Haya niya kweli kuhusu Vodacom?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya niya kweli kuhusu Vodacom??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark City, Apr 16, 2010.

 1. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwa siku ya pili leo, nimetembelea duka moja ambalo liko njia ya kuelekea nyumbani. Ni duka kubwa kidogo na wanauza vitu vingi. Jana niliomba waniuzie vocha ya Vodacom ya shs 5000 lakini hawakuwa nayo. Leo pia nilipoulizia hiyo vocha haikuwepo. Ndipo muuza duka akaamua kuniambia kuwa hawawezi kuuza aina hiyo ya vocha kwa sababu hazina wateja. Aliendelea kueleza kuwa vocha kubwa za voda walizonazo ni za shs 3000 na hazitoki kirahisi. Na kwamba Vodacom inapitwa na hata TTCL na Zantel (na hapa ni Tz bara). Kwa kadri ya maelezo ya huyo jamaa, kampuni inayoongoza ni Tigo ikifuatiwa na Zain.

  Nilishangaa kiasi kwani sikutegemea kusikia kwamba Voda imefulia kiasi hicho. Ukizingatia majigambo yao yote na taarifa aliyotoa Mwamvua Makamba leo, kwamba Voda ndiyo yenye bei nafuu kuliko kampuni zote nchini. Hii kitu nilichokutana nacho ni hali halisi au ni tatizo la hapa mtaani kwetu?
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Usishangae, kulikuwa na thread hapa JF ya kuhamasisha wanatumiaji wa simu wasusie kampuni ya Vodacom kwa sababu ina element za ufisadi.

  Labda ile kampeni imejibu, ukizingatia kuwa Vodacom ni expensive ukilinganisha na makampuni mengine ya simu.
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ukweli halisi voda haina subscriberz wengi kuliko tiGO au kama inavyotaka wasikilizaji na wasoma matangazo kuamini. Na voda wanalitambua sana hilo na wana mbinu kamambe za kuhadaa mamlaka husika zikubaliane na takwimu mfu. Mfano inachukua siku 120 kwa database ya voda kutambua na kuondoa inactive sim card wkt zain na tiGO wanatumia siku 90 na 60 respectively. Hapa utagundua kuwa kwa mteja aliachana na voda kwa sbb yoyote, voda wataendelea kumwesabu na kujiridhisha kwamba bado wanae. Na pia watahadaa halaiki kwa takwimu zilizopitwa na wakati.
   
 4. m

  mimi-soso Senior Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mmmh
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Apr 17, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  Dark city afadhali umeuliza na haujatoa conclusion voda ina wateja wengi kwa sababu nyingi

  1. Kampuni ya zamani wengi wanahitaji ku-retain namba zao
  2. wateja wengi wengi wa Vodacom na hasa makampuni hayahitaji vocha, wanalipia kwa mwezi na haya yako mengi na tangu siku nyingi.

  Kutokana na ushindani na kuwa na namba zaidi ya moja ni rahisi ku-draw conclusion unayoisema , lakini kuna tafiti nyingi zikiwamo mpaka za saikolojia ya rangi! vodacom na tigo are likely kwenda mbali kwa saikolojia ya rangi ya bluu!! haya sio maneno yangu mkuu, I once worked there na watafiti wao walilisema sana hili na hata Logo ya kwanza ilipobadilishwa walipunguza sana kijani, na kuna logo zingine huoni kabisa kijani. People tend to like blue colour than others!!1 LOL!

  Ukija kwenye halisia( ukiuliza bado voda ina wateja wengi sana kuliko makampuni yote , issue ni how active are they? maana kama kwa conlusion hiyo, makampuni yote ya simu bongo hayana wateja wa kununua vocha wa kudumu kwa sababu watu ni dynamic, they seek opportnity from any company........

  Tigo staff ukiwauliza ni kweli kuwa mitambo yao inafurika sana kunapokuwa na promotion na wanapungua remakarbly promotion inavyoisha.

  I love this trend ila kuna wengine wana chuki za kijinga na vodacom ambazo haziwasaidii lets enjoy this competition na free market, kuwa ni kampuni ya kifisadi ilo tunalijua JF!! believe me! huko uraiani no one cares! na hata tukijua bado hatujafika hiyo level ya kususia vitu vya mafisadi. Kama ni hivyo we will need kususia daladala zote za mafisadi na nyumba za kupanga tunazoishi zilizojengwa na mafisadi!!!

  I simply love the level of competition in telecom. However, I must congratulate Tigo to break all barriers and done wondeful to stimulate competition
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  sidhani kama haya yana ukweli Dark City labda maeneo ya kwenu tu
   
 7. S

  Subira Senior Member

  #7
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  inategemea uko mtaa gani na ni watu wa level ipi unaoishi nao, ukienda sehemu zingine ni zentel kwa kwenda mbele huko dar ni tigo kwa sana arusha vodacom zaidi na zaini hivyo you cant analyse kwa njia hiyo, ila maneno ya huyo makamba ni ya uzushi kwani tigo sasa hivi ni kwa thumuni na ukicompare na one shiling anasema uongo, na zaini ni sawa na wao one shilling hivyo bado compt iko juu ila research halisi bado ili tuconclude
   
 8. Mama Nim

  Mama Nim Senior Member

  #8
  Apr 17, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vodacom bado gharama zake ziko juu. Wakitaka watu watmie mtandao wao basi waruhusu watu wapige sime bure. Imeshajengeka vichwani vya Watanzana kwamba Vodacom na Zain gharama zao ziko juu kinachowasaidia ni kuenea kwa mitandao yao. Unakuta maeneo mengine ni mtandao wa Vodacom au Zain ndio unapatikana kwa hiyo wakazi wa maeneo hayo hawana jinsi bali kuitumia mitandao hiyo.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkuu analysis yako ya kutumia ununuaji wa vocha wala si sahihi. voda bado customers kibao. kwanza kuna postpaid wanalipa kwa bill, makampuni kibao yapo kwenye mkataba. kuna vodajaza hawa wanalipiwa na makampuni yao kutokana na wadhifa wa mtu. mfano meneja anawekewa credit ya laki moja kwa mwezi, labda wafanyakazi wa ngazi nyingine kwa mwezi wanawekewa alfu 80 kwa mwezi na kampuni inailipa voda. kuna bundles mtu ananunua minutes labda minutes 300. mkuu dark city technolojia ya sasa si analogue, ishapitwa na wakati, vilevile kukwangua ma voucher nako kunapitwa na wakati, kwa mtindo huo kuna vodafasta mkuu, lengo la kampuni ni kuondokana na physical recharge na kubase zaidi na electronic recharge ndo maana ya vodafasta.kaka kuna mpesa. katika menu ya mpesa unaweza kununua credit kuingiza kwenye akaunti yako, ukamtumia mtu pesa, ukalipia dawasco na tanesco. atm recharge za nmb, nbc zote hizi unaingiza credit kwenye simu. sasa means zote hizi baba why bother scratching voucher? hawa hawa wenye vibanda ndo walikuwa wanaongeza bei za voucher? ya buku 5 utauziwa buku 5 na mia tano. kitu kingine jamani mfahamu voda hawategemei kupiga simu tu, kuna data pale subscribers kibao, kuna wimax pale sijui km mnaifahamu wadau kuna yale mabenki sijui yana atm zao zinaitwa umoja, connection yote pale ni wimax, very speed na bandwith yake ni ya kufa mtu, nbc, barclays km sijakosea na makampuni mengi tu yatakuja, yote hiyo ni wimax. just a tip mkataba wa bank moja kwa mwezi thamani yake yafikia milioni 500. haya kaeni chonjo soon mtaanza kulipwa mishahara yenu kupitia mpesa hiyo yaja, ni suala la marketing tu, wala msiogope technolojia hiyo mwajiri wako akikubali utakuwa kwenye karne mpya. subscriber base inaongezeka daily sababu ya mpesa, pita vodashops angalia ile misululu ya watu wanaochukua na kuweka mpesa, kuna jamaa alilalamika sana humu eti kachajiwa elfu saba kutoa pesa, hiyo ni option mazee, km unapanda ndege kwenda mwanza kwa laki 2 wakati kuna basi la elfu 50 sijui, ni uchaguzi wako tu. jaribuni kuangalia product and services kampuni inazo offer kuliko kuangalia voice peke yake. na hiyo tigo ni dar tu huko mikoani utalia na kusaga meno.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Dogo yupo huko, naona kamwaga data za kufa mtu. nilimpa hii topic aisome akapandwa na mzuka akaamua achane vibaya mno
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana Mkuu wangu. Nikuhakikishie kuwa nimeelimika sana.
   
 12. shiumiti

  shiumiti JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2010
  Joined: Jun 4, 2009
  Messages: 438
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nasikitika sana kusema mtandao wa Tigo kwa kweli unazidiwa sana, ukiingia kwenye majengo marefu na yenye msongamano watu, mtandao unakuwa wa shida sana kupatikana. Na ukiwa unaongea kwa muda mrefu utashangaa ghafla unakata... Nime-experience hii kwa siku kadhaa sasa..

  Naomba sana wahusika wa TIGO walifanyie kazi hili..
   
Loading...