Uchaguzi 2020 Haya ndio yatakayoiangusha CCM kwenye uchaguzi 2020

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,322
Sitaelezea kwa undani lakini pamoja na nguvu ya dola CCM wenyewe wanajua hali si shwari.

Zaidi sana kuna mambo ambayo hawajui yanafuta nyaso zao za mambo makubwa ambayo wameyafanya kwa wananchi.

Mambo hayo ni kama yafuatayo kulingana na tabutupu media group (TMG)

1. Ukatili wa baadhi ya Wakuu wa Wilaya na mikoa juu ya Wananchi wasio na hatia.

2. Ubaguzi wa wazi kisiasa

3. Kauli za viburi na majigambo kwa baadhi ya viongozi

4. Mishahara ya wafanyakazi kuzimia toka 2015 bila kuamka hadi leo

5. Unyanyasaji wa TRA

6. Rushwa ya kununua viongozi wa upinzani.

7. Wizi wa kura serikali za mitaaa.

8. Hali mbaya ya maisha

9. Kutoajiri walimu graduates hasa masomo ya sanaa.

10. Mafao kuchelewa.
 
namna bora ya kuwa accomodate hawa wahamiaji ni changamoto kubwa!! kuna taarifa kwamba wahamiaji wanaweza kupita bila kupingwa majimboni - no kura za maoni kwa CCM.

Hili litafanya mgawanyiko mkubwa wa kambi za kampeni ndani ya chama!! ku practise demokrasia ni kazi nzito ndani ya CCM kwa sasa - wachache watacheka wengi wataumia.
 
Watanzania hata ukiwaweka kidole katika sikio bado CCM itapata kura. Hayo uliyoyaandika ni sahihi but si kwa Watanzania niwajuao mimi
Mtanzania ana pata kazi kama tarishi ofisini lakini ana matumaini kuwa kesho ni afadhali ya jana,kimiujiza?
 
Vipalata, nasikia baadhi ya maeneo vimewadodea kiasi ya kwamba wanaenda mpaka kwenye mabaa na mahoteli usiku kulazimisha wavinunue wakati hao ni waajiriwa na wala si wajasiliamali, Aibu.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Namba 9 ina nguvu kubwa sana ya kuimaliza CCM.

Hakuna mhitimu wa digrii ya Ualimu masomo ya Sanaa anafurahia kutokuajiriwa tangu 2015 alipohitimu Chuo Kikuu, hakuna!
Vijana hawa wamejiandikisha kupiga kura na wengine wameshachukua fomu kuwania nafasi za uwakilishi. Wataimaliza CCM mapema sana kuliko inavyotarajiwa.

Jambo pekee linaloweza kuibadili nia yao walau kwa asilimia kadhaa ni kuwamwagia ajira si chini ya 60,000 (Sitini Elfu) ili 'kuwamonyoa' (kuwamega) na kupunguza umoja wao lakini kama hali ndiyo hii... haki ya baba, atajamba moto.
 
11. Kuharibu soko zuri la mazao ya Korosho, ufuta, mbaazi na Mahindi kutokana na serikali kuingilia kati biashara ya haya mazao

12. Kuharibu uwekezaji na uchumi kupelekea watu wengi kusitishwa na kukosa kazi kutokana na makampuni mengi kufunga biashara na kuondoka Tanzania Mf Makampuni ya uchimbaji gesi mtwara, makampuni ya consultancy na kilimo pamoja na makampuni ya uuzaji wa bidhaa mbalimbali bila kusahau mabenki.

13. Kubambikia watu makesi na kufilisi watu kwa sababu za kisiasa
 
Back
Top Bottom