mabadiliko4015
Member
- Oct 14, 2015
- 6
- 12
Habari za jumapili wadau, ni matumaini yangu mko poa nyote, to cut the long story short ni ivi, miaka miwili nyuma nilitokea kumpenda msichana mmoja mrembo sana, alikua ni msichana wa kisasa nikimaanisha alikua anapelekwa na matukio ya dunia kuparty sana, kunywa pombe,kuvaa mini skirts n.k lakini mbali na mapungufu yote hayo nilimpenda, kasheshe likaja kwenda kumtambulisha kwa wazazi, walimkataa baada ya kumuona, nililia sanaa maana G alikuwa ameuteka moyo wangu na sikuweza kumuona mwanamke mwingine kabisa.
Nikafanya ivi, niliwapuuzia wazazi wangu nikamuoa kwa nguvu, siku ya harusi Mama yangu alinipigia simu na kuniasa nisienda kufunga pingu za maisha kwani ndo utakua mwisho wa maisha yangu, nilipuuzia nikamuoa G
Wazazi walikua hawaji kutusalimia, Japo maisha yetu na G yalikuwa matamu sana, nilianza kumbadilisha G, niliacha kunywa pombe na yeye baada ya muda akaacha baada ya kukosa kampani ya ulevi, nilikua nikimnunulia nguo za heshima, automatically akaachana na zile nguo zake za kutembea nusu utupu.
Sasa ivi niko kwenye process ya kumpatanisha na familia yangu waweze kumpenda.
Kuna muda huwa nawaza haya mahusiano yasio na baraka za Mungu wangu wa pili (wazazi) yatatoboa kweli?. Kiukweli nampenda sana G licha ya mapungufu yake mengi.
Ivi huu ni ukosefu wa akili au niko sawa?