Haya ni mapenzi au kujidhalilisha!!

Haya ni mapenzi au kujidhalilisha!!

He he he he, hii taarabu naipenda
Kwa mfuga Mbwa inapigwa mwamnzo mwisho

Kanikumbusha kuna jirani baba mzima aliwahi shushuliwa sina hamu

aliambiwa na binti karibia kwa kumzaa "mtu mzima ushahidi" Aliondoka kainamisha kichwa
Baba yangu akamwambia, wewe utaingiliaje mambo ya familia za watu

Huwa sitaki ushahidi kwenye familia za watu
Jina la taarabu ni lipi?
 
Mgawanyo wa kazi mkuu, hujui mama anakazi zipi ngumu ambazo mumewe ameshindwa kuzifanya.
So hayo ya Ngoswe mwachie Ngoswe mwenyewe!

Very good point. Ningekupa like, ila natumia simu ya mchina kuperuzi mtandao
 
Kwani huyu baba amelalamika? si ndicho walichokubaliana na mwenzi wake?
 
Nenda kamsaidie

  • :target:

mwashangaa nini??na hayondio matunda ya BEJING.mwacheni kaka wa Mwenzenu achakalika hayo ndio maisha bora kwa WOTE huyo ni wakupewa pongezi wakipatikana 10 kama hao swafi sana MAISHA NI KUCHAGUA sio kuchaguliwa
 
Tuna tatizo kubwa, baadhi yetu, katika kuangalia mambo na kuyaelewa. Uhusiano wa kimapenzi una mapana na marefu yake; maana halisi ya mapenzi inatofautiana sana baina ya jozi za wapendanao; na mambo gani yanawafanya wapenzi wawe kwenye mapenzi yanatofautiana sana.

Tofauti hii ya mitazamo ndiyo huwa inaleta kutokuelewana baina ya watu; wazazi na wakwe zao; madada na wifi zao; makaka na shemeji zao; majirani, ndugu na jamaa kama mleta mada hii.

Yote haya yanatokea kwa sababu tunajaribu kufananisha mapenzi yetu sisi wawili, na yale ya wengine...kwa kufanya hivi, ni sawa na kuona mke wako ni mzuri kuliko wa wengine...ilhali unajua kabisa vionjo vyako si lazima viwe sawa na vya wengine, na kwamba mkeo hata kama ni mzuri namna gani, huo ni uzuri unaokufaa wewe tu. Sana Sana wengine wanaweza kuona ni mzuri kwa kazi fulani tu, na kwamba baada ya hapo ataendelea kukufaa wewe mwenyewe.

Kwa sababu niliziainisha hapo juu, ni vigumu sana kuyaelewa mapenzi ya huyo bwana anayeelezewa kwenye mada hii. Sana sana wengi wetu tutaishia kumkashifu tu; jambo ambalo halitakuwa sahihi. Mipango ya ndani ya nyumba, haifanani, na kama ni shughuli za ndani, hizi ni "socially learnt activities" ambazo hubadilika from time to time, na kutegemea mazingira halisi.

Wakati Tanzania ni nadra sana, na huwa gumzo anapoonekana mwanamama anaendesha lori, nchi kama Ubelgiji, Japan, Uholanzi nimeona wanawake wanaendesha trucks na ni jambo la kawaida. Kwa mtoa mada, pengine itaonekana hii ni kazi ya kiume na hawapaswi kufanya hivyo?

Masuala ya kazi sasa hivi hayafuati sana jinsia...yanabadilika haraka kutokana na hali halisi. Kwetu, Tanzania, kwa sababu ya society sensitivity ndiyo maana maendeleo katika eneo hili yanachelewa sana. Hawa akina dada wanaojiuza, kwa mfano, kwa sababu hawaoni cha kufanya zaidi ya hicho, wangeweza kuwa drivers kwenye taasisi nyingi tu...na masiaha yangekuwa bora zaidi. Taasisi nyingi za UN zinahimiza akina mama drivers.

Tubadilike. Sidhani kama tuna taarifa muhimu za kutosha kujadili anayoyafanya huyo jirani yako. Tutakuwa tunapoteza muda tu kwenye jambo tusilolijua. Mapenzi yana siri sana ndugu zangu, hayaishii kufuliana na kushikana mikono tu hadharani. Na, kama haikudhuru wewe, na hakuna sheria zinazovunjwa, na hasa kama mkewe ameridhia, na wanawe, ni vema tumuache. Vinginevyo, tutaonekana kama tunamuonea wivu huyo mama...
 
pole yake jamani na kama ni dawa itafikia kipindi itaisha 2 nawe ucwe na wasiwasi kila ki2 kitaenda sawa 1 day ma dear
 
Mambo ya mtu na mke wake yanakuhusu nini.
 
Mtafutie kazi
Shughulika na maisha yako, achana na ya wengine

Inanikera na leo imenikera zaidi hadi nasikia kukereketwa kooni! Jamani hapa ninapoishi kuna jirani ambaye ni baba mwenye familia ya mke na watoto wanne. Kati ya watoto hao mmoja wa kufikia ni wa kike ambaye amehitimu elimu ya msingi, na wa kiume yupo darasa la sita wakati hawa wengine wawili ni wadogo.
Huyu bwana akiwa nyumbani anafanya kazi zote kama mke/mdada wa kazi ikiwa ni pamoja na kupiga deki, kuosha vyombo, kupika, na kufua nguo zote hadi nguo za ndani za mke wake na matambala anayotumia akiwa katika siku zake (hii ni kweli kabisa) na mbaya zaidi kazi hizi huzifanyia nje kweupe kabisa na akina mama majirani wakiwa wanamwangalia ikiwa ni pamoja na hao watoto wake wote !! Sasa kitu ambacho kimeniudhi leo ni kuona anafua suruali na nguo zingine za huyo binti yake wakati yeye anacheza lede barabarani, binafsi najiuliza haya ndio mapenzi tunayostahili kuwaonesha/kuwafanyia watoto na wake zetu? Na Je, nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kuwa anayofanya ni kujidhalilisha? Kwani imefika sasa watoto wanamuona kama mhudumu tu hapo nyumbani. Naombeni ushauri wemu kwani mwanakwetu anatutia aibu.
 
aaah jamani lakini huyo baba amezidi.haya kama mleta topic ni mbea,lakini is too much.kusaidiana kupo na ni vizuri mume amsaidie mke,lakini kwa hii imepitiliza.

Yaelekea jamaa anapenda ndio maana halalamiki, na anazo sifa zote za kuwa house maid. Mleta topic we yako macho
 
Unalijua limbwata la Dubai wewe??

Lile likikolea unaaza kuweka kichupa juu ya meza, unaenda kazini afu unamwambia

Utakunywa hilo limbwata vijiko viwili mara 3, na anakunywa religiously

Hiyo kali! Haki ya nani!
 
Kwani huyu baba amelalamika? si ndicho walichokubaliana na mwenzi wake?

Nasikitika kusema amekubalishwa huyo, akili zikirudi kutoka huko zilikofichwa mwanamke ataipata habari yake. Bujibuji, angalia na wewe yasije yakakukuta huko kwa mijimama yako - nasikia huwa yanaloweka kinyama sehemu sehemu halafu kesho yake kinachanganywa kwenye chakula yako mzee! Utasahau na kwenu.
 
Inaelekea na wewe ni kati ya hao wakinamama wanaokuwa wakimwangalia ikizingatia umeweza hadi kuona aina ya nguo azofua matambala anayotumia akiwa katika siku zake.
Nakushauri USIMWANGALIE haitakukera tena.
 
Inanikera na leo imenikera zaidi hadi nasikia kukereketwa kooni! Jamani hapa ninapoishi kuna jirani ambaye ni baba mwenye familia ya mke na watoto wanne. Kati ya watoto hao mmoja wa kufikia ni wa kike ambaye amehitimu elimu ya msingi, na wa kiume yupo darasa la sita wakati hawa wengine wawili ni wadogo.
Huyu bwana akiwa nyumbani anafanya kazi zote kama mke/mdada wa kazi ikiwa ni pamoja na kupiga deki, kuosha vyombo, kupika, na kufua nguo zote hadi nguo za ndani za mke wake na matambala anayotumia akiwa katika siku zake (hii ni kweli kabisa) na mbaya zaidi kazi hizi huzifanyia nje kweupe kabisa na akina mama majirani wakiwa wanamwangalia ikiwa ni pamoja na hao watoto wake wote !! Sasa kitu ambacho kimeniudhi leo ni kuona anafua suruali na nguo zingine za huyo binti yake wakati yeye anacheza lede barabarani, binafsi najiuliza haya ndio mapenzi tunayostahili kuwaonesha/kuwafanyia watoto na wake zetu? Na Je, nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kuwa anayofanya ni kujidhalilisha? Kwani imefika sasa watoto wanamuona kama mhudumu tu hapo nyumbani. Naombeni ushauri wemu kwani mwanakwetu anatutia aibu.

namtafuta huyo MGANGA aliyetoa dozi ya LIMBWATA... kwi kwiiii kwiiiiiiiiiiiiiiiii
 
nampa pole sana huyo baba anataseka sana siyo hivi hivi hiyo ni limbwata . jalibu kumshauli aweze alimike.:target:
 
hii nakumbuka majirani zangu walisha sema sana ila huwa nafanyaga hasa weekend siwezi kujisikia vizuri niko ndani mke wangu anahangaika na mtoto wakati huo huo anapika na kazi nyingine zinamsubiri na nguo za kufua ziko ati kwakuwa ni mume niwe nimelala ndani tu. huwa nafua namsaidia kuosha vyombo kukuna nazi na wakati mwingine namlazimisha anipishe jikoni nipike. Si shurrutushwi na mtu ila namuonea huruma kwani na yeye ni binadamu wakatyi mwingine ikibidi napiga deki na kufagia nyumba
 
umbea tu unamsumbua fanya yako tena inawezekana unashindapo unaomba msaada ndo maana unachunguza kila analolifanya huyo baba, kaa kwako fanya kazi za kukuletea kipato, ukiwa busy hutapata muda wa kuchunguza ya watu.
 
Duuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!! hapa kuna jambo nyuma ya pazia
 
Back
Top Bottom