Uchaguzi 2020 Haya ndio yatakayoiangusha CCM kwenye uchaguzi 2020

Namba 9 ina nguvu kubwa sana ya kuimaliza sisiemu.
Hakuna mhitimu wa digrii ya Ualimu masomo ya Sanaa anafurahia kutokuajiriwa tangu 2015 alipohitimu Chuo Kikuu,hakuna!
Vijana hawa wamejiandikisha kupiga kura na wengine wameshachukua fomu kuwania nafasi za uwakilishi.Wataimaliza sisiemu mapema sana kuliko inavyotarajiwa...
kuna madogo walienda JKT wakiwa na matumain hat ya kuajiliwa hata upolisi, wakamaliza 3 years na miezi. na bado wakachukuliwa wachache kwa kigezo cha walienda kujitolea kujenga ukuta. its not fair.

licha ya elimu au kufundishwa ujasiriamali, bila ya mtaji ni kazi bure, ukiwaona wanavyosafa kitaa unawaza wangekua kitaa wangeendesha hata boda boda life lingesonga kuliko.....mi nawaza tu kwa sauti hivi mama, mjomba,kaka na ndugu wengine wanawaza nini kuhus govt?

kuna vijana wana TEN years kitaa na degree zao, ni afadhali wangeenda VETA tu wawe hata mafundi umeme wangekua mbali. licha ya yote hayo Bodi bado inawapa presha ya kuwadai na warudishe fedha za mikopo hata kama huna kazi(nasikia kuna tetesi juu ya hili sina uhakika) .
 
Sitaelezea kwa undani lakini pamoja na nguvu ya dola CCM wenyewe wanajua hali si shwari.

Zaidi sana kuna mambo ambayo hawajui yanafuta nyaso zao za mambo makubwa ambayo wameyafanya kwa Wananchi...
Bora itoke tuone wengine watafanya nn
 
JPM atapata 98%ya kura,hao machizi wengine wazee wa lockdown watagawana hiyo 2%.

Hiyo 98% atakayopata ni ya KUBEBWA NA TUME YA UCHAGUZI ISIYO HURU.
Kama tukiwa na TUME HURU itakuwa kinyume chake kwa Magufuli kuambulia hiyo 2%.....!!
 
Uchaguzi uliopita OCD na jeshi la polisi walisaidia chadema...

Ref; Lijuakali maelezo ya how tuliiba kura
Ukatili wao unafahamika na wananchi! Hata traffic police. Miye mwenyewe nnayo video clip, nilipigwa na traffic! Tena wakati anawatrain vijana ndani ya ofisi na mkuu wao akiwa ofisini.

Naikumbuka namba yake na walinitesa na kunitisha kuwa wanafahamiana na Siro! Maana nilenda hospital kupatiwa matibabu! Hii serikali ni ya kikatili sana kama rais hafahamu!
 
Tulishaambiwa tusipoichagua CCM maendeleo hatupati na la kuwa fanya hatuna.
 
Tulishaambiwa tusipoichagua CCM maendeleo hatupati na la kuwa fanya hatuna.

Hiyo ni contradicting story! Jiwe siku zote anajinasibu kwa kauli ya kipuuzi: MAENDELEO HAYANA CHAMA! Lakini kiuhalisia anasema CCM NDIYO INAWALETEA MAENDELEO WATZ......which in the real sense siyo kweli hata kidogo!
 
Sitaelezea kwa undani lakini pamoja na nguvu ya dola CCM wenyewe wanajua hali si shwari.

Zaidi sana kuna mambo ambayo hawajui yanafuta nyaso zao za mambo makubwa ambayo wameyafanya kwa wananchi..
Haya ni kweli kabisa Ila tatizo .Tume huru na magoli ya mikono
 
Hapo kwenye kukosa ajira hapo ndo penyewe,vijana walisoma ili wapate nafuu ya maisha viongizi wanatoa maneno ya rejareja kuhusu ajira
 
Namba 9 ina nguvu kubwa sana ya kuimaliza sisiemu.
Hakuna mhitimu wa digrii ya Ualimu masomo ya Sanaa anafurahia kutokuajiriwa tangu 2015 alipohitimu Chuo Kikuu,hakuna!
Vijana hawa wamejiandikisha kupiga kura na wengine wameshachukua fomu kuwania nafasi za uwakilishi.Wataimaliza sisiemu mapema sana kuliko inavyotarajiwa.
Jambo pekee linaloweza kuibadili nia yao walau kwa asilimia kadhaa ni kuwamwagia ajira si chini ya 60,000 (Sitini Elfu) ili 'kuwamonyoa' (*kuwamega) na kupunguza umoja wao lakini kama hali ndiyo hii.. .. .. haki ya baba, atajampa moto.
Hata Mimi Nina 4years Sina ajira. Hafu naambiwa kunaajira 6,000,000. Wakati hata temple tu ya ajira nilifukuzwa kwenye shirika flani hivi. Sasa ninayo ya moyoni yananiuma tu. Hakika lazima nipige kura mwaka huu. Siasa zina effect kubwa Sana katika maisha ya kila siku.
Muhimu ungefunguliwa uzi wa kuamasisha watu wakapige kura bila kujali watashinda kwa magoli ya mikono au mguu. Mana unaweza shindwa hafu ukaiba kura ili ushinde. Mana unaweza bebwa mwisho wa siku ukawa mzito na ukashindwa kubebeka.
Muhimu tuendelee kusisita watu kupiga kura. Bila kujali kama kura zitaibiwa au raha..
 
Kupoteza ndugu zetu kina Azory Gwanda, Ben Saanane ,Kanguye hatujasahau, kutumia pesa za nchi kununulia ndege , Kajenga uwanja wa chato bila idhini ya bunge.Kupora hela za mifuko ya hifadhi ya jamii.Kuipeleka n hi uchumi wa kati hewa.
Uchumi hewa huo...... labda niende chato nitauona uchumi wa kati.....

WAKULIMA hoi
WAFANYAKAZI hoi
WAFANYABIASHARA hoi
WANAFUNZI hoi

Sasa uchumi wa kati cjui mtz yupi anauona
 
Ingekuwa Tanzania ya Ulaya Magharibi, hayo mambo yangeiangusha CCM na kuisambaratisha kabisa. Ila kwa TZ ya kusini mwa jangwa la Sahara, CCM mbele kwa mbele
 
mawazo yako ni uharo mtupu, hakuna chama chenye ubavu wa kupambana na CCM kwa sasa ikizingatiwa kwamba vyama vya upinzani Tz ni vyama maslahi vinavyoendeshwa kifamilia kama chadema,udp,tlp nk.JPM kwa sasa anakubalika balaa hakuna cha membe wala lissu hata wenyewe wanalijua Hilo ni ukichaa tu unawasumbua
Rubbish
 
Pole mkuu...
Ukatili wao unafahamika na wananchi! Hata traffic police. Miye mwenyewe nnayo video clip, nilipigwa na traffic! Tena wakati anawatrain vijana ndani ya ofisi na mkuu wao akiwa ofisini. Naikumbuka namba yake na walinitesa na kunitisha kuwa wanafahamiana na Siro! Maana nilenda hospital kupatiwa matibabu! Hii serikali ni ya kikatili sana kama rais hafahamu!
 
Sisiemu haitamalizwa kwa haya mambo wala sanduku la kura...
Wenye kuelewa hayo mambo hawajazaliwa...
 
Back
Top Bottom