Haya ndiyo yanayotukera sisi wanaume

Haya ndiyo yanayotukera sisi wanaume

The Retired Planner

Senior Member
Joined
Sep 22, 2015
Posts
166
Reaction score
242
Wasalaaaaam!


Ndugu zangu leo nimeona nianzishe huu uzi hapa ili pawe kama Centre maalumu ya kupumulia na kupata ushauri kwenye masuala ya mahusiano, ndoa na hata urafiki baina ya wanaume na wanawake.

Hii ni kutokana na mfumo tulionao sisi wanaume wa kushindwa mara nyingi kuongea yale yanayotukwaza kwa namna yoyote ile kwenye mahusiano, ndoa na hata urafiki. Na tathimini za kiafya pia zinaonesha wanaume wengi hufa kwa “stroke” kwa sababu ya kutunza mambo mengi ya siri ambayo hukutana nayo kwenye mahusiano na hivyo kupelekea umauti wao.

Kupitia forum hii, utapata mahali pa kuongelea yote hayo na kupata ushauri wa namna yoyote ile. Kupitia wanawake wenyewe au wanaume kwa ujumla wetu.

Karibuni Uwanjani sasa..................!

Ushauri wangu: Usipende kukaa na makwazo moyoni, unakaribisha kifo kwa haraka sana!
 
Demu wangu anapenda sana kuchati na marafiki zangu wa kiume..namkataza ila hasikii..
Siku moja mweke chini umuulize kama kweli anakupenda. Ila jiangalie labda na wewe huchati nae kwa sana kwahiyo anatafuta njia nyingine mbadala.
 
Back
Top Bottom