Haya Majina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya Majina

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Afrika Furaha, Jan 7, 2011.

 1. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu Google haya majina halafu nipe feedback:
  1.Andrew James Tice (Canada)
  2. Gopalakrishnan Balachandaran (India)
  3. Hon Sung Woo (Singapore)
  4. Guy Picard (Canada)
  5. Sulaiman Al Adawi (Oman)
  6. Stanley Munai (Kenya).
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Feedback: Wanamuwakilisha ROSTAM AZIZ
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  what !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:crazy::crazy::crazy::crazy: is it wat I see is wat I get?:attention::attention::attention::hail::hail::hail:
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wamefanyaje?nimejaribu kufanya kama ulivyosema lakini naona kila mmoja ana historia tofauti na mwenzake!kulikoni!!
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Ndugu,
  Hawa ndio Ngeleja atawapa cheki ya DOWANS bila riba
   
 6. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Eti ndo wamiliki wa Dowans
   
 7. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi ninachojiuliza, mbona wamechelewa sana kuwataja hao wamiliki wa Dowans???? Mi siamini kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
  sio hawa!!
  Wapo humu humu Tanzania, tena ktk Sirikali
   
 8. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #8
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali yakubali kulipa 94 bilioni Dowans Send to a friend Thursday, 06 January 2011 20:03 0digg

  [​IMG]Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja

  Raymond Kaminyoge
  SERIKALI imeamua kuilipa kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Sh 94 bilioni kama ilivyoamuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kuwataja wamiliki na wakurugenzi wa kampuni hiyo ambao wote si Watanzania.

  Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wake na waandishi wa habari.Alisema Sh.185 bilioni zilizokuwa zikitajwa kwenye vyombo vya habari ndizo ambazo kampuni ya Dowans iliiomba ICC ilipwe fidia kwa Tanesco kwa kukatiza mkataba walioingia wa kufua umeme, lakini mahakama iliafiki ilipe dola 65 milioni za Marekani.

  Alisema fedha hizo zitalipwa baada ya pande hizo zitasajili uamuzi huo katika mahakama kuu.

  " Serikali tumekwishaamua kuwa tutailipa Dowans dola za Marekani 65 milioni, kama ilivyoamuliwa na ICC ambazo ni sawa na Sh 94 bilioni, kuchelewa kuwalipa kutatufanya tulipe riba ya asilimia 7.5," alisema.

  " Siyo kwamba kiasi tunachotakiwa kulipa ni kidogo, ila tumeona ni muhimu Watanzania wakafahamu kiasi halisi ambacho tunatakiwa kuilipa Dowans," alisema.

  Alisema wameamua kulipa baada ya mwanasheria mkuu wa serikali, kusema kuwa hukumu hiyo ilikuwa halali na kuipinga kungeizidishia serikali gharama.

  "Mwanasheria mkuu wa serikali ameshauri kutekeleza uamuzi wa mahakama ya usuluhishi endapo uamuzi huo utasajiliwa katika mahakama kuu ya Tanzania," alisema Ngeleja.

  Aidha Ngeleja aliwataja wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, na hisa wanazomiliki katika mabano kuwa ni Dowans Holding S.A ya Costa Rica (81) na Portek Systems and Equipment (PTE) LTd (54).

  Aidha Waziri Ngeleja huku akirejea barua ya Wakala wa Usajili wa Kampuni (Brella), aliwataja wakurugenzi na nchi wanazotoka kuwa ni Andrew James Tice (Canada) na Gopalakrishnan Balachandaran (India).

  Wakurugenzi wengine kwa mujibu wa Waziri Ngeleja ni Hon Sung Woo (Singapore), Guy Picard (Canada), Sulaiman Al Adawi (Oman) na Stanley Munai (Kenya).

  Kiini cha sakata hilo kilianza mwaka 2006, wakati Tanesco ilipoingia mkataba wa mauziano ya umeme wa Tanesco na kampuni ya Richmond Developmen LLC.

  Miezi sita baadaye mkataba huo ulihamishiwa kwa kampuni ya Dowans Holdings ya nchini Costa Rica na baadaye kwa Dowans Tanzania Ltd,
  Wakati wa utekelezaji wa mkataba huo, ilizuka hoja kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo wabunge kwamba mkataba baina ya Tanesco na Richmond haukuwa halali kisheria hivyo usingeweza kurithiwa na Dowans.

  Suala hilo lilizua mjadala mkubwa hali ambayo Tanesco kwa kuwatumia mawakili wa kampuni ya Rex Attorneys ya jijini Dar es Salaam walivunja mkataba huo.

  Baada ya kuvunjwa kwa mkataba huo, ndipo kampuni hiyo ikalipeleka suala hilo ICC kama walivyokubaliana na Tanesco kwenye mkataba.
  Uamuzi huo wa ICC ulizua mjadala katika siku za hivi karibuni baada ya viongozi wa serikali kutofautiana kuhusu kuilipa kampuni hiyo au kutoilipa.

  Wakati Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Samwel Sitta, akiitaka serikali kutolipa Dowans kwa kuwa kufanya hivyo ni uhujumu wa nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema akitaka kampuni hiyo ilipwe.
   
 9. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Utashangaa hakuna mtu hata mmoja wa majina hayo anayejua WHAT IS DOWANS . . ..
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Kuna waziri wetu alikuwa anagombea ubunge wa SADC na hajui hiyo SADC ni nini
   
 11. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mgombea mmoja wa CHAMA CHETU aliulizwa kirefu chake akajibu SOUTHEN DEVELOPMENT CLUB
   
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wamechakachua tu!
   
 13. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  FEEDBACK HII HAPA:

  1.AndRew James Tice (Canada)
  2. Gopalakrishnan Balachandaran (India)
  3. Hon Sung Woo (Singapore)
  6. Stanley Munai (Kenya).
  4. Guy Pic(a)rd (Canada)
  5. Sulaiman Al Adawi (Oman)

  CASE SOLVED!
   
 14. S

  SUWI JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hahahahhahahhhhh!!!!!!!!!! Kaaazi kwelkwel.... TZ bana!
   
 15. Afrika Furaha

  Afrika Furaha JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahahahahahahahahah
   
Loading...