Haya sasa, nani mkweli na nani anaihujumu Tanzania kati ya ADB na IMF?

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Mpaka sasa inaonekana kunahujuma ilipangwa na IMF kuihujumu Tanzania dhidi ya takwimu za kiuchumi,

Naipongeza serikali kwa kushitukia mchezo huo mchafu,kwa kutoichapisha ripoti hiyo,IMF walitaka tujikaange kwa mafuta yetu wenyewe.

Hili limethibishwa leo ikulu na kiongozi mwandamizi kabisa wa bank ya ADB ,amesema uchumi wetu unakua vizuri na unatarajiwa kukua vizuri kwa asilimia 6 mpaka 7.

Nzuri zaidi ni mwafrika mwenzetu.

Nategemea Zitto ajitokeze na kundi lake kumpinga kiongozi huyu mbobezi wa masuala ya kiuchumi .

Mwisho, ni nani wako nyuma ya hujuma hii dhidi ya nchi yetu?,na nini lengo lao?
 
a beautiful lie kills, whilst an ugly truth heals.
 
Zitto na mabeberu wanahujumu nchi yetu. TZ ishirikiane na ADB tuachane na IMF.
 
Numbers don't lie!!! Hatutaki maendeleo ya tarakimu tunataka maendeleo yanayoonekana. Uchumi ukikua hata kwa .00001 tutauona, tutausikia mshindo wake. IMF iseme uongo, iseme kweli tutayaona sisi wenyewe. Muda ndio mwalimu wetu. Labda kutokee muujiza na wte tutauona kwa macho yetu wala hatutaambiwa kuwa huu muujiza ndo umetuinua au umetuangusha. Acheni utetezi wa maneno
 
Fanyakazi mkuu utayaona maendeleo usishinde humu tu JF na kubaki kulalamika tu! Hapa Kazi Tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…