Je, inawezekana Prof Lipumba 'alitumwa' ku-test public mood kuhusu kuongezwa kwa muda wa urais? Kwa upande mwingine Rais wa Jamhuri wa Muungano akishapatikana chini ya katiba mpya , hawezi kusimamia mchakato wa katiba ya Tanganyika? Au Tanganyika haiwezi kuunda serikali ya mpito kusimamia uundwaji wa katiba yake?Nina Mawili kuhusu JK1. Nasubiri atangaze kusimama kwa muda kwa mchakato wa katiba ya Muungano na atangaze kuanza kwa mchakato mpya wa katiba ya Tanganyika kwanza ili tukishapata katiba ya Tanganyika ndipo tuje tuendelee na mchakato wa hii katiba ya Muungano.2. Naanza kuhisi kuwa Prof. Lipumba was right kuwa JK ataongezewa muda wa kukaa madarakani na hataondoka 2015 sababu lazima mchakao uchukue muda mrefu kuliko ilivyodhaniwa. Mchakato wa katiba ya Tanganyika haujaanza na haijulikani utaanza lini ukizingatia kuwa lazima tujue namna gani tutakuwa na Bunge la Bara, Rais wa Bara, Mfumo wa mahakama wa bara na mengineyo mengi.Just thinking aloud!