Haya ni madini gani?

Hapo kuna Quartz (Crystal clear) hayo meupe kabisa na pia kuna Amethyst (Ha yenye rangi ya zambarau) ambayo haijafikia kiwango chake

Huo mzigo ulionao hauna thamani, endelea kuchimba
Nashukuru Mkuu! So sifa ya High Quality ya hizo Quartz na Amethyst ni ipi?
Na inavyoonekana Size yake ni hiyo hiyo ndogo ndogo, je kwa hiyo High Quality yake huwa na size ile ile!?
 
Pia hata kama ni madogo yahifadhi kuna wakati wanatokeaga wateja, wananunua kwa kilo, japo watakupa fedha ya kula, cha msingi endelea kuchimba hapo hapo ulipo endelea kuchimba, utatoka mkuu,
Shukrani Mkuu!
 
Hayo ni white QUARTZ, Crystal shape. kama moja lina kuanzia nusu kilo ni biashara, kama jiwe moja lina kilo 1 bei ya mwaka 2012 wkt nayachimbaa ilikuwa tsh 20000, likiwa na kilo nyingi ndivyo na bei iazidi kuwa juu, ilimradi yawe clear kiasi kwamba unaweza kusoma gazeti ukiweka juu yake. Kama yako makubwa makubwa uniambie uko mkoa gani ili nikutafutie soko

Kilo moja 20,000? Hapana kiongozi fana thaman ndogo sana kuliko hiyo. Nimechimba sana hayo madude Gairo pale. Tani moja ilikuwa inauzwa laki 7. Tena hiyo gharama ni ya mwaka 2013.
 
Yakiiva vizuri yanakuwa kama yamechongwa. Yanang'aa sana. Maeneo uliyoyapata kutakuwa na madini ya almas japo si lazima.
Nimekusoma mkuu! Baadaye ntaweka picha ya hayo Madini mengine....then ntasikia toka kwako...
 
Kilo moja 20,000? Hapana kiongozi fana thaman ndogo sana kuliko hiyo. Nimechimba sana hayo madude Gairo pale. Tani moja ilikuwa inauzwa laki 7. Tena hiyo gharama ni ya mwaka 2013.
Hayo uliyouza laki 7 tani ni high capshon sio quartz clear, zikiwa clear na yenye ukubwa Wa kuanzia kilo moja bei inaanzia tsh 20000, Mimi Nina mgodi Wa guartz ya mapande(block) handeni. Capshon zake nilikuwa nauza 250000 kwa tani.
 
Ya aina hii

Kama ni ya aina hii basi hiyo itakuwa ni Amethyst, na ndio maana nilikwambia kwenye sample zako naona zipo Amethyst ambazo hazijakoza rangi yake ya dhambarau

Nimekusoma mkuu! Baadaye ntaweka picha ya hayo Madini mengine....then ntasikia toka kwako...

image.jpg
 
Ya aina hii
Ni tofauti na haya, yenyewe ni mawe size ya kokoto pia yanakua na ukubwa mpaka wa 1 kg..
Rangi ni Zambarau iloiva, sometimes inakua light purple n.k..

Soon ntaweka picha!
 
Yakiiva vizuri yanakuwa kama yamechongwa. Yanang'aa sana. Maeneo uliyoyapata kutakuwa na madini ya almas japo si lazima.

Almasi tena?, mbona hakuna uhusiano au kwa sababu hizo Quartz zinatoka kama zimechongoka?, Almas ni pure Carbon na hizo Quartz ni Silica na Oxygen
 
Kama ni ya aina hii basi hiyo itakuwa ni Amethyst, na ndio maana nilikwambia kwenye sample zako naona zipo Amethyst ambazo hazijakoza rangi yake ya dhambarau

View attachment 530912
Sure Mkuu! Nnayo kama hayo, hivyo hivyo, japo yangu mengine ni Makubwa, rangi na hiyo japo nyingine imekoza.
 
Ni tofauti na haya, yenyewe ni mawe size ya kokoto pia yanakua na ukubwa mpaka wa 1 kg..
Rangi ni Zambarau iloiva, sometimes inakua light purple n.k..

Soon ntaweka picha!
Ni Amethyst hizo, zikiwa nzuri zinauzika, unazitoa Tanga nini?
 
Hayo uliyouza laki 7 tani ni high capshon sio quartz clear, zikiwa clear na yenye ukubwa Wa kuanzia kilo moja bei inaanzia tsh 20000, Mimi Nina mgodi Wa guartz ya mapande(block) handeni. Capshon zake nilikuwa nauza 250000 kwa tani.

Ok huwenda.
 
IMG_20170626_130934.jpg
IMG_20170626_130950.jpg
IMG_20170626_130756.jpg
IMG_20170626_130558.jpg

Wakuu hii ndo aina nyingine ya Madini niliyonayo, na kwa Comments za wengi hapo juu, nadhani hii ndo Amethyst!
Nipo sahihi!???

..Nimeshindwa kuyaosha vizuri, nimetoa tu Vumbi na mengine niliyapasua kuona ndani kukoje!!
 
Back
Top Bottom