Haya ndio maisha Mazuri, na hakuna Mengine

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,573
Maisha mazuri ni yapi?

Kutumikia tamaa za mwili?

Kutumikia tamaa ya mwili hakuna faida ni hasara tupu, ukiwa mpenda kubadili wanawake kila siku, unatambua hasara zake, mfano mdogo tu, ukipata magonjwa ya zinaa hasara yake hadi uzeeni unatambua vizuri.

haya mfano uwe mwizi, hivi siku ukishikwa hiyo aibu na Kipondo kitakacho kuhusu utajisikiaje?

Ukiona umependa sana mambo hayo jua basi una roho ya shetani ndani yako na si wewe peke yako unatenda hayo, na ukibaki hivo, jua wazi hukumu Inakuja.

Basi twende kisomi kabisa. Kunywa pombe nyingi kupita kiasi ni hatari kwa Afya yako, nani anataka kuwa mtumwa wa Pombe? hivyo hivyo hata kuvuta sigara, kama ipo dawa ya kuondoa kiu ya Sigara ni wangapi watatumia dawa hiyo?

Ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa usio tibika, Nenda kaangalie unasababishwa na nini.

Hili ni andiko la Biblia.
Note: Utauwa- means (Maisha ya kupenda kutenda mema)

1 Timotheo 6:6-11

[6]Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
[7]Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
[8]ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
[9]Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
[10]Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
[11]Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole.


Jambo kubwa la pili ni kuwa na kiasi (Too much is Harmful)
Neno kubwa ni 'Haki'

Maisha mazuri ni Kupenda haki, hata katika Siasa, Neno haki linatamkwa, mashule, kazini hata watu wasio mjua Mungu hutumia neno haki.

Kupenda haki kutakuepusha na Mengi na hiyo ndio siri pekee ya maisha Mazuri na wala hakuna sheria itakayo kufunga ukiwa mpenda haki.

Usifanye jambo ambalo hata wewe mwenyewe ukifanyiwa huwezi jisikia vizuri.

Ukiona upendi haki jua kuna roho za kishetani zimekuingia ndani yako na unatakiwa utafute msaada.

Mtu asikuvuruge na sheriaaa nyingiiiii ety Usiuwe, usizini, usiseme uwongo, mala ishike sabato, mala Toa zaka.

Hizo sheria hazikufungi kwa lolote wala kuzishika sheria hakuna malipo yoyote.

Lakini kupenda haki kutakuepusha na matatizo mengi hapa duniani, kama vile uzima wa kiafya kwa kula chakula cha Afya, Kupendwa na watu hata kama si tajiri, kuwa mchapa kazi, na utaipenda familia yako na kuwa mvumilivu.

Ni Hayo tu.

Tukutane Jukwaa la Dini, Tuelezane ni Ipi Tiketi ya Kupata Uzima wa milele.

Wagalatia 2:16

hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria,
 
Mtazamo wako na uko sahihi! as long as huingilii haki za wengie, basi ni haki yako kuchaga ukipendacho
 
Tuambie, nawe mtizamo wako?
Dhamira yangu ndiyo msimamo wangu as long as siingilii haki za wengine!
Tatizo lako you believe in Life after life on earth! Life after Africa aliyoisema Achebe katika Trial of Christopher Okgbo!
 
Dhamira yangu ndiyo msimamo wangu as long as siingilii haki za wengine!
Tatizo lako you believe in Life after life on earth! Life after Africa aliyoisema Achebe katika Trial of Christopher Okgbo!
Huwezi kutengenisha Dhamiri Njema na Kupenda haki.

kuhusu kuamini maisha baada ya Kufa kusitutenganishe ndugu.

Je wapenda Dhamiri Njema maishani mwako au Umebeba hadi Dhamiri ambayo hata nafsi yako inakusuta kuwa si njema?.
 
Back
Top Bottom