temeke.

Daladala zimeandikwa kuwa zinaishia bunju b sokoni, ila zinaishia bunju b bila kuingia sokoni. Makonda tembelea huku nako pia ni Dar eneo lako la kazi.

Wadau,

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda ana ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kusikiliza kero mbalimbali za wananchi. Kuzunguka huku kunaambatana na Watendaji mbalimbali kuanzia serikali za mitaa, Kata, mpaka Wilaya au Manispaa ambao ndio wajibu tuhuma. Wapo Wenyeviti wa serikali ya Mitaa, Polisi, Madaktari, Maafisa Ardhi, Maafisa Masoko, Elimu etc

Kinachofurahisha ni jinsi ambapo Wananchi hutoa malalamiko yao kisha Mhusika huitwa na kuanza kujitetea. Yaani ni kama "Public Court" fulani hivi ambapo Mhusika hutakiwa kujibu tuhua zake hadharani. Hapa ndio patamu sana maana wengine wanaonekana kabisa hawana majibu, wanajikanyaga, kujikanganya au kutetemeka.

Kuna haja ya hii style kuanza kutumika pia kwa Mawaziri Mbalimbali waliopita, Makatibu wakuu wa Wizara, Wakuu wa Idara, Wakuu wa mashirika mbalimbali, Taasisi mbalimbali etc. Tunatafuta Uwanja Mkubwa kama Uwanja wa Taifa hivi tunaanza kumwagia mtu tuhuma mmoja mmoja.
TAARIFA KWA UMMA
Novemba 24, 2016

Leo Novemba 24, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameendelea na ziara yake mkoani humo iliyobeba ujumbe wa tunakufikia ulipo, kwa kutembelea wilaya ya Ilala akianzia na kiwanda cha kutengeneza tambi cha Tanzania Pasta Industries Ltd, kilichoko Vingunguti.

Akiwa kiwandani hapo ametoa wito kwa wazazi kuhimiza watoto wao kusoma masomo ya sayansi ili viwanda vinavyoanzishwa nchini vipate rasilimali watu wazalendo badala ya kutegemea watumishi kutoka nje ya nchi.

Aidha ameagiza uongozi wa kiwanda hicho, kuandaa utaratibu mzuri wa kulipa fidia wananchi walio jirani na kiwanda hicho, ambao walitoa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wake katika eneo hilo kwa sababu ujirani mwema ni jambo muhimu kwa ustawi wa kiwanda.

Baada ya tukio hilo alitembelea barabara ya Segerea - Bonyokwa, ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami na baadaye alikagua soko la Kerezange na daraja la kivule ambalo linatishia usalama wa wananchi kutokana na kuchakaa kwake.

Kwenye daraja la Segerea, ambalo lilianza kujengwa mwaka 2013 kwa mkataba wa kumalizika 2015, lakini mpaka sasa bado halikamilika, RC Makonda alitumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi ambao walimweleza kuwa kutokamilika kwa daraja hilo kunawasababishia usumbufu mkubwa.

Walisema Mkandarasi wa daraja hilo, ambaye anatoka kwenye Kampuni ya ujenzi ya Texas, Francis Musiba, amekuwa mzito kutekeleza majukumu yake hivyo kusababisha muda uliowekwa kumaliza ujenzi huo kupita.

Makonda alimhoji Mkandarasi huyo, sababu za kuchelewesha kukabidhi daraja hilo, ambapo alijitetea kuwa kuna sehemu inahitaji kubomolewa kwa kibali kutoka kwa Wakala wa Barabara (TANROADS), ambacho bado hawajapewa.

Alisema pamoja na hilo, daraja lenyewe mali ya TANROADS, limechelewa kukabidhiwa kwao hivyo walianza rasmi ujenzi Aprili mwaka huu, tofauti na inavyosemwa kuwa lilianza kujngwa miaka minne iliyopita.

Kutokana na majibu hayo, Makonda alimtaka Mwenyekiti wa mtaa huo, aeleze muda hasa ambao ujenzi wa daraja hilo ulianza ambapo alisema ni miaka minne iliyopita kama ilivyoelezwa na wananchi .

Naye Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonna Kaluwa, alisema aliwahi kuzuru kwenye daraja hilo zaidi ya mara tano, ambapo alikutana na Mkandarasi huyo na kumuahidi kukamilisha ujenzi huo siku zisizozidi nne.

“Nilikuja zaidi za mara tano, mara ya mwisho Mkandarasi huyu (Francis), aliniahidi kukamilisha siku zisizozidi nne mpaka sasa naona bado,” alisema Bonna.

TANROADS walipopewa nafasi ya kuelezea maendeleo ya daraja hilo walisema kibali cha kubomoa sehemu ya barabara inayohitajika ili kukamilisha ujenzi huo watakitoa ndani ya siku mbili, kwa sababu ombi wamelipokea jana kutoka kwa manispaa ya Ilala.

Makonda mara baada ya kusikiliza maelezo ya pande hizo, aliagiza Mkandarasi wa Wilaya ya Ilala, Ndango Masatu, kutoa wakaguzi wamsimamie mkandarasi wa kampuni hiyo mpaka atakapomaliza na kisha atume wataalamu kukagua ubora wa daraja hilo mara litakapokamilika.

Alimwonya mkandarasi huyo kuwa ndani ya siku 25, kama atakuwa hajakamilisha ujenzi huo, yeye na mtu aliyempa tenda hiyo watawajibishwa ikiwa ni pamoja na kukosa tenda zingine za ujenzi wa madaraja na barabara za mkoa wa Dar es Salaam.

“Endapo litakamilika lakini likawa na ubora wa viwango vya chini na ikathibitishwa na wataalamu wa halmashauri, wewe Mkandarasi hutapewa tenda yoyote mkoani kwangu labda uende mikoa mingine ambayo haijali wananchi wake, na pia mtapelekwa mahakamani wewe na aliyekupa tenda,” alisema RC Makonda.

Akiwa njiani kwenda Chanika kutakakofanyika mkutano wa hadhara Alasiri hii, alisimama kwenye kituo cha basi cha Mombasa na Gongo la Mboto na kuzungumza na wananchi ambako alitoa maelekezo kadhaa kwa makundi mbalimbali wakiwemo madereva bodaboda juu ya kutotumika kwenye matukio ya kihalifu pamoja na kupiga marufuku uuzaji wa matunda pembeni mwa barabara kwa sababu za kiafya.

Alimuagiza RPC wa Ilala kutoruhusu wafanyabiashara wa matunda kuuza bidhaa zao pembeni mwa barabara kwa sababu pia ni hatari kiusalama.
Pamoja na hilo, Makonda amefanya uzinduzi wa shule ya msingi Maghorofani iliyojengwa eneo la jeshi la wananchi kikosi cha 511 Gongo la Mboto, ambayo ni zao la fedha za Rais Dk. John Magufuli zilizolenga kutatua changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa Dar es Salaam.

Shule hiyo itachukua wanafunzi 1,500 huku ikiwa na maabara ya kisasa ya kompyuta.

Kesho RC Makonda ataendelea na ziara hiyo ya siku 10, katika manispaa ya Kinondoni.
d907a311811d3ec0b932ce9c26ed563d.jpg
View attachment 439033
Bi Chiku Said akiwa chini ya ulinzi

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kuuza viwanja vya serikali kinyume na sheria bila kuwahusisha wajumbe wenzake hali ambayo imesababisha mgogoro mkubwa wa ardhi katika eneo hilo.

Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa huyo kumtaka Afisa Ardhi wa Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela kuthibitishwa kuuzwa kwa eneo hilo kinyume na sheria.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa, ni kweli tulikuwa na eneo Block J lakini limeuzwa,” alisema afisa huyo “Nataka kuwaambia kitu mwenyeviti wa mtaa hawaruhusiwi kuuza eneo katika mtaa. Mimi ningewataka wenyekiti kufuata taratibu za kisheria zilizowekwa ili kuepuka kutokea kwa hayo mambo,”

Baada ya kauli hizo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

November 26 2016 ziara ya Dar Mpya ilikuwa Ubungo ambapo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alitembelea kampasi ya chuo na hospitali ya taaluma na tiba ya chuo kikuu cha afya na sayanzi shirikishi, Muhimbili iliyoko Mloganzila, wakati akiondoka eneo hilo wananchi walisimama barabarani kuzuia msafara wakidai kutopewa fidia baada ya nyumba zao kubomolewa kupisha mradi huo.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole aliwaambia wananchi hao kuwa suala lao linashughulikiwa na wengi wao ameshaonana nao akawambia wakalete taarifa za ziada ili awatafutie msaada wa kisheria ila hawakurudi hivyo DC polepole akawaomba wafuate utaratibu.

Aidha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alisimama na kuwaambia ni marufuku kwa yeyote kuzuia msafara kwa kuwa hakuna kero itakayotatuliwa kwa kuzuia msafara hivyo wafuate walichoambiwa na Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anaendelea na ziara yake mkoani humo ambapo leo ameianza wilaya ya Kinondoni, huku akiwaogusa watumishi wa umma aliodai wanatumia hirizi.

Akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya hiyo, Makonda alisema kuwa anafahamu wapo wanaoshinda kwa waganga na wanaotumia hirizi ili kujikinga wasitumbuliwe.

“Kuna baadhi ya watumishi wanatembea na hirizi ili wasitumbuliwe, wakikutana na viongozi wao wanazibinya,” alisema Makonda. “Mimi ninachokitaka kutoka kwenu ni kuwatumikia wananchi wa chini,” aliongeza.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo, Ally Hapi aliwaambia watumishi hao kuwa atahakikisha anawashughulikia watendaji ambao hawawajibiki ipasavyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wao

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam anaendelea na ziara yake katika wilaya za mkoa huo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Chanzo: Dar24
Kwa siku tisa sasa makonda anafanya ziara ya kuwasikiliza wananchi kaibua kero nyingi lakini sioni mawaziri husika na taasisi za serikali kama wanatoa ushirikiano. Mama mmoja amekiri kuuza eneo la shule lililotolewa na mwananchi hakuna kauli yeyote kutoka kwa waziri wa elimu wala tamisemi.

wajumbe wamelalamika kutopewa miongozo ya utendaji kazi hakuna kauli iliyotolewa na waziri wa tamisemi juu ya ukweli wa jambo hilo. mwenyekiti amekiri kuchangisha fedha na hazijulikani ziliko wananchi wamekuwa wakitozwa 10% ya mauzo ya mali zao na wenyeviti wa mitaa na fedha hazijulikani ziliko mpaka sasa takukuru wako kimya.

Makonda kashauri eneo la uwanja wa fisi panapaswa kuendelezwa, nategemea lukuvi na simbachawene walitolee ufafanuzi hili, nategemea nhc nssf ppf waje na proposal ya namna ya kuliendeleza hili eneo la uwanja wa fisi, haiwezekani tuweke breeding centre ya wahalifu katikati ya mji, hili eneo ni prime kibiashara kama hamuwezi kuliendeleza waiteni wawekezaji, hapa ukimpatia yusuf manji au bhakressa atachekelea mno.

Wapo wananchi wanalalamika kudhulumiwa fidia, nategemea takukuru walifanyie kazi na sio wazo la kijinga la kutaka waende mahakamani, ni kazi ya serikali kutetea wanyonge, hawa wananchi wanaohangaika kupata mlo wakapoteze muda mahakamani tena.

Makonda kaonyeshwa madanguro tena akiwa na sirro mwenyewe nategemea kusikia kauli ya waziri mwenye dhamana analifanyia nini hili tatizo la madanguro ya uwanja wa fisi.

Nategemea ziara ya pili ya makonda itakuwa ya kupeleka majibu ya kero alizoziona kwa wananchi na nategemea ataambatana na mawaziri husika. Huo ndio utawala bora.



 
Makonda amesema yeye ataongea na idara zake katika kutaka kuleta ufumbuzi wa changamoto za Dar Es Salaam!
sisi wote tukiwa na shida lazima tutareport ktk idara zilizopo chini yake!
lakini pia sisi ni wakazi wa Dar Es Salaam ambao hayo yote anayoyataka makonda ni nafuu kwetu!
kama ukiibiwa hutotaka msaada wa polisi?
Je huitaji maji?
je, huitaji jiji lililo safi!
wabongo jaribuni kuwa sehemu ya ufumbuzi na msipende sana zogo!
Ni aibu kumbeza makonda aliyekuwa hata na some idea za kuboresha jiji!
tupo wakazi mil 5, huyu mmoja kaamka na idea ambayo tukiifanyia kazi pamoja inaweza kuleta tija, yet wengine mnabeza!
kwanza inawezekana huna mchango wowote hata nyumbani kwako, sembuse huu wa jiji!
 
Aache siasa za sifa. Sio rais kasema kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tufanye usafi yeye anakuja na lake ati jumamosi zote tufanye usafi hakuna kazi.
Tunatakiwa wafanya biashara tumgomee huyu masifa asie ona mbali.
Watu tunataka tufanye kazi yeye funga maduka jumamosi.
Kwa si uhimize tu sehemu za biashara ziwe safi ?
Huyu hafai kabisa
 
bado wapo wakazi wa Dar wanaosapoti hii movement!
hili la kubeza lisimkatishe tamaa!
wapo hata wanaombeza bwana Mungu wao, sembuse Makonda!
Nadhani anatakiwa awe focused, tupo baadhi ya wana Dar tutakuwa naye pamoja! atupe tu roles za sisi kuwa sehemu ya mchango ktk utatuzi wa baadhi ya kero za jiji letu pendwa!
 
bado wapo wakazi wa Dar wanaosapoti hii movement!
hili la kubeza lisimkatishe tamaa!
wapo hata wanaombeza bwana Mungu wao, sembuse Makonda!
Nadhani anatakiwa awe focused, tupo baadhi ya wana Dar tutakuwa naye pamoja! atupe tu roles za sisi kuwa sehemu ya mchango ktk utatuzi wa baadhi ya kero za jiji letu pendwa!
Mnatumia utaratibu gani kuwachunguza maafisa uliowatuhumu? Kwanini wasisimamishwe kazi kupisha uchunguzi? Hii ni double standard kwa watumishi wa umma
 
Aache siasa za sifa. Sio rais kasema kila jumamosi ya mwisho wa mwezi tufanye usafi yeye anakuja na lake ati jumamosi zote tufanye usafi hakuna kazi.
Tunatakiwa wafanya biashara tumgomee huyu masifa asie ona mbali.
Watu tunataka tufanye kazi yeye funga maduka jumamosi.
Kwa si uhimize tu sehemu za biashara ziwe safi ?
Huyu hafai kabisa
Hili ni tatizo, then deal n case kwa case!
mimi pia simuungi mkono kwa watu kuacha kufanya kazi kila jmosi, alitakiwa apange team yake ifanye ukaguzi kila jmosi na wadeal na wale watakaokuwa wachafu! wengine wamesafisha lini, saa ngapi it doesn't matter cha msingi wakati wa inspection hiyo jmosi wanapaswa wawe wasafi!
 
Mnatumia utaratibu gani kuwachunguza maafisa uliowatuhumu? Kwanini wasisimamishwe kazi kupisha uchunguzi? Hii ni double standard kwa watumishi wa umma
si kila tuhuma mtu anasimamishwa kazi!
kuna saa wazembe wanaitwa tu kwa board!
kuna saa wazembe wanasetiwa targets na kuwekewa wasimamizi!
kuna saa wazembe wanahamishwa vitengo!
kuna wakati wazembe wanaondolewa some priviledges!
kuna saa wazembe wanapewa adhabu!
kuna kipindi wazembe wanasimamishwa kupisha uchunguzi!
kuna kipindi wazembe wanapelekwa mahakamani straight na jamhuri inafanya upelelezi!
kuna kipindi wazembe wanafutwa kazi on spot!
ndugu yangu ukizembea kazini kuna factors kadhaa hutazamwa kabla ya kuamua!

anyway, kuna maneno makonda anakosea ktk operations zake, mojawapo ni hili la kutaka kuboresha vitu huku akiwaponda wenzake! sidhani kama mtu mmoja anaweza kupush kila kitu, hata Yesu au Muhammad hawakuweza walikuwa na lundo la watu pembeni yao wakiwa na majina tofauti lkn technically walikuwa wakiwasaidia kufanya kazi za Mungu!
Hili la kuchanganya Dar Mpya na maneno kuwa kuna idara zinazembea, naomba tulipuuze! ndio yale mapungufu ya Makonda tuliyoyasema hasa anapojitia anavaa kofia ya kisiasa/utumishi kama kiongozi mwakilishi wa raisi/chama tawala!
 
Aache matamko ya kisiasa yenye kulenga cheap popularity bila kujali implications za kisheria! Jana katamka hadharani kuwa kuna wafanya biashara 4 wa shisha walimwendea ofisini kutaka kumhonga @million 5 ili kumziba mdomo akazikataa! Akatuhumu kwamba pengine PRC na jeshi lake huenda wamepokea hizo millions, akatuhumu na hata DCs kwa mtindo huo huo! Tunajua kuwa rushwa ni kosa la jinai kwa anayetoa na kwa anayepokea! Kama serikali ya awamu hii ingekuwa na nia ya dhati kweli kupambana na rushwa, saa hizi Makonda angepaswa awe anaisaidia TAKUKURU kuwatambua hao wahalifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa! Cha ajabu PM naye akachukulia kana kwamba hamna tuhumu za jinai zimetolewa hadharani!
 
bado wapo wakazi wa Dar wanaosapoti hii movement!
hili la kubeza lisimkatishe tamaa!
wapo hata wanaombeza bwana Mungu wao, sembuse Makonda!
Nadhani anatakiwa awe focused, tupo baadhi ya wana Dar tutakuwa naye pamoja! atupe tu roles za sisi kuwa sehemu ya mchango ktk utatuzi wa baadhi ya kero za jiji letu pendwa!

mnatafuta kick za kishamba tu, waalimu wanasafiri bure? Anakuja na mipango hewa ili aonekane ni mbunifu? Yeye abaki kuwadanganya hao wazee wanaompa vyeo kwa kushitakia wengine mambo ya kikuda.
 
si kila tuhuma mtu anasimamishwa kazi!
kuna saa wazembe wanaitwa tu kwa board!
kuna saa wazembe wanasetiwa targets na kuwekewa wasimamizi!
kuna saa wazembe wanahamishwa vitengo!
kuna wakati wazembe wanaondolewa some priviledges!
kuna saa wazembe wanapewa adhabu!
kuna kipindi wazembe wanasimamishwa kupisha uchunguzi!
kuna kipindi wazembe wanapelekwa mahakamani straight na jamhuri inafanya upelelezi!
kuna kipindi wazembe wanafutwa kazi on spot!
ndugu yangu ukizembea kazini kuna factors kadhaa hutazamwa kabla ya kuamua!

anyway, kuna maneno makonda anakosea ktk operations zake, mojawapo ni hili la kutaka kuboresha vitu huku akiwaponda wenzake! sidhani kama mtu mmoja anaweza kupush kila kitu, hata Yesu au Muhammad hawakuweza walikuwa na lundo la watu pembeni yao wakiwa na majina tofauti lkn technically walikuwa wakiwasaidia kufanya kazi za Mungu!
Hili la kuchanganya Dar Mpya na maneno kuwa kuna idara zinazembea, naomba tulipuuze! ndio yale mapungufu ya Makonda tuliyoyasema hasa anapojitia anavaa kofia ya kisiasa/utumishi kama kiongozi mwakilishi wa raisi/chama tawala!
Kumbe?? Waliotumbuliwa hadharani walipewa nafasi ya kujitetea? Au walisakamwa mpaka wengine mauti yaliwakuta wakiwa kwenye suspension.?????
 
Kumbe?? Waliotumbuliwa hadharani walipewa nafasi ya kujitetea? Au walisakamwa mpaka wengine mauti yaliwakuta wakiwa kwenye suspension.?????
Kila kesi na hukumu yake!
lakini makonda hakuwahi kumtumbua mtu barabarani ktk kumbukumbu zangu!
ila hiyo topic sio sehemu ya Dar Mpya, labda magu akija na tz mpya umuulizie kuhusu utumbuaji!
 
mnatafuta kick za kishamba tu, waalimu wanasafiri bure? Anakuja na mipango hewa ili aonekane ni mbunifu? Yeye abaki kuwadanganya hao wazee wanaompa vyeo kwa kushitakia wengine mambo ya kikuda.
Hili wazo anauza kwa wana Dar, sasa hewa au sio hewa hapo tutazame reaction ya wananchi!
wewe just play your part!
huu ni mpango shirikishi, makonda yeye ni kama captain ktk team, ushindi unawahusu hata wachezaji wa reserve, si huwa unaona ktk soccer medal wanavaa wote hata wasiocheza, sio captain peke yake!
njoo uwekeze ktk Dar Mpya, acha porojo!
 
Hili wazo anauza kwa wana Dar, sasa hewa au sio hewa hapo tutazame reaction ya wananchi!
wewe just play your part!
huu ni mpango shirikishi, makonda yeye ni kama captain ktk team, ushindi unawahusu hata wachezaji wa reserve, si huwa unaona ktk soccer medal wanavaa wote hata wasiocheza, sio captain peke yake!
njoo uwekeze ktk Dar Mpya, acha porojo!

wazo lake lipi lenye tija mpaka sasa? acheni hizo.
 
wazo lake lipi lenye tija mpaka sasa? acheni hizo.
Ngoja nikupe hili moja toka ktk Dar mpya!
" Nataka kujenga (kumobilize resources kwa ujenzi wa..) kituo cha size ya kati vya polisi 20 ktk jiji la Dar Es Salaam".... anaendelea, unajua ukitokea kipawa hadi Chanika eneo lote lile lina kituo kikubwa kimoja tu cha polisi Stakishari... vingine ni vidogo mno ambavyo tunaviita polisi post, vyenyewe huwa na askari wawili au watatu ambao hawawezi kutoka pale wananchi wanapopata tatizo kwa kuwa hawawezi kuacha kituo wazi!"....
vituo vya ukubwa wa kati vitakuwa na askari hadi 200 kwa ajili ya kusupport tarafa/wilaya.

ajenge au asijenge.... kuliona tu hili tatizo ni jambo la msingi sana kwa kiongozi wa jiji husika!
unaweza kumchukia mtu kwa kadri unavyopenda, ila kama ameleta idea nzuri ni wajibu wetu kusifia na kulifanyia kazi hilo wazo!
 
inauma sana kwa mfumo wetu. wananchi wa dar walichagua ukawa mwaka jana, lakini matokeo yake wameteuliwa watu kuja kuwaongoza wana dar kwa kila kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom