Hili sio tatizo la madereva, polisi wala nani; Hili ni tatizo la Watanzania wengi - KUTOKUJALI, hakuna anayejaji juu ya usalama wa mwingine, afya ya mwingine, haki ya mwingine, na mengineyo. Tunaweza kuwalaumu madereva barabara, lakini na wewe unajali juu ya wengine katika eneo lako la kazi au hata biashara; labda wewe ni daktari, hakimu, mwalimu, au taaluma nyingineyo. Hatuna utamaduni wa kufikiri zaidi juu ya wengine, badala yake tunajifikiria zaidi wenyewe katika nafasi zote kuanzia ngazi ya Taifa hata katika familia zetu (UBINAFSI NDIO UNAOTUMALIZA).
Nimekuwa nikifuatilia sana mambo ya usalama katika vyombo vya usafirishaji, wenzetu wako mbali sana na ethics kubwa inayowafanya kuwa huko ni KUJALI JUU YA WENGINE, mfano inapotokea ajali; uchunguzi unakuwa wa kina sana kubaini tatizo ili ajali ya namna hiyo isitokee tena. Wanajali sana viwango vya uendeshaji na vyombo vinavyotumika.
Nimekuwa na proposal juu ya uendeshaji wa mabasi ya abiria, nimejaribu sana kupenyeza wazo langu kwa baadhi ya wamiliki wa mabasi ya abiria lakini naona wanaridhika zaidi na faida wanazopata kuliko kufuata matakwa ya abiria na usalama wao. Wenzetu wanakuwa ni kitu kinaitwa code of practise, ikiwa ni madereva na wahudumu lazima waendane sawa na taratibu zilizowekwa na kampuni husika ambazo zinaendana na sheria na kanuni zilizowekwa na serikali. Halafu kuna taasisi ambazo ni watch dogs, wanahakikisha uendeshaji wa huduma za usafirishaji zinaendana sawa na matakwa ya abiria kwa upande wa usalama na mambo mengineyo. Kwetu hapa hakuna anayejali, hizi sheria na kanuni zinazotungwa zimekuwa zikitumika kama mtaji wa watendaji kama polisi katika kujinufaisha.
Kwa kweli tupo katika giza nene kwa sababu kila mtu anashughulika na mambo yake binafsi, bila kujali wengine. Kilichobaki tuendelee kumuomba Mungu atuletee MASIHI kama ilivyokuwa kwa wana wa Israel walipokuwa misri kama watumwa hatimaye Mungu aliwaletea mkombozi (MUSA). Sijui na sisi MUSA wetu atakuja lini, lakini naamini wakati upo ambapo Mungu atatuletea MUSA kuja kututoa katika dimbwi hili la utumwa. Kwa sasa hatuna tofauti na watumwa kwani hatuishi kama tutakavyo, bali wachache wamekuwa wakituburuza na hakuna anyetoa mwelekeo wa kutufikisha Kaanani yetu.