Haya mambo 30 yanayonisumbua sana, sijui wewe

Haya mambo 30 yanayonisumbua sana, sijui wewe

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,762
Reaction score
4,978
Katika mambo yanayonisumbua maisha yangu, mambo haya 30 yanaongoza;
1. Kila kitu ni kitapita au ni cha muda tu ukiwemo uhai au maisha yangu.
2. Ukweli kuwa sitoridhika na nilichonacho au niliyonayo mpaka wakati wa kufa
3. Uhalisia kuwa uchu ndiyo unaotawala uchumi na uchumi nao kutawala uchu.
4. Kuwa na marafiki wengi siyo uhakika wa furaha
5. Ukweli kuwa marafiki wa karibu ndiyo watakaonikimbia wakati wa changamoto
6. Pesa siyo kila kitu ila kila kitu kinahitaji pesa.
7. Kila mtu ni mbinafsi ila huifanya kazi isiyo na tija ya kuuficha.
8. Ulimwengu unavyofundisha mtu kujithamini kwanza kabla ya kuwataka wengine wamthamini.
9. Hakuna ajuaye yatakayotokea au kesho (wakati ujao)
10. Kamwe huwezi kuelewa mafanikio kama hujaionja ladha ya kutofanikiwa.

11. Unatafsirika kwa kile unachojua na siyo kile unachomiliki.
12. Kufanya ni vizuri kuliko kufikiri.
13. Kusamehe ni sawa kuupanda mlima mkubwa.
14. Maisha unayoyataka kuyaishi yanatafsiriwa na wewe.
15.Baadhi ya watu siyo wa kiwango chako, na wengine hawakuumbwa kuwa rafiki zako.
16. Kuna wakati mambo mabaya yanawapata watu wazuri.
17. Elimu siyo ufunguo wa maisha ila matumizi ya Elimu ni ufunguo wa maisha.
18. Serikali kwa asili yake haikuundwa kukupa unachotaka ila kuchukua ulichonacho.
19. Tamaduni na imani nyingi huwapotosha watu ila ni jukumu la mtu mwenyewe kuchagua au kuunda utamaduni na imani yake.
20. Watu wanaokuzunguka ndiyo wanaokutafsiri, wanachokifikiri, wanachosema au wanachokiamini hukuathiri na wewe.

21. Mawazo hasi huyashinda mawazo chanya kwa wingi lakini mawazo chanya hushinda mawazo hasi kwa uzito.
22. Fikra chanya ni kama mto unaopita kwenye miamba na milima.
23. Ujinga ni ugonjwa unaiba maono ya watu.
24. Mbuni anayejificha kwa kuchimbia kichwa chake mchangani ni sawa na watu wawili wanaojihusisha katika mahusiano ya kimapenzi kijinga kwa kupuuzia wengine kuwa wanawaona.
25. Umasikini wa fikra ni mbaya kuliko umasikini wa ukosefu wa mali.
26. Kusimamia maono yako ni kazi ngumu kuliko kulaumu.
27.Kaa mbali na wambea, hawawezi kufurahia ukifanikiwa.
28. Usifikiri mawazo duni, waza mawazo makubwa. Muumbaji alituumba hivyo.
29. Jiamini kwanza kabla ya kuwaambia wengine wakuamini.
30.Usiyachukulie maisha yako kirahisi kuna watu wanaota kuwa kama wewe.

Kuna rafiki ameongezea hapo chini kuwa upo msemo " USIKATE TAMAA NA WAKATI HUO TUNAAMBIWA TAMAA MBAYA"
 
Back
Top Bottom