Haya majanga: Nyoka kuwafanyia massage binadamu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,388
2,000

Ukisikia maajabu makubwa ambayo hufikirii kukutana nayo hapa duniani hii ni moja wapo, Kuna mbuga moja ya kufugia nyoka wakubwa inatoa huduma ya “massage” kwa binadamu kwa kutumia nyoka hao “giant pythons” lakini kabla ya kuanza zoezi hilo nyoka hao hulishwa kuku ambao idadi yao hufikia 10 ili wasije kusikia njaa katikati ya shughuli hiyo.

Nyoka hao wana uzito wa kilo 250 na mtu anayefanyiwa massage anaweza kupiga kelele au hata kupumua bila nyoka hao kufanya chochote.Unaweza usifikirie kama kuna kitu kama hiki kinafanyika lakini mbuga hii iliyopo katika mji wa Cebu nchini Ufilipino inapata wateja wengi sana wakipanga foleni kusubiri huduma ya kukandwa mwili “Massage” ambayo hutolewa bure lakini kwa wanaoweza tu kuhimili mikiki yake.


Nyoka hao wakubwa wanne waliopewa majina ya Michelle, Walter, EJ and Daniel hutolewa nje kutoka kwenye eneo wanapofugwa na kuwekwa juu ya mtu anayetaka huduma huyo wakati mtu huyo akiwa amelala chini kwenye kitanda maalum karibu na lango kuu la kuingilia katika mbuga hiyo.Watu wengi wanashangazwa na mbuga hii na huduma inayotolewa sasa jiulize unaweza kufanya hivyo hata kama una uchovu kiasi gani?Credit: Millardayo
 

Attachments

 • nyoka 1.jpg
  File size
  29.1 KB
  Views
  2,292
 • nyoka 2.jpg
  File size
  39.8 KB
  Views
  2,025
 • nyoka 3.jpg
  File size
  34 KB
  Views
  2,038
 • nyoka 4.jpg
  File size
  31.9 KB
  Views
  1,950

PrN-kazi

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
2,894
1,225
hmmm!!!, labda;kama hakuna kamchezo kakina Jet Li, ngoja tusadiki hivyo.
 

bysange

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
4,432
2,000
kwenye picha tu nawaogopa,atakaye nipeleka hapo anipige kwanza ile nusu kaputi.
 

mwallu

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
6,787
2,000
labda kwa lazima
tena nitaomba wanidunge sindano ya usingizi kabla ya tukio
 

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,328
2,000
Kuwaona tu katika picha mwili unanisisimka namna hii, je nikiwaona live si nitakufa kabisa...!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom