Haya ndio matokeo ya mwanangu darasa la saba nimefarijika sana

Kuna mtoto anaefeli darasa la saba miaka hii???

Kama mwanao yupo english medium schools na hana A hata moja basi huyo ni kiliza plus plus plus. Hamna changamoto yoyote na bado dogo afeli

Hata dogo awe kilaza namna gani matokeo yake lazima yawe njema kwenye hizo shule.
Nashangaa mnawadanganya watoto wenu mnakuja na kutudanganya tuliosoma pamoja...shule zetu form two nakumbuka ndio tulianza kusoma mwili wa binadamu wakati sasa hivi wanasoma watoto wa darasa la pili mpaka la Tatu nilikua naangalia daftari la mtoto wa Physics darasa la sita kipindi hiki ni Form two na miaka ile watoto wanasoma mambo ya Resistance wapo shule ya msingi harafu mnataka kudanganya watu kuwa nanyi mlipokua primary mlisoma mambo ya Resistance...
 
Kiswahili - A,
English - A,
Maarifa - B,
Hisabati - A...
Mama ana influence kubwa sana kwenye ubongo wa mtoto na intelligence yake na si baba , kwa kiswahili kisicho fasaha ni kwamba mtoto anarithi akili ya mama na si baba .
 
Kuna siku nilimkuta mwalimu akisahihisha mitihani.ya wanafunzi wake.

Utaishia kucheka.

Madogo hata kuandika Railway au Mosque hawawezi.

Hata Play ground inawashinda.
Sema vitabu vyetu vya sikili sijui kibanga ampiga mkoloni au Juma na Roza nao wakiviangalia watabaki kucheka tuu...
 
Kufauli san ni sawa mjenge ktk hali ya uwezo wa kumudu misingi ya MAZINGIRA yake na maisha
 
Kiswahili - A,
English - A,
Maarifa - B,
Hisabati - A,
Science - A,
Uraia - B,

Average Grade - A
Alafu miaka 15 mbele anakuja kua mchoma Chips maarufu kwenye Banda moja njiapanda ya kuelekea Gongo la Mboto km unataka kuelekea Kinyerezi kabla haujafika Stakishari,

Kuna dogo kapiga 1 form six kaenda Chuo na mkopo kapewa mzuri tu kamaliza Chuo Sasa hivi kazi anayoifanya ni kuvuta bangi tu hakuna kazi nyingine aliyonayo
 
Hiyo ni lugha tu ya watawala mkuu,kinachotakiwa sana ni skills,nenda hapo bungeni,aslimia karibu 90 ni hao unaosema zee zee,lakini ndio wanapiga hela mbaya....
Kwahiyo hao ambao hawajui lugha ndio wote watakuja kuwa wabunge.

Unatumia kipimo cha wabunge wengi kutosoma sana wakati hawafiki hata 400 katika nchi ya watu milioni 60.
 
Mshukuru Mungu Mkuu na endelea kumwombea kijana isije siku akakuletea boy friend.
 
Hongera sana japo kuanzia form four naona ndio kipimo sahihi but usiache kumpa motisha afanye vizuri mbeleni
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kiswahili - A,
English - A,
Maarifa - B,
Hisabati - A,
Science - A,
Uraia - B,

Average Grade - A

Amemaliza katika shule ya English medium

Mimi baba yake ni kichwa zaidi yake ila matokeo yangu hayakuwa mazuri Kwa sababu ya hali ya maisha magumu ya familia yangu

Ni kama vile nilikuwa najisomesha mwenyewe maana sare za shule na viatu nilivyo nunuliwa na wazazi ni zile nilizovaa siku napelekwa kuanza darasa la kwanza Baada ya hapo nilijinunulia mwenyewe Kila kitu hadi namaliza darasa la saba

Huko secondary na advance ndio kabisa nilikuwa nauza maji Ili kupata naurli ya shule na mahitaji mengine ada zote nimelipa Baada ya kumaliza advance ndio nakachukua vyeti vyangu ada ilikuwa elfu 20 Kwa mwaka lakini bado familia yangu ilishindwa kulipa

Ila bumu la chuo ndio lilinifariji na kunifanya nisome chuo bila ya stress

Ila elimu niliyoipata sio elimu Bora naamini hilo 100% Yani nilikuwa nafaulu tu Kwa sababu Nina akili nyingi

Nikajiapiza watoto wangu sitaki wapitie haya na sitaki wasome kayumba kama Mimi baba yao
ULIMBUKENE NA HAFIKI MBALI,,, PUMBAV
 
Muuza mchicha alieishia la Saba ni don kitaa kuliko graduates was chuo kikuu!!!
Tutajie jina la muuza mchicha don, maana madon wote wanajulikana. Au don kwako wewe ni kuwa na net worth gani? Yawezekana mmiliki wa Bajaj wewe unamuita don.
Tunatumia nguvu nyingi kufundisha elim isiyomkomboa mtoto kifikra!!

Sasa Hapo unafurahia A za mtoto no Hela hizo !!?yaani unafurahia ujinga was mtoto kukariri.badala kufurahia mtoto anaejua walau kulima nyanya na mchicha na kuuza bidhaa kitaa!!!?
Tuonyeshe mtoto wako wa darasa la saba, au wa ndugu yako au wa Mtanzania yeyote ambaye mtoto huyo amefanikiwa kwa kuuza nyanya au ni mmiliki wa shamba la nyanya na mkulima mzuri wa nyanya at that age, around 12yrs.
Subiri akimaliza chuo halafu arudi nyumbani Hana ishu ndio utaona mahela meengi uliopoteza hayana maana!!!
Wishful thinking. Huna evidence kwamba akimaliza chuo atakosa ajira au atakosa kujiajiri.
Na utueleze kama kusoma government ukibeba vidumu na mbolea ndio guarantee ya kuajiriwa ukimaliza chuo.
Nimesikitishwa na attitude Yako na wachangiaji ambao wengi nimeona ni vilaza was kufikiri!!
Kwamba wewe ni mjanja wa kufikiri. Kwa mawazo haya ya darasa la saba kuuza nyanya?
Kwa hio hizo A ndio zitakuja kumletea ugali mezani so ndio!!!?
Wapi uliona A zinaleta ugali.
Basi A hazitomletea ugali, ulitaka apate alama zipi ndio zilete ugali. B, C, D au F?
Mimi ni msomi graduate Tena sayansi nilikuja gundua elimu yetu ni ya kipuuzi Kwa sana!!!
Sawa elimu yetu ni mbovu, ila yawezekana hata wewe ni mpuuzi na hujijui. Kwenye hiyo sayansi yako unayojiita nayo msomi hukuwahi pata A, B, C?
Kwa maelezo yako hapo ulikuwa unatafuta ugali kwenye alama za ufaulu. Sasa kwanini usijilaumu na usione maisha ni magumu.

Mpaka sasa hujui maana ya elimu na ni graduate.
 
Mkuu hizo thamani za score na pesa ulizoweka vinalingana?

Mimi sitaki kukuvunja moyo lakini nataka ufikirie namna hii.

Je hapo alipo akimaliza anaweza kupata kazi? Kama umelipa ada let say milioni moja kwa mwaka je hayo matokeo yanaleta impact gani?

Hizo milions ungenunua ardhi akimaliza Form 4 atakuta ina thamani takriba milioni 50+

Then unawekeza pesa ndefu kwa mtoto ambaye akimaliza anakuja kutembeza bahasha kutafuta Mshahara wa Laki Saba?

Unless wewe ni Mlamba Asali and ofcourse Walamba asali ndio wanaosomesha shule za ghalama ila kwa sisi wavuja jasho ni bora tuwekeze kwenye biashara wapate cha kurithi baadae.

Hongera kwa Mwanao amezingatia masomo kwa bidiii na unatakiwa usimvunje moyo aendelee hivyo hivyo.
Hayo ni Mawazo ya kimasikini kwani kama ada ni million Kwa mwaka si inavunjwa vunjwa na kulipa kidogo kidogo ni kama tu matumizi ya kawaida
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Nashangaa mnawadanganya watoto wenu mnakuja na kutudanganya tuliosoma pamoja...shule zetu form two nakumbuka ndio tulianza kusoma mwili wa binadamu wakati sasa hivi wanasoma watoto wa darasa la pili mpaka la Tatu nilikua naangalia daftari la mtoto wa Physics darasa la sita kipindi hiki ni Form two na miaka ile watoto wanasoma mambo ya Resistance wapo shule ya msingi harafu mnataka kudanganya watu kuwa nanyi mlipokua primary mlisoma mambo ya Resistance...
Nilikuwa sekondari kitu kama form three shule ya serikali nikachukua madaftari na vitabu vya dogo yuko darasa la tano shule ya kawaida ya private. Humo nikaona TEHAMA wanayofundishwa inaridhisha kuliko niliyofundishwa sekondari.

Nikaja chuo nikakutana na jamaa kutoka Simiyu wanasoma kozi na rafiki yangu, IT. Wao hawakuwahi kuishika laptop mpaka wanafika chuo. Alafu chuo wakaenda kusoma IT, my friend, walidisco. Na kuna jamaa nilisoma nae A level alipata I ya 8 PCM akaenda UDSM kusoma Computer Science kadisco. Yeye kwao Kigoma hajawahi shika PC mpaka chuo.
Na nina best friend alipata I ya 8 hivyohivyo akaenda Computer Engineering, huyo aliishi na ndugu ni mwalimu shule za msingi private. Kaanza kuishi na computers akiwa mdogo shule na nyumbani, akapata passion ukouko mpaka tunafika A level yeye kwa muda wake alishajisomea languages mbili. Alimaliza chuo kapiga interview moja tu kaitwa kazi kampuni kubwa ya mawasiliano.

Sasa jichanganye sikiliza ushauri wa watu humu kwamba mwanao darasa la saba alime nyanya.
Nimesoma shule za kayumba na hunambii kitu, classmates wangu wa A level na chuo waliosoma private ndio wanaongoza kukimbiza kimaisha mtaani baada ya chuo.

Mtu kasoma shule haina alumni wa maana unategemea nini? Shule wazazi wanapigana kwenye vikao wakijadiliana watoto wale au wasile shuleni, hapo kuna mgomo wa kuchangia mahindi.
 
Back
Top Bottom