Filipo Lubua
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 339
- 578
Nyingine si ndoa, ni ndoano
Mengine si mapenzi, ni ushenzi
Pengine, ni wizi, ubezi, ubazazi
Yakache, ya siku chache yasikuchache
Mwingine si upendo, ni utando
Mengine si asali, ni ajali
Ni utweza, poteza, lemeza
Tulia, pana nia pana njia
Mengine si furaha, ni karaha
Mengine si utamu, ni udamu
Ni fweza, uweza, uoza
Jikubali, usikubali kukubali
Sidhani yatuliza, yanaliza
Sidhani ni mapendo, ni uvundo
Si uhondo, ni ugando, kimondo
Usilie, yakimbie ujitue
© Filipo Lubua
23 Feb. 2013
Mengine si mapenzi, ni ushenzi
Pengine, ni wizi, ubezi, ubazazi
Yakache, ya siku chache yasikuchache
Mwingine si upendo, ni utando
Mengine si asali, ni ajali
Ni utweza, poteza, lemeza
Tulia, pana nia pana njia
Mengine si furaha, ni karaha
Mengine si utamu, ni udamu
Ni fweza, uweza, uoza
Jikubali, usikubali kukubali
Sidhani yatuliza, yanaliza
Sidhani ni mapendo, ni uvundo
Si uhondo, ni ugando, kimondo
Usilie, yakimbie ujitue
© Filipo Lubua
23 Feb. 2013